Je, ni kweli ndugu ukiwasaidia wanahisi unavimba? Nini sababu yako kuhisi hawakutakii mema?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,516
27,007
Wakuu, salaam!

Kumekuwa na nyuzi nyingi humu watu kulalama kuhusu ndugu zao, ndugu hivi mara ndugu vile... yaani ndugu lawama.

Binafsi sikuwahi kuwaza katika picha hiyo, ila baada ya kusikia stori za hapa na pale nikaanza kuunganisha nukta nikajikuta naanza kujenga chuki kwa ndugu.

Je, hii inaweza kuwa sababu ya baadhi ya watu kutojenga kwao licha ya kufanikiwa huko mijini?

Je, kuna ukweli kiasi gani kwamba wanaojenga kwao ni kwa hofu ya kuaibika pindi yatakapowafika?

Karibuni.
 
plan yako hiyo nyumba akae nani?

Kwetu kijijini, ni kwenye uwanja wa familia... of course nimejenga kutia heshima ili alama ibakie pale.

Mdogo wetu ataishi pale, na hata mimi ninapokuwa naenda likizo nikisema niende kwetu naenda pale... dogo aliyebaki pale ndo mkazi rasmi.
 
sio mbaya wala sio kitu kibaya achana na hao wanaolalamika
 
Ukijenga nyumban kwenu bila au hata kwa makubaliano jiandae kisaikolojia kwa lolote,migogoro isiyo na kichwa wala miguu,lawama,kuambiwa unataka kudhulumu ndugu zako kiwanja n.k

Jenga kwastyle ya kutoa msaada bila kusubiria shukrani. Hapo inajumuisha na wewe kujipa chumba au sehemu ya kufikia ulipojenga.
 
Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo....huyo blaza alitamani hiyo pesa ungempa ajikwamue zaidi.
Lakini mpango wako ni tofauti na mawazo yake. Fanya vile vikupendezavyo,huwezi kuwaridhisha watu,na Kama hutajali hifadhi hii_____baada ya muda nyumba itapata wakazi wengi tu,na watadai wanahaki nayo maana wewe ni mdogo wao.
BTW inakatisha tamaa lakini lazima tuendelee kutenda mema.
 
Umenena vyema mkuu👏
 
Unapotaka kufanya kitu au Jambo kwenu au kwa wazazi wako uwe makini sana.
Hili lililokupata ni la kawaida. Tena huenda ni dogo mno kulinganisha na mengi yanayotokea au yanayofanywa na ndugu.
LA MUHIMU:
Unalowahudumia wazazi wako au unapofanya jambo kwenu, usiwaze sana kuhusu ndugu zako.
Jione kama ulizaliwa peke yako. Ukiwashirikisha wakakuunga mkononi jambo la kumshukuru Mungu.
Wakikutosa, usipoteze muda wako kulalamika au kuwalaumu na Hata kuwabembeleza.
Chapa kazi. Songs mbele. Jione wewe ulizaliwa peke yako.
Pole sana rafiki.
 
Back
Top Bottom