Je, naweza kumshitaki aliyekuwa mpenzi wangu kwa kunitapeli tukiwa bado pamoja?

Samehe tu 7 mara 70! Hakuna namna. Ulitakiwa kuusoma mchezo kuanzia mwanzo. Sasa wewe ukawa unatoa tu kila uisikiapo sauti yake nzuri na ya kumtoa nyoka pangoni!

Ukienda kumshtaki kila mtu atakushangaa.
 
Kutapeliwa na mpenzi inauma yaani unajiuliza nilivyokuwa kichele alikuwa anakuwa ananichukuliaje huyu boya
 
Wewe ni kaka au dada?

Huyo mpenzi wako ni kabila gani?

Jumla ulituma sh.ngapi?

HIYO NI KESI YA WIZI WA KUAMINIWA. KAMA MESEJI UNAZO NA VOICE CALL UNAZO BASI HIZO HELA ZINARUDI.
 
Wanawake wenzangu wana bahati sana mie mbona siwaoni hao wanaume wa hivyo jamani
Wapo ila mpaka utembee na wanaume wengi tofauti tofauti ndio unaweza kupata ngekewa ya kukutana na mtu wako mmoja kama mleta mada. Ni kama "jackpot bingo", biko, tatu mzuka, patapata, bahati nasibu ya taifa tu kadiri unavyocheza mara nyingi ndivyo unapoongeza nafasi ya kushinda. Kwa hiyo hakuna cha bahati wala nini wewe jilipue tu kila anayekuja mbele yako twende nina hakika baada ya muda utakuwa na wewe umepata wako kama mleta mada. Vinginevyo njia rahisi mwendee mleta mada DM fasta uchukue nafasi iliyoachwa wazi kwani mleta mada hakusema kama kuna mwingine kashachukua nafasi.
 
Kiasi cha pesa ulichotapeliwa please!! Ndiyo ile laki 4?
Hahaaa hapa ndio nimeelewa, Niki relate na ule Uzi.
N. B siku zote kwenye mahusiano tutimize malengo yetu kuliko malengo ya wapita njia loh
 
Reactions: BAK
Kesi za uhawara kama hizo huwa hazichukuliwi uzito mkubwa, labda kama mmeumizana kwa kuchomeana nyumba ama kwa kuchomana kwa magunia ya mkaa.

Hizo kesi ni sawa na bibi kushitaki wajukuu zake kwa kuingia shambani kuvunja mahindi bila ya kibali chake.

Kwanza unapopeleka malalamiko, ukishaulizwa huyo mtu ni nani yako, ukiishasema tu 'ni mpenzi wangu', utakuta sura za wanaokusikiliza zinabadilika muda huo huo na pressure ya kuchukua hatua inashuka..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂😂😂 muanzisha uzi pesa yake bado inamuuma. Namuonea huruma kusema kweli. Pesa katiwa ndani, kugegedwa kagegedwa na jamaa anamletea UTEMI kwenye pesa yake. Maskini kaogopa kufungiwa tena kaja na ID mpya na baadhi ya facts kaamua kuzificha.
Hahaaa hapa ndio nimeelewa, Niