Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,842
- 10,765
Wakuu umuofia kwenu,
Nianze kwa kukiri kuwa hii ni mojawapo ya mada ngumu kabisa kuijadili mbele ya kizazi cha leo, yaani kizazi kipya. Najua si kila mtu ataipokea kwa mtazamo wa kupingana kwa hoja, bali wako ambao wataibuka na matusi na kejeli, kwa wakuu wa mtazamo huo, niombe tu tuvumiliane. JF where we dare to talk openly ndio motto yetu.
Nianze kwa kuelezea mtazamo wangu kuhusu mchakato mzima wa ndoa hapo awali na kisha nioanishe na kile kinachofanyika hii leo.
Mtazamo wa awali
Ndoa ilikuwa na pande mbili, kwanza kabisa ni muunganiko wa ukoo wa mwanamke na mwanamume, halafu pia ilikuwa ni muunganiko wa mume na mke na kuwa familia moja, ama mwili mmoja. Kwa kawaida mwanamke alitakiwa kusubiri nyumbani kwa wazazi wake mpaka pale atakapochumbiwa, kisha kutwaliwa na mume. Wazazi wa mume ndio waliokuwa na jukumu la kuchagua kati ya mabinti wengi ili kumpata ambaye walidhani ataweza kuendana na kijana wao kwa kuzingatia jinsi walivyomlea.
Kijana yeye alionyeshwa tu kuwa tunataka uoe binti wa familia fulani, naye alipokea kwa mikono miwili. Wazazi walishafanya uchunguzi wote kujua ni familia gani inafaa, binti ni mwenye adabu na kujua malezi, hakuna magonjwa ya kurithi kwenye ukoo husika (mfano ukoma) n.k. Taratibu za posa zilifanyika, mahari ikatolewa na harusi ikapangwa. Binti kwa upande wake hakuwa na hoja ya kujadili, wazazi wake walichunguza ukoo na familia iliyoleta posa kuona kama ni wenye maadili na wachapa kazi, ili asije akapata dhiki mara aolewapo, hakuna magonjwa ya kurithi n.k. Ndio maana ilikuwa kawaida kuambiwa tutawapeni majibu siku zijazo, mtupe muda wa kutafakari.
Sasa katika dunia ya leo utaratibu huu unaweza kudhaniwa kuwa ni wa kipuuzi na kandamizi. Mtazamo huu hasa umejengwa kwenye jamii za kiafrika na wale wa kipato chini huko ulaya na Marekani. Nasema hivyo kwa sababu mfano jamii za kihindi bado wana mchakato huo mpaka sasa, ndio maana sio rahisi kwa mmakonde kuoa binti wa kibaniani. Ndivyo ilivyo kwa familia tajiri huko ulaya na marekani, binti hawezi kukurupuka tu kuolewa na mwanamume yeyote. Sasa jambo hili lina sababu muhimu sana kwa jamii hizi:
1. Vijana wadumu katika ndoa
Sikumbuki ni mara ngapi nimesikia maharusi kutoka koo tajiri wametengana. Siongelei wasanii ambao maisha yao ni usanii, naongelea matajiri wanaojulikana hivyo, waliotulia vema na familia zao. Hawa huhakikisha watoto wao wanaoa na kuolewa kwenye familia zinazoeleweka na vijana wenye maadili. Kama familia ni tajiri lakini wana sifa mbaya (mfano wauza unga) basi wazazi hukataa posa. Wanawalinda watoto wao.
2. Kukwepa magonjwa ya kuambukiza
Wazazi walikuwa makini kuona magonjwa ya kurithi hayaingizwi kwenye ukoo. Hili lilikuwa jambo la muhimu sana kwa magonjwa kama asthma, sickle cell anaemia, reprosy n.k.
3. Kulinda mali za ukoo/ familia
Kwa sababu wazazi waliwandaa watoto wao wa kiume kulingana na shughuli wanazofanya, kijana alitarajiwa aje kuwa mrithi wa kuendeleza mali za ukoo. Wazazi walihakikisha legacy yao haifi na kwa kuwa wanadamu muda wetu ni mfupi, ilikuwa ni muhimu kuhakikisha kuwa kijana anakua katika misingi ya kuendeleza hilo.
4. Kuendeleza kizazi bora
Utaratibu wote huu ulilenga kuhakikisha mwanamume anajenga kizazi bora kabisa kama mwendelezo wa ukoo. Kama mwanamke hakuwa na sifa za kuwa mke hangeweza kuolewa kwani uzao wake ungekuwa usio na maadili. Mwanamke ndiye mwalimu mkuu wa watoto katika familia.
5. Kupunguza uwezekano wa kutokea migogoro
Kwa sababu wazazi walitazama tabia na mwenendo wa mwanamke na mwanamume, hii ilipunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kutokea migogoro mikubwa isiyoweza kupata suluhu.
6. Kumfanya mwanamke kuwa sehemu ya ukoo
Mwanamke aliyeolewa kwa utaratibu huu alifanywa kuwa sehemu ya ukoo. Alibadili jina lake la mwisho kuwa la ukoo alikoolewa na ilikuwa heshima kubwa kwake. Ukoo mzima ulimpokea kama mwanafamilia na alikuwa na haki sawa na wanaukoo wengine. Kwa muktadha huu, hata matatizo yaliyojitokeza kwenye kati yake na mumewe, kimbilio la mke ilikuwa ni kwa wazazi wa mumewe (ukoo wake mpya) ambako alisikilizwa zaidi kuliko hata mumewe. Mke hakupaswa kupeleka shauri lolote kwao bali kama kungekuwa na tatizo kubwa la kuweza kufikia kushirikisha wazazi wake, basi wazazi wa mume wangehusika katika hilo, sio mwanamke ama mume wake.
Ndoa za siku hizi
Siku hizi ndoa si kati ya koo mbili, mchakato umetekwa na watoto. Mtoto anatafuta mke wake mwenyewe, anampeleka kwa wazazi wake kumtambulisha. Sasa mke wa namna hii hawawezi kamwe kuchangamana na wazazi wa mume, ndivyo ilivyo pia kwa upande wa wazazi wa mwanamke, hawawezi kwenda sawa na kijana muoaji.
Utakuta mtazamo wa ndoa kwa kijana ni tofauti kabisa na wazazi. Kinachofanyika ni wazazi kuamua kuruhusu tu waoane ili kuepusha lawama za kizazi kipya. Wazazi wa binti wataruhusu binti aolewe hata bure kwa sababu anaweza kuzalia nyumbani, kwani mara nyingi inapoletwa posa, ujue watu hao walishachomana sana tu. Sasa wamelewa penzi, ndipo wakaamua watafute ushahidi kwa jamii kwamba wanalala pamoja.
Sasa athari za ndoa ya aina hii
1. Hakuna muunganiko kati ya mke na wazazi wa mume
Mara nyingi muunganiko huu haupo kabisa. Wazazi hawaafikiani na mwenendo wa mwanamke na hivyo kuona mwana wao amepotea. Wakati binti akiolewa hapo zamani ilikuwa kawaida kabisa kumtembeza kwa ndugu mbalimbali ambako alipewa heshima kubwa na kutambulika rasmi kama mmoja wa wanaukoo. Lakini kwa mfumo wa kisasa, si ajabu kwa mwanamke kujulikana na wazazi wa mume tu, nasema kujulikana na si kuchangamana.
2. Hakuna muunganiko kati ya mume na mke
Kwa sababu wamekutana na kujenga mahusiano kwa kuzingatia mambo ya juu juu (false premises), pindi mambo hayo yanapoyumba ufa hutokea. Kila mmoja ana namna ya ku-react pale hali inapobadilika, hawana tabia zinazofanana. Sasa ijulikane kuwa ndoa sio mali bali ni character. Kama hamuendani kwenye tabia na mitazamo, basi ndoa haiwezi kuwa na maisha marefu. Ndipo tulipopata ule msemo ndoa ni kufanana, sio kufaana!!
3. Wazazi wanapoteza imani na kijana wao
Kama hapo juu, kwa vile wazazi wamemhesabu kijana wao kama amepotea, basi ni ushahidi kwao kuwa hana uwezo wa kujenga ukoo bora na pia kusimamia mali za familia. Hawawezi kukubali kamwe kumwamini katika hilo na pia hata mke watamwona kama ni mporaji tu. Wanaanzaje kuwa na imani na mwanamke ambaye hata historia yake hawaijui wala ukoo aliotoka?
4. Mume atatatoka kwao lakini mke atabaki kwao
Wakati mwanamume anatarajiwa kuwaacha wazazi wake akiambatana na mkewe wakaendeleze ukoo, ukweli ni kuwa mke atabaki kwa wazazi wake na mumewe atakuwa part time. Ni kawaida kwa mwanamke huyu pale akipishana na mumewe kusema sijafukuzwa kwetu, kama umenichoka nirudishe n.k. Huyu sio mwajiriwa wa kudumu, ni kibarua tu ndani ya ndoa asiye na mkataba. Kwani hata akiona mambo yamekuwa magumu kimaisha hachelei kumwacha mumewe kwa sababu hana muunganiko wa kweli naye. Tena anaweza hata kuanzisha project za siri akishirikiana na watu wa kwao (akimwibia mume). Ni aina ya mwanamke ambaye mara tu anapoingia kwenye ndoa huanza kujiandaa kutoka.
5. Mke atakuwa adui wa kudumu wa ndugu wa mume
Mwanamke wa namna hii huwa ugomvi wa kudumu na ndugu wa mumewe, hasa wanawake wenzake. Hii hutokana na ama mafundisho potofu kuwa usiruhusu ndugu wa mume wakuzoee watavunja ndoa, ama sababu ya kutokubalika kwake ndani ya ukoo. Jambo hili litampelekea mwanamume kutothaminiwa na ndugu zake na hivyo wengi wa wanaume hujikuta wakijipambanua zaidi na ukoo wa mwanamke na hivyo wao kuolewa. Nyumba hugeuka kaa la moto kwa ndugu wa mume huku ndugu wa mke wakikaa kwa nafasi, mwanamume kwa vile hajui maana ya ndoa huona kuwa jambo la kawaida huku aliwatupia lawama ndugu na wazazi wake.
Vipi kuhusu mali?
Kufuatia mazingira ndoa za zamani, mwanamke hakuhitaji kurithi mali kwa sababu tayari alikuwamo kwenye ukoo wa mumewe. Hata kama mumewe angefariki, wazazi/ndugu wangesimamia mali hizo pamoja na matunzo ya mwanamke na watoto mpaka watoto wa kiume wapate ufahamu. Mwanamke kama mwolewaji asingeweza kurithi mali za ukoo kwani mali kwenda kwa mwanamke ni kuhamishia kwenda ukoo wake. Hata mtoto wa kike hakurithi kutoka kwa baba yake kwa sababu ataolewa kwenda kujenga ukoo mwingine. Pia kama mambo yangemshinda alipaswa kurudi nyumbani kwao ambako mali za ukoo zilitunzwa.
Mazingira ya namna hii yaalipelekea wazazi kuacha mali zao zisimamiwe na watoto wao wa kiume kwani walijua ziko kwenye mikono salama. Lakini leo hii hakuna mzazi anakubali kutoa mali zake kwa mtoto wa kiume kwa sababu ya mwenendo usiofaa. Kwa sababu ile misingi ya kuendeleza mali imekiukwa, vijana wamekuwa wanahisa kwenye ndoa, asilimia 50 kwa 50, hakuna muoaji wala muolewa. Vijana wanaanzisha koo zao wala si kuendeleza ukoo, yaani kilichobaki ni kujitambulisha kwa majina tu, mimi ni ukoo wa Lizarazu lakini kiuhalisia ni ukoo mpya kabisa. Ni kawaida siku hizi kuwaonyawazazi wasiingilie mahusiano ya watoto, tena mada hizi fitinishi zikitokea mpaka kweenye nyumba za ibada. Wazazi wako waliojinyima kukujengeamaisha ya baadaye unawatosa kwa sababu ya tamaa za kimwili. Baada ya kujidhiki ili mtoto wao awe na maisha bora, anakuja kuwalinganisha na mali na kuona hawaenei. Dunia inakwenda kasi sana.
Wako wanaojipambanua kudai wao wametafuta mali peke yao wakiwa na wake zao, hivyo mali hizo ni zao. Hawa huanzisha ukoo mpya kwa kutazama mali ambazo ikitokea zikaisha, wao ama watoto wao hutaabika sana kwa kukosa ndugu wa kuwa karibu nao. Walitumainia mali kuliko kuwekeza katika kuendeleza ukoo. Ndio maana siku hizi kumeibuka vita kubwa ya kugombea mali punde mume anapofariki. Hebu waza tu kwa akili ya kawaida, marehemu mzee wetu alietuacha màjuzi halafu mali zote zirithiwe na mke na hivyo ukoo wake kupotea kwenye ramani ya matajiri, kuna usawa hapo? Mwanamke atahamisha mali kwenda kwa ukoo wake.
Hizi ni baadhi ya sababu kwa nini mwanamke hakuwekewa kurithi mali tangu enzi. Tusubiri hoja za Mh Makonda kama zitaleta mabadiliko ya sheria.