Je, Nchi kununua ndege wakati vijiji havina maji, ni sawa na mwenye nyumba kununua gari wakati hakuna bomba la maji?

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,863
2,000
Je, maamuzi ya nchi kununua ndege wakati tuna uhaba wa miundombinu ya maji, kunaweza kufananishwa na familia inayonunua gari, wakati haina hata bomba la maji nyumbani, ili hali inaomba maji kwa jirani mwenye bomba?

Kama ni ndio, Je, mwenye nyumba anayefanya maamuzi hayo anakuwa na lengo na madhumuni gani?
 
  • Thanks
Reactions: BAK

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,668
2,000
Fikiria pia katika mazingira haya:
huyo mwenye nyumba ana milion 5 tu , ambapo kuweka maji ni milioni moja na kununua gari ni 4, 500, 000. Je atafanya nini kati ya kununua gari na kuweka maji kwanza?

N.B: kumbuka gari atakalonunua litazalisha
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,604
2,000
Endelea kujiuliza hadi mradi unaisha utakuwa tayari umepata majibu
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,978
2,000
Tuliambiwa nchi yetu haiwezi kukosa ndege wakati vinchi vidogo vina midege kibao, so zilinunuliwa just for prestige
 
comred

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
1,867
2,000
Hili jamaa kumbavuu kwelii
Ndege na Maji vijijini vinamahusiano gani..?!?
Kila kimoja kinaumuhimu wake pale kilipo.
Hizi akili na mawazo ya kimaskini mtaachananazo linii?!?

"Mimi namiliki gari lakini napoishi kuna huaba wa maji, gari linaniwezesha/kurahisisha kwenye mizunguko yangu na nimeweza kuchimba kisima, sasa nina maji"
 
kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
4,682
2,000
Kuna vitu vya muhimu na vitu vya muhimu zaidi,kiongozi mwenye maono angelijua. Ingalikuwa ndege zitatuletea pesa za ziada tukasambzia maji haposaws lakini enyi watu msio na akili nzuri ninawaambia midege mnayonunua italeta hasara hatutopata zidio hata la kujnunua kiberiti!! Ni sifa tuu...sifa tuu!! Kisa Rwanda wanazo basi nasisi tununue...ni sifa tuuuuu.
 
relis

JF-Expert Member
May 24, 2015
2,737
2,000
Je, maamuzi ya nchi kununua ndege wakati tuna uhaba wa miundombinu ya maji, kunaweza kufananishwa na familia inayonunua gari, wakati haina hata bomba la maji nyumbani, ili hali inaomba maji kwa jirani mwenye bomba?

Kama ni ndio, Je, mwenye nyumba anayefanya maamuzi hayo anakuwa na lengo na madhumuni gani?
Kwa tunavyojuana waswahili ni kulialia tu,hata ikisitishwa ununuzi wa ndege mkatandikiwa mabomba kila chochoro nchi nzima maji mpaka mlangoni kila nyumba wakataka kununua ndege bado mtasema tena tununulieni na vikombe mtunyweshe hayo maji,kiujumla hamueleweki kabisa.
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
45,929
2,000
Je, maamuzi ya nchi kununua ndege wakati tuna uhaba wa miundombinu ya maji, kunaweza kufananishwa na familia inayonunua gari, wakati haina hata bomba la maji nyumbani, ili hali inaomba maji kwa jirani mwenye bomba?

Kama ni ndio, Je, mwenye nyumba anayefanya maamuzi hayo anakuwa na lengo na madhumuni gani?
Kila kimoja kina bajeti yake. Labda utuambie kuwa bajeti ya kusambaza maji imetumika kununua ndege.
 
Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,850
2,000
kila mtu ajikune pale anapoweza
msiishi maisha ya kukaririshwa na wazazi wenu
wanaopanda ndege tangu awali walikuwepo pia waliokosa maji tangu awali wapo
pia Mikoa ya Tanzania ni vivyo hivyo, ipo Mikoa mikame haswa km Dodoma na Singida na bado haina viwanja hata ndege Bomberdier ikienda Dodoma ina watu 15
Wakati Mbeya Kilimanjaro na Kagera vyote vipo na maji yanatiririka sasa sio lazima kuwasubiri Singida waletewa maji ya Victoria
 
prs

JF-Expert Member
Feb 22, 2013
2,642
2,000
Tatizo huelewi mada inazungumzia nini kaa utulie.
😂,Mleta mada kauliza swali Wewe ukamjibu kimipasho ,pengine hukuielewa mada,
Ndege kwa Akili zenu na Jiwe ni Fahari ya macho tu, hakuna faida itakayopatikana hapo.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
125,013
2,000
Ni ujinga wa hali ya juu ya huyo nduli kukurupuka pia kutojua vipaumbele vya Tanzania na Watanzania. Eti alishauriwa anunue ndege na Kagame? Who is Kagame to Tanzania!?

Je, maamuzi ya nchi kununua ndege wakati tuna uhaba wa miundombinu ya maji, kunaweza kufananishwa na familia inayonunua gari, wakati haina hata bomba la maji nyumbani, ili hali inaomba maji kwa jirani mwenye bomba?

Kama ni ndio, Je, mwenye nyumba anayefanya maamuzi hayo anakuwa na lengo na madhumuni gani?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom