Emanueli misalaba
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 1,113
- 1,659
Wana jukwaa pendwa la Jf habarini za leo!
Katika kuja kwangu mara moja Dar es salaam nikitokea zanzibar niliamua nichukue zawadi walau kiduchu kwa ajili ya shemeji yangu sukari kilo 5, cha ajabu nilipofika bandarini Dar kulingana na maelezo ya wakanguzi wa bandarini wamenifanya niwe na maswali kadhaa moyoni mwangu na hasira zikawaka sana nafsi mwangu, wakasema sukari kutoka zanzibar kuja bara hairuhusiwi hata kama ni nusu kilo hata kama ni kwa matumizi ya nyumbani.
Mm najiuliza kwani zanzibar si sehemu ya Tanzania?
Kwani sukari ya zanzibar ina madhara kwa mlaji?
Uharamu wa sukari ya zanzibar kuja nayo Bara ni upi?
Hivi mtu akiwa anatoka na sukari kutoka Mwanza anahojiwa? Hivi ile kamati ya kushughulikia kero za Muungano hili hawajaliona?
Wiki iliyopita nilisafiri na mchele kilo 10 kutoka Dar es Salaam kwenda nayo zanzibar sikuulizwa na mtu yeyote wa bandari zote mbili.
Niwaombe wizara ya Muungano ituambie wananchi ni bidhaa zipi haziruhusiwi kutoka bara kwenda zanzibar na kutoka zanzibar kuja Bara.