Je, ni halali kwa mgombea Urais CCM kufanya haya?

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Kuna Jambo haliko sawa kwenye Kampeni za Wagombea Urais hasa kwa mgombea wa CCM Bwana John Pombe Magufuli.

Bunge la JMT lilivunjwa mwezi June, 2020 ili Rais, Mawaziri na Wabunge waende kwenye Uchaguzi kuomba ridhaa ya wananchi ili warudi tena Ikulu, Wizarani na Bungeni.

Katika Kampeni zake Rais aliyefikia ukomo wa kukaa Ikulu Bw. John Pombe Magufuli anakwenda akiahidi kutoa pesa za miradi na fedha ati ipo.

Amefikia hata kuwapigia simu Mawaziri waliomaliza muda wao na Makatibu eti wapeleke pesa mara moja kupeleka huduma ambazo alitakiwa kuzikamliisha ndani ya miaka 5 iliyopita.

Hii naweza kuiita ni Rushwa moja kwa mojani ili aweze kupigiwa kura ifikapo tarehe 28 Okt, 2020.

NEC na TAKUKURU mnakwama wapi katika hili? Chukua hatua mapema.

2525599_IMG-20200921-WA0004.jpg

Soma hiyo Makamanda.
 
Huyu mzee anachosha sana. Sitaamini siku atakapo ondoka madarakani.

Kwanini Magufuli, CCM, NEC na TAKUKURU wanatufanya Watz hatuna akili? Hawa jamaa ni kuwa FYEKELEA MBALI ifikapo tarehe 28 Okt, 2020!

Mungu na atusaidie maana Tumechooooooooooka.
 
Nani Atamgusa? Nani Atasema Lolote?
Mamlaka Zote Kimya!!
Acha Tuone

Ni sawa mamlaka zote ziko kimya maana kazitia mfukoni.

Je, Vipi kuhusu Umma wa Watz unao- suffer tokana na Utawala huu dhalimu? This must be a wake up call!
 
Haya Ndiyo Mambo yananifanya nikate tamaa na Chaguzi za kibongo.
IMG-20200921-WA0004.jpg

Hivi nikweli Kuna Wajinga Ambao Bado wapo miaka nenda Rudi wanatumika Kama mtaji!!! Wa Chama.
IMG-20200921-WA0000.jpg
Ndiyo maana huwa Sina Imani na Siasa za kibongo sipotezi muda wangu.

Bunge limevunjwa, Baraza la Mawaziri lililopo Ni Batili kisheria lilipaswa kuvunjwa Baada ya Bunge kuvunjwa, Maana hakuna Waziri ambaye siyo Mbunge. Bado Waziri
Batili anapigiwaa simu Tena kwenye Jukwaa la Kampeni,

Maswali
1.Angefanya Mpinzani Angeachwa Salama?? Na Tume??

2.Anapiga Simu Ina maana ana uhakika atarudi Ikulu Ila anatufanyia maigizo.!!?,Sasa kwanini tunapoteza muda na fedha?!!
3. Kama Waziri atatekeleza Ahadi he hizo Fedha zimejadiliwa na Bunge lipi?? Kwanini asiache uchaguzi upite atekeleze??!

4.Je hapo Uvinza ndiyo pekee wanastahili!! Kama ndiyo Je hiyo Ni haki au fadhila??

Sheria ya Uchaguzi Imeweka wazi Sheria za uchaguzi, Ila Tume wapo kimya, Je akishindwa Uchaguzi wanaweza kumuangusha kweli??

Mtu aliyekwisha kutamka akupe kazi, Nyumba,Gari, Halafu umtangaze Mpinzani !!? HUWEZI kusarvive. Niwazi Kuna Ubakwaji wa Demokrasia na Ukiukwaji wa Katiba.
 
Tayari kuna barua hapa tunamalizia kuitype iende kwa wafanyakazi wa tume wamchukulie hatua za kukiuka kanuni za uchaguzi.
Japo inaweza isizae matunda ila lazima tuweke kumbukumbu sawa ili ikija tokea asiwepo wa kurahumu.

Hiyo na iende faster.....tuone reaction yao. Kwa sasa UN, EEU na US wanafuatilia kwa katibu Sana.
 
Kuna Jambo haliko sawa kwenye Kampeni za Wagombea Urais hasa kwa mgombea wa CCM Bwana John Pombe Magufuli.

Bunge la JMT lilivunjwa mwezi June, 2020 ili Rais, Mawaziri na Wabunge waende kwenye Uchaguzi kuomba ridhaa ya wananchi ili warudi tena Ikulu, Wizarani na Bungeni.

Katika Kampeni zake Rais aliyefikia ukomo wa kukaa Ikulu Bw. John Pombe Magufuli anakwenda akiahidi kutoa pesa za miradi na fedha ati ipo.

Amefikia hata kuwapigia simu Mawaziri waliomaliza muda wao na Makatibu eti wapeleke pesa mara moja kupeleka huduma ambazo alitakiwa kuzikamliisha ndani ya miaka 5 iliyopita.

Hii naweza kuiita ni Rushwa moja kwa mojani ili aweze kupigiwa kura ifikapo tarehe 28 Okt, 2020.

NEC na TAKUKURU mnakwama wapi katika hili? Chukua hatua mapema.

Nilikuwa mzito mno kutaka Katiba ya Tanzania ifanyiwe 'Marekebisho' makubwa ila kwa sasa nadhani nitakuwa ni Shabiki wa kudai Katiba Mpya TZ.
 
Back
Top Bottom