Je, Ni kweli tunawahitaji zaidi ya wanavyotuhitaji?

Je, Ni kweli tunawahitaji zaidi ya wanavyotuhitaji?

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
Kauli ya kusema kuwa watu wa nje tunawahitaji kuliko wanavyotuhitaji imetamkwa kwa zaidi ya mara moja na Rais Samia Suluhu. Kauli hii inashida kidogo na tunahaja ya kuhakiki kama ni kweli kuwa tunawahitaji kuliko wanavyotuhitaji

Ili kuangalia namna tunahitajiana ni muhimu kwanza kuangalia vitu ambavyo sisi tunafaidi kutoka kwao ukilinganisha na vitu wanavyofaidi kutoka kwetu. Mataifa yaliyoendelea yana rasilimali fedha na teknolojia, huku taifa kama Tanzania likiwa na mazingira mazuri ya biashara, cheap labour, madini, gesi, mbuga za asili, wanyama nk. Eeekh! Hadi hapo tunaweza sema tunavyo vingi ambavyo wao wanavihitaji huku sisi tukihitaji fedha tu kutoka kwao kwa kuwa suala la teknolojia hatuna muda nalo(Lingekuwepo suala la Leap frogging kwenye uchumi lingetokea zamani sana)

Hivyo basi nadhani kauli sahihi kusema ni kuwa tunahitaji fedha zao. Lakini hata kama tunasema tunahitaji fedha zao tusisahau maneno ya Rais Nyerere kwenye azimio la Arusha kuwa anayeweka hela ndio anayechagua wimbo, ambapo alipinga suala la kutegemea fedha za nje na kuweka kuwa ili tuendelee hatuhitaji hela bali tunahitaji watu, ardhi, siasa safi, uongozi bora

Kauli ya Rais Samia inaonesha kuwa kwa sasa sisi tunahitaji fedha, and only money, sio watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora kama ambavyo misingi ya maendeleo inahitaji.

Fikra hizi ndio zinafanya tukose hata nguvu ya kubargain katika masuala ya kimataifa kisha kupata hasara za kudumu na resource curse mbali na kuwa na vitu vingi ambavyo wao wanavihitaji na tungeweza kuvitumia kujipatia faida

Signed
OEDIPUS
 
Wewe ni maskini ,nchi yako ni maskni na huwezi kujitegemea ...!

Jiwe aliforce kama wewe kuwa na akili mgando ,ameambulia kukopa trilion 29
 
Wewe ni maskini ,nchi yako ni maskni na huwezi kujitegemea ...!

Jiwe aliforce kama wewe kuwa na akili mgando ,ameambulia kukopa trilion 29
Pumba.....v...u!!!

Hao wanaotukopesha wanatupa za bule?

Kama kigezo nchi yetu masikini, ni kina Nani ni matajiri na hawakopi,?

Halafu ukome kusema nchi yetu ni masikini, utajiri wote ulio ktk nchi yetu utasemaje ni nchi masikini

Tofautisha umasikini wa mtu na nchi jinga wewe
 
Wewe ni maskini ,nchi yako ni maskni na huwezi kujitegemea ...!

Jiwe aliforce kama wewe kuwa na akili mgando ,ameambulia kukopa trilion 29
Bahati mbaya haujasoma kuelewa hoja umekuja kujibu. Lakini tuende hivyo, Je, ni kweli tunawahitaji kuliko wanavyotuhitaji?
 
Kauli ya kusema kuwa watu wa nje tunawahitaji kuliko wanavyotuhitaji imetamkwa kwa zaidi ya mara moja na Rais Samia Suluhu. Kauli hii inashida kidogo na tunahaja ya kuhakiki kama ni kweli kuwa tunawahitaji kuliko wanavyotuhitaji....
Kwa uchache na kukusaidia, Kila kitu mnacho rasilimali zote, tangu gesi, mafuta, madini, upepo, maji, jua, ila vyote hivyo kama taifa havijaweza kuwa msaada kwa taifa bila usaidizi wa tunao wahitaji kuliko wanavyotuhitaji, kwanini na sema hivyo, najua utasema tuu matajiri, ila jua kuwa, kama ni umeme wenzetu wanauwezo wa kuzalisha Kwa uranium, mafuta yetu, gesi, vimedoda, nguo za ubora tunaenda kwao.

Pamoja na kijigamba uchumi wa viwanda tuangalie ubora wa bidhaa, na gharama za uzalishaji, hapo tutajua hatujui, je kwa namna hiyo kwanini tusiwahitaji.. Yote hayo kawaida saana, tuje kwenye science na tekelinalowajia hapo Bado hatuwahitaji zaidi ya wanavyotuhitaji, tumelala usingizi wa pono maeneneo hayo. Je nani anae mhitaji mwenzie. Au ndio tuseme tuko kwenye raiti tiraki🤔.
 
Back
Top Bottom