Je, ndoa hii nani mkosaji?

Pole huo mkasa uliokukumba. hapo huna jinsi zaidi ya kumuacha huyo mwanamke.
 
Kiongoz kwa ushauri wa maana mfanyie icho anachokufanyia,japo we ufanyi kwa kusudi,tafta wadada watatu tofauti wapange wawe wanakupigia cm usiku halaf ungee nao kimapenzi,...trust me ataacha mbaya anaumia sana ukimfanyia ubaya wake ila usivunje ndoa mkuu INA athari

NB uwe mwangalif usifall na wale wengin afu hakikisha unafanya akiwepo,..utaona anajirud
 
Pole sana kaka, laana ya yule manzi wako wakwanza wewe miaka 7 halafu unamtosa malipo hapa hapa duniani, mapenzi sarakasi wengine tunasumbuliwa na waume wengine wake zao mie hujiuliza kwanini Mungu asingekuwa anakutanisha wenye tabia moja? Kama nikweli du huyo mkeo kiboko wanaume mmezidi mtu akikupenda mnamnyanyasa sasa umekutana na choo cha city[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Pole sana mkuu bt Kuna jambo ambalo ulifanya makosa makubwa Sasa wewe vituko vyote alivyokuwa anakufanyia kabla hujafunga nae ndoa hulikuwa uvioni na Mara kwa Mara akawa anakuomba msamaha daa mkuu sijui uliwaza nini mambo yote ulikuwa unayaona bado tena ukaamua kwenda kanisani kufunga ndoa? Mkuu Mimi navyojua ndoa zetu za kanisani ni ngumu na kumbuka uliapa mbele ya mungu na mbele ya kanisani utampenda kwa shida na raha na kifo ndio kitawatenganisha Sasa mkuu ni kumuomba mungu akusaidie kwenye hio ndoa bt hautaweza kumuacha na yeye anajua
 
Kunguru hafugiki, huyo achana naye, nakushauri fuata taratibu na wahusishe ndugu na jamaa
 
Kwahyo unazan ndo Atabadlka?.... Bible inaruhusu kumuacha Mke kwa uzinzi.... Wanaokwambia uongee naye nazan wanachklia poa Sana.... Lakin mtu makin aliyekuelewa hawez shauri hivyo.... Huyo hawez badlika kamwe! ......zembea akuue kwa ukimwi..... Au uendlee kufa taratb kwa stress..... Achana nae bro mtamuacha mtoto wenu yatima bure...... Fanya biashara Zako wanawk ni wengi utapata tulizo la moyo tu.....
 
Daaaah asee pole sana
 
From today nimeshavua Pete na nipo kwenye maamuzi ya mwisho wazaz wangu tayar nimewapa taarifa,sasa bado kanisani na ndg zake.
 
Kabisaa
 

Hapo ulipofika kaka mimi nisingefika, ningekuwa nishakusanya virago vyangu nishatafuta msitu mwingine wa kuhangaika nao.
 
Ndg,pole sana kwa hayo yanayokusibu.Kutokana na maelezo yako nilivyoelewa mm chanzo cha hayo yote ni ww,ingawa yawezekana pia mwanamke huyo anatabia mbaya toka awali ww hukumjua vzr kachanganya na ulipizaji visasi,mm nikushauri kuwa makini sana na maamuzi yako juu ya ndoa vinginevyo mtamsumbua bure mtoto kimalezi kwa tabia zenu,kaa chini na mkeo mtafute suluhisho kwani uamuzi wa kuoana na kuachana upo mikononi mwenu.NB ndoa ni ya watu wawili inahitaji uvumilivu sana,muda tu hautoshi ningekusimulia mkasa wangu wa ndoa sizani kama huo wa kwako ungeuona mkubwa kwa kifupi mm na mke na watoto wawili na miaka 8 ya ndoa lakini ni shida,mwanamke Jeuri,mgomvi,dharau,matusi usikukucha hana heshima,adabu na utii kwa mume anachat na wanaume hovyo kwenye simu yake,hafui nguo zangu hadi ajisikie pia haweki hata chakula wakati mwingine mbaya zaidi nimenyimwa unyumba kwa miezi 8 nalala chumba kimoja kitanda kimoja ww unaweza?na unatoa matumizi vzr kama baba wa familia niishie hapo ndg ndoa inahitaji kipaji vinginevyo utaoa sana na kuacha wanawake wa karne hii shida sana ingawa si wote wenye vijitabia hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…