Je, ni kweli hii!

Je, ni kweli hii!

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,374
Reaction score
38,248
Naskiliza Radio hapa ndani ya MWENDOKASI, mtangazaji wa AE, anaizungumzia Korea Kaskazini. Anasema KK kule hakuna huduma ya "international calls" simu za kutoka!

Pia akeandelea kusema eti, serikali ndio yenye mamlaka ya kuamua nani akae Mjini. Yaani mtu hawezi kujiamulia tu akae Mjini!

Tuelimushane Jamani!
 
Yote hayo mawili ni kweli.Korea kaskazini ni jehanam!Hii picha hapa ni mji mkuu pyongyang mchana.Fikiria mwenyewe kwa nini barabara za mji mkuu ni tupu mchana. Hii inawezekana kwa mji mkuu kama dar au nairobi?
North_Korea-2011-275_new.jpg
 
Yote hayo mawili ni kweli.Korea kaskazini ni jehanam!Hii picha hapa ni mji mkuu pyongyang mchana.Fikiria mwenyewe kwa nini barabara za mji mkuu ni tupu mchana. Hii inawezekana kwa mji mkuu kama dar au nairobi?
North_Korea-2011-275_new.jpg
duh! na zile tamthilia zao inakuwaje?
 
Drama ni kk kwa maana ya Korea kusini ambao tulikuwa sawa nao kwa ngazi ya maendeleo miaka ya 1960s ila Leo wao wako first wold na GDP ya juu sana , sisi bado tuko third world na GDP ndogo sana. Walipata kiongozi mwenye vision akaongoza kwa miaka 30 ndiye aliwafikisha hapo ila aliwanyima Uhuru wa kutoa maoni hakukuwa na demokrasia hata kidogo.

Baada ya kustaafu akasema anajutia kuwanyima wananchi Uhuru Wa kutoa maoni ingawa baada yake Korea kusini kuna demokrasia ya hali ya juu. Hats rais anaweza kushitakiwa akifanya madudu. Lakini mbona nchi nyingi hazina democrasia lakini kimaendeleo zinachechemea .wao ni mabepari.

Sasa ukienda Korea kaskazini wao ni wajamaa hadi Leo ila maendeleo yao ni shida .Kaskazini anatawala yule Kijana mkorofi baada ya kurithishwa toka kwa babu na baba .laiti kuongoza muda mrefu ingekuwa ndio maendeleo basi kaskazini wangekuwa zaidi ya kusini maana maana tangu 1950s wanatawala ukoo Wa KIM IL SUNG babu, KIM JONG IL Mtoto , na sasa ni KIM JONG UN mjukuu, Mambo yao ni ovyo.

Wanatengeneza zana za nuclear nja kila mwaka kwao ,pia wanashindwa hata kuwatibu wananchi minyoo ya tumboni. Hayo maendeleo ya vitu sio watu. Lakini kusini hawajishughulishi na nuclear . kusini ndio wana makampuni yanayotamba dunia nzima mfano SAMSUNG, DAEWOO ,KIA MOTORS NK. Korea zote zina somo kwa viongozi Wa Leo Afrika wanaotaka kuwaletea wananchi wao maendeleo halisi , sio maendeleo ya vitu. Kamchango hako kadogo kwa waliozaliwa hawajafikisha miaka 30.

Kiongozi aliyeiendeleza kusini ni LEE KUAN YEW kama sijakoea . Mwenye interest atagoogle amjue zaidi, lakini alikuwa dictator per se, Ndiyo benovelent dictator (dictator mwema anayeendeleza nchi) ? Asanteni.pia nimalizie kaskazini ni watoto pendwa wa Russia na China , wakati kusini ni watoto pendwa Wa marekani tangu cold war hadi leo. Bila hao yule dogo hawezi kukohoa kwa Marekani.

Ndiyondiyoyoy6ana Trump anaibana China kwa biashara na China ameanza kumbana dogo apunguze jeuri Tukumbuke Marekani ndiyo mteja mkubwa kwa biashara za China. Mpaka kiongozi Wa China akalalamika eti anaonewa akiwekwa vikwazo kwa makosa ya dogo.

Unajua bado Marekani bado anafurukuta ingawa Siku zake za ubabe ni chache mbeleni, kama China hatakwaa kisiki miaka kumi au ishirini ijayo.
 
Yote hayo mawili ni kweli.Korea kaskazini ni jehanam!Hii picha hapa ni mji mkuu pyongyang mchana.Fikiria mwenyewe kwa nini barabara za mji mkuu ni tupu mchana. Hii inawezekana kwa mji mkuu kama dar au nairobi?
North_Korea-2011-275_new.jpg
Kwa mwonekano wa kupendeza wa huo mji, unaamini kuwa ni Jehanamu?
Tatizo mnataka watu wote waishi kwa standard ambazo ameweka mzungu ndipo muone wana maisha mazuri
 
Back
Top Bottom