Je Ni Kweli IPP Inaghushi Bidhaa Za Urembo?

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,070
4,105
Ukienda kwenye masaluni na maduka ya bidhaa za urembo unakuta makopo yanafanana na bei zimetofautiana.
Ukiuliza unaambiwa hii ni original na hii nyingine ni ya ipp.
Swali langu ni kutaka kujua kama kweli viwanda vya ipp vimekuwa vikighushi vidhaa za nje?
Kama ni kweli wanaghushi bidhaa hizo, bodi ya chakula na dawa wana taarifa? Je wamechukua hatua gani kuokoa afya za watumiaji wa bidhaa hizo?
 
Mbona umerukia huko kwenye kutengeneza bila idhini? Ungeuliza kwanza kama wanatengeneza kwa idhini (under license) au la. Kwa sababu pia wanatengeneza (au walikuwa wanatengeneza) bidhaa za Colgate-Palmolive chini ya idhini
 
Kugushi sounds very criminal. Nadhani fanya utafiti /tafuta ukweli kwanza kabla ya kutumia neno baya kwa kampuni kubwa kama ipp. ushauri wa bure
 
Kwani IPP bado wana kiwanda cha aina hiyo kweli? Nilidhani walikachana na hiyo biashara siku nyingi.
 
Siyo feki, ila ndiyo original ya IPP. unless kama walilenga katika kughushi.
 
Hata mie nilishasikia maana ni mteja mkubwa wa sabuni za Protex na dettol, sasa kuna nyingine ukinunua povu lake haliwi soft kama zile za Kenya au South Africa ukiuliza mwenye duka utaambiwa za Mengi hizo, sasa sijaelewa jamaa ana fanya za kichina china au vipi?
 
Ukienda kwenye masaluni na maduka ya bidhaa za urembo unakuta makopo yanafanana na bei zimetofautiana.
Ukiuliza unaambiwa hii ni original na hii nyingine ni ya ipp.
Swali langu ni kutaka kujua kama kweli viwanda vya ipp vimekuwa vikighushi vidhaa za nje?
Kama ni kweli wanaghushi bidhaa hizo, bodi ya chakula na dawa wana taarifa? Je wamechukua hatua gani kuokoa afya za watumiaji wa bidhaa hizo?
Je Ni Kweli IPP Iinajishughulisha na Bidhaa Za Urembo?
 
Uzushi mwingine unatia kinyaa...hasa ukiwa unazushwa na majina ya watu wanaoonekana kuwa na busara... Kwanza bidhaa zinazozungumziwa mbona hazitajwi kwa majina!!! Ila kwa taarifa IPP ilishaacha biashara ya kutengeneza bidhaa za urembo zaidi ya miaka mitano iliyopita, na kampuni yake ya Bodycare ilishauzwa kwa wawekezaji wengine ambao nao walishaacha uzalishaji.
 
Ni uzushi ulioenezwa toka miaka ile wakati IPP watengeneza mafuta ya bodycare.Kipindi hicho nilikuwa nauza duka, na kila mteja akija kununua cream,lotion au mafuta ya kujipaka anakuuliza kama ni original au ya Mengi!.Nilikuwa napata kazi ya kuwaelesha kwa sababu nilikuwa na details za bidhaa zote za bodycare.Hawakuwa wakitengeneza cream wala lotion hizo feki.
 
Back
Top Bottom