Je ni kosa? Naweza kufungwa?

sychellis

Senior Member
Oct 16, 2018
135
114
Habari wakuu, tangu wiki iliyopita natumiwa sms na bank moja hapa nchini wakiniambia laki tatu imeingia kwenye akaunti yako mara laki mbili imetoka mara laki na nusu imeingia, sasa nikawa nashangaa maana sina acount katika hiyo bank, nikahisi labda mwenye hiyo account atakuwa labda amekosea ameandika namba yangu.

Hivyo nikawapigia bank nikawaambia kwamba sina account na waache kunitumia sms lakini bado wakaendelea nikawapigia mara ya pili ila hali ikawa vilevile sms zinakuja.

Sasa majuzi wakanipigia simu wakaniambia kuhusu Mobile Bank kuunganisha account ya bank na simu ambapo nitaweza kuhamisha pesa kutoka kwenye account ya huyo mtu ambae simjui na kuingiza kwenye simu yangu na jamaa akanambia atanitumia ujumbe wavkuniunganisha na nitaweka namba ya siri mpya.

Ila mpaka sasa bado hajaniunganisha, ila ninachojiuliza akiniunganisha na nikahamisha pesa watanitafuta? Watanishtaki? Watanifunga? Iikiwa nilishawapa taarifa zaidi ya mara mbili.
 
Hatari sana...

Nenda bank wakutoe kwenye hizo transaction, la sivyo kuna watu watakua wanapiga pesa haramu kupita mgongo wako...

Jumba bovu litakuangukia wewe...


Cc: mahondaw
 
Una hofu gani mkuu?? Mbona unaogopa kujibizana na mashine?? Tulia kidogo tu halafu uulizie salio. Likiwa kubwa ndo ujiulize, huyu mtu anazipataje. Likiwa la kawaida jua ni kabwela tu kakosea namba. Mzimie pass word uiweke ya kwako hadi ashike adabu aende huko bank arekebishe mwenyewe. Kama ni nyingi, jikopeshe za kuanzisha mradi wala usiogope jela kwa sababu hujawahi kwenda bank hiyo
 
Back
Top Bottom