JE! NI HARAMU KUSAFIRI NA SUKARI KUTOKA ZANZIBAR?

Emanueli misalaba

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
1,053
1,591
Wana jukwaa pendwa la Jf habarini za leo!
Katika kuja kwangu mara moja Dar es salaam nikitokea zanzibar niliamua nichukue zawadi walau kiduchu kwa ajili ya shemeji yangu sukari kilo 5, cha ajabu nilipofika bandarini Dar kulingana na maelezo ya wakanguzi wa bandarini wamenifanya niwe na maswali kadhaa moyoni mwangu na hasira zikawaka sana nafsi mwangu, wakasema sukari kutoka zanzibar kuja bara hairuhusiwi hata kama ni nusu kilo hata kama ni kwa matumizi ya nyumbani.
Mm najiuliza kwani zanzibar si sehemu ya Tanzania?
Kwani sukari ya zanzibar ina madhara kwa mlaji?
Uharamu wa sukari ya zanzibar kuja nayo Bara ni upi?
Hivi mtu akiwa anatoka na sukari kutoka Mwanza anahojiwa? Hivi ile kamati ya kushughulikia kero za Muungano hili hawajaliona?
Wiki iliyopita nilisafiri na mchele kilo 10 kutoka Dar es Salaam kwenda nayo zanzibar sikuulizwa na mtu yeyote wa bandari zote mbili.
Niwaombe wizara ya Muungano ituambie wananchi ni bidhaa zipi haziruhusiwi kutoka bara kwenda zanzibar na kutoka zanzibar kuja Bara.
 
Bidhaa nyingi kutoka Zanzibar huzuiliwa bandari za Bara kwa sababu ya kuchanganyikana na bidhaa za kimagendo, dumped cheap products na maswala ya kodi
 
Duuh
naijatwittersavages-20190528-0002.jpeg
 
Bidhaa nyingi kutoka Zanzibar huzuiliwa bandari za Bara kwa sababu ya kuchanganyikana na bidhaa za kimagendo, dumped cheap products na maswala ya kodi
mmmmmh nusu nasadiki na nusu sisadiki.
Kwani TRA, TIIS na majeshi mengine ya kupambana na magendo zanzibar hawaruhusiwi kufanya kazi kule?
 
Kiufupi ndugu zetu wanateleza na huu muungano kuliko sisi.

Wewe peleka hata ubuyu kule hakuna wa kukuuliza, ila beba hata mchanga kule uone kimbembe hapo ferri.
Huu ni Muungano wa Kipekee duniani, Mtanzania Bara anaye ung'ang'ania ndo Ananyonywa, anayetaka uvunjike ndo mnyonyaji mkuu

Britannica
Hebu kaa angalau dakika moja ufikirie.

Unatoka na kitu znz huzuiliwi ila bandari ya huku wanakuzuia. Nani ananyonywa hapa? Huoni kama mzanzibari ndio ananyonywa?

Viwanda vyao vya sukari vinazalisha kwa ajili ya znz tu hawaruhusiwi kuuza bara ila bara viwanda vyao vinauza kote kote?

Kuna mbunge znz aliwahi lizungumza hili.
https://www.mwananchi.co.tz/habari/...kuuzwa-Bara/1597578-4232658-db2q5s/index.html

Huu ni unyonyaji mwengine wa Serikali kuvifanya viwanda vya znz visikue.
 
Wana jukwaa pendwa la Jf habarini za leo!
Katika kuja kwangu mara moja Dar es salaam nikitokea zanzibar niliamua nichukue zawadi walau kiduchu kwa ajili ya shemeji yangu sukari kilo 5, cha ajabu nilipofika bandarini Dar kulingana na maelezo ya wakanguzi wa bandarini wamenifanya niwe na maswali kadhaa moyoni mwangu na hasira zikawaka sana nafsi mwangu, wakasema sukari kutoka zanzibar kuja bara hairuhusiwi hata kama ni nusu kilo hata kama ni kwa matumizi ya nyumbani.
Mm najiuliza kwani zanzibar si sehemu ya Tanzania?
Kwani sukari ya zanzibar ina madhara kwa mlaji?
Uharamu wa sukari ya zanzibar kuja nayo Bara ni upi?
Hivi mtu akiwa anatoka na sukari kutoka Mwanza anahojiwa? Hivi ile kamati ya kushughulikia kero za Muungano hili hawajaliona?
Wiki iliyopita nilisafiri na mchele kilo 10 kutoka Dar es Salaam kwenda nayo zanzibar sikuulizwa na mtu yeyote wa bandari zote mbili.
Niwaombe wizara ya Muungano ituambie wananchi ni bidhaa zipi haziruhusiwi kutoka bara kwenda zanzibar na kutoka zanzibar kuja Bara.
Zanzibar ni nchi ya kigeni... muungano ni kung'ang'anizana hautofautiani na nyumba ya mabua...
 
Hapa Unguja sukari kilo moja sh1500 wamefungasha kilo 5 kwa 8500 tu ,hapo kwenu bara sukari mwanunuaje? Maana mie kusafiri kwangu mwisho "chumbe"
 
mmmmmh nusu nasadiki na nusu sisadiki.
Kwani TRA, TIIS na majeshi mengine ya kupambana na magendo zanzibar hawaruhusiwi kufanya kazi kule?
Huo ndo ukweli.... Zanzibar biashara za magendo na dumped cheap products ni kwa sana licha ya kuwepo TRA na Vyombo vya Ulinzi na Usalama (Polisi, JWTZ navy command, Uhamiaji na TISS).

Ukiacha sukari, kuna mchele wa magendo, mafuta ya kula ya magendo, ngano, saruji, vifaa vya ujenzi na used electronics kibao
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom