Je ni dharau, kudata au tamaa ya mapenzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni dharau, kudata au tamaa ya mapenzi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kisute, Jun 18, 2011.

 1. kisute

  kisute Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juzi rafiki yangu ambaye ni mfanyabiashara mkoani Tabora yalimkuta yafuatayo katika hali isiyo ya kawaida na hakutegemea kama mkewe mpendwa angemfanyia hayo. Akinisimilia alisema; kama ilivyo desturi ya mfanyabiashara yoyote usafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kufuatilia zilipo bidhaa na masoko mazuri. Katika biashara zake uchukua mzigo Mwanza , kupeleka Dar then Dar Kigoma, Arusha na kwingineko.
  Wakati mwingine huchua hadi wiki moja hajarudi nyumbani kwake. Anasimulia kwamba; wamekaa na mkewe miaka tisa sasa na wamejenga nyumba kubwa ya kifahari, kwa bahati mbaya hawajabahatika kupata mtoto. Siku hiyo ya tukio, alifika mjini hapo saa mbili usiku na alikwenda moja kwa moja kwa mama yake mzazi kumsalimia. Mama yake alimwandalia chakula akala na baadaye alimwaga mamake na kurejea nyumbani kwake majira ya saa nnne usiku. Alipofika pale kwake alikuta taa za nje zimezimwa na za ndani hali kadhalika. Alipousogele mlango wa mbele akasikia watu wakinong'ona lakini hakutilia shaka, aligonga mlango mara kadhaa pasipo kujibiwa. Basi alizunguka uwani na kufunga komeo la nje la mlango wa kutokea uwani. Kisha alirudi tena kugonga mlango wa mbele, lakini ukimya ulitawala. Akakumbuka kwamba ndani ya nyumba yake alikuwa akiishi na mtoto wa dada yake ambaye anasoma sekondari kidato cha pili. Alimgongea ili amfungulie mlango, na akawa kafunguliwa. Desturi ya rafiki yangu akifika nyumbani huanzia bafuni kuandaa maji kisha huenda chumbani kuvua nguo ili aoge. Baada ya kuandaa maji alielekea chumbani kwake kupitia kwenye korido, lakini roho ilisita kuingia chumbani kwake. Alimwita mkewe akimwomba atoke chumbani, mkewe alifanya hivyo. Rafiki yangu alimhoji mkewe kulikoni chumbani honey mbona naogopa hata kuingia huko? Mkewe alimjibu hakuna kitu mme wangu. Mkewe akimjibu hayo akitembea kuelekea sebuleni ambako alifika na kuzima taa ya sebuleni kukawa giza nene nyumba nzima. Ghafla mmewe alipigwa kikumbo na mtu ambaye alitokea chumbani kwake. Rafiki yangu alijigonga ukutani na kuchanika kichwa, lakini alifanikiwa kuudaka mguu wa mwizi wake. Jamaa kuona sasa anaumbuka alimpiga teke zito usoni na kutokomea nje. Rafiki yangu alinyanyuka pale chini wakanza kufukuzana lakini hakufanikiwa kumpata mwizi wake. Wakati anarudi kwake alimwona mkewe akiwa kashikilia mkoba akitimua mbio, alijaribu kumkimbiza lakini mkewe aliingia nyumba ya tatu tu kutoka pale kwake na mlango alifungwa, baadaye alitoka jamaa mmoja na fimbo nene mithili ya mkono na chumba kingine alitoka kijana mwingine walianza kumpiga rafiki yangu ile mbaya. Rafiki yangu alipiga kelele kuomba msaada hukuakisema mke wangu unaniua ndipo mtoto wa dadake alifika na kuomba msaada zaidi. Rafiki yangu alikuwa kaumizwa vibaya sana. Watu walifika pale kujua kulikoni, nae aliwaeelezea kisa kizima na yaliyojiri. Wakati huo huo alipiga simu kw a wazazi wa mkewe na kwa mamay ke mzazi kumwelea yaliyomsibu. Rafiki yangu alienda Polisi kuchukua PF3 ili apate matibabu.
  Anaomba ushauri nini afanye kwa mke wake huyo? kwani tangu akimbie usiku ule hajaonekana hadi sasa. Wazazi aliwapa taarifa nao kimya. Je, hayo ndo mapenzi ya kweli? Je ni vizuri mkewe kumletea wanaume katika nyumba yake? Je huko ni kudata au ni nini? Jamani niusaidieni.
   
