Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,016
- 9,885
Ameandika Martin Maranja Masese.
Kiumbe ambaye CIVICS kidato cha nne alicheza na mswaki (F) anawezaje kuwa waziri wa kushughulika na masuala nyeti ya teknolojia, Habari na mawasiliano? Hatupo ‘siriazi’ kabisa wanetu.
Paula Ingabire ni Waziri wa Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Ubunifu, kachapa University of Rwanda (B.S.) na Massachusetts Institute of Technology (M.S.)
Paula akiwa Massachusetts Institute of Technology (MIT) alikuwa Mfanyakazi wa Ubunifu na Usimamizi wa Mifumo. Rwanda wamemfanya kuwa Waziri wao wa Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Ubunifu
Paula Ingabire pia alifanya kazi kama mratibu wa Smart Africa, mpango ambao unalenga kuimarisha miundombinu ya broadband kuendesha uchumi wa kijamii na kiuchumi barani Afrika.
Kabla ya kuteuliwa, Paula Ingabire alikuwa Mkuu wa mpango wa Kigali Innovation City. Kabla ya hapo, alishika wadhifa wa Mkuu wa ICT katika Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB)
Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB), ni idara ya serikali inayounganisha mashirika yote ya serikali yenye jukumu la kuvutia, kuhifadhi na kuwezesha uwekezaji katika uchumi wa taifa.
Bodi ya Maendeleo Rwanda (RDB) wanahusika; usajili wa biashara, uhamasishaji uwekezaji, uidhinishaji wa mazingira, ubinafsishaji, utalii, SMEs na ukuzaji wa uwezo wa watu katika sekta binafsi.
Bodi ya Maendeleo Rwanda (RDB) hupima mafanikio yake katika (a) uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni na ndani, (b) kuongezeka kwa mauzo ya nje na (c) idadi ya nafasi za kazi zilizoundwa.
Unaiona ile Visit Rwanda? Ndiyo kazi ya Bodi ya Maendeleo Rwanda (RDB). Wamesaini mkataba na Arsenal, Paris Saint-Germain, Basketball Africa League (BAL), Fußball-Club Bayern München, AFL.
Ukifungua portfolio ya Paula Ingabire inakueleza ni mtaalamu wa teknolojia na mwanasiasa kutoka Rwanda. Sasa fungua portfolio ya Waziri wako wa Teknolojia. Utakutana na BUMUNDA. INAKERA!
Lakini wanetu, kama nawakwaza, semeni..…
Brigedia Mtikila, MMM.