 2. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,869
  Trophy Points: 280
  hmmmm!!! kwa kweli hapa busara za akina babu Aspirin n th Co zinahitajika, lets wait them...!
   
 3. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mwambie huyo jamaa aache kumtafuta huyo mke aendelee na shughuli zake, amekosa adabu huyo mke guest zilivojaa hivi ameshindwa kwenda huko mpaka aende kwake? kamaameshindwa kuheshimu hata nyumba yao na wanafamilia wake hawezi muheshimu milele, aanze maisha yake, vitu vingine Mungu huvifanya kwa makusudi, labda ameona jamaa anamuhandle mkewe vizuri pamoja na kuwa mtoto kakosekana , wanaume wengine miaka minne tu shughuli ama hujazaa, labda Mungu kakuonyesha mkeo ni wa aina gani ili uendelee ne maisha yako aliyokuandalia
   
 4. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,518
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kwanza mpe pole sana rafiki yako kwa yaliyomsibu maana hapo kweli hekima kutoka kwa mkewe haikuwepo.....
  Pili inabidi afuatilile matibabu kwanza apone kabisa na baada ya hapo amshtaki mwizi wake na amtafute mkewe amuulize kulikoni? inanishangaza kuona hata wazazi wa mkewe kukaa kimya katika jambo hili kana kwamba walijua nini kinaendelea kwa mtoto wao. hizi ndio ndoa ndugu yangu huna budi kupitia challenges nyingi za maisha na vitu kama hivi ni baadhi tu ya challenge zinginezo. ila kweli hii ni noma sana mke kuingiza mtu chumbani kwangu na sio chumbani tu kulala kitanda ambacho nakitumia kuzalisha familia yangu kweli huu si uungwana. mi nafikili hakuna ndoa hapo.
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  nadhani bado nina hangover ya mbege, hii stori inanichanganya kidogo, kikuombo cha namna gani mpaka mtu achanike tena ukutani, hapo hapo jamaa mwenye nyumba alimshikaje mwizi wake mguu ilihali kuna giza tororo? haya na huyo mwingine alietokea huko chumbani na fimbo ni nani na nia ya hawa watu ni nn, walikuwa wapenzi au? mbege hii inanipeleka pabaya sasa, Asprin hebu njoo nifafanulie plz.
   
 6. d

  designer spenko Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmmmh kwa kwli ni jambo zito bt mwombe mungu akupe busara kama ikishndka kuelewana tafuta maisha mengine
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Zinaa haina msamaha......
  Na hivi hawajazaaa.....aaaa mwache aende
   
 8. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,643
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Hapo hakuna mapenzi, na pengine kutozaa ni plani ya huyo mama. Aangalie maisha yake tu, haiwezekani mtu unamfumania halafu anashiriki kukupa kichapo, amekwepa kifo huyo.
   
 9. wahida

  wahida JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ana weza kudata kwa mapenzi, bcz kumueka mtu rohon ,then aka kutenda it too bad, mpe pole ndio maisha ,binaadamu tuna kua tuna sahau nini wajibu wetu sometime,,
   
 10. o

  ombeni Member

  #10
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndio maana mimi sitaki kuoa!
   
 11. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #11
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  ndoa ndoano
   
 12. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hii hadithi kama ya kutunga vile..
  .......
  Kisha akarudi kugonga tena, hakufunguliwa..
  Akaenda kumgongea mtoto wa ndugu yake, akamfungulia.. kwa nini hakumfungulia tangu mwanzo?
  ........
  Akasita kuingina chumbani, kisha akamwambia mke wangu njoo, akaja... ina maana walikuwa wanamsikilizia ili wamdhuru?
  ............
  Pia hili la mkewe kumpita na kwenda kuzima taa, kisha kikumbo, mara teke, mara vijana na fimbo, yaani imekaa kama muvi vile...
  ...................
   
Loading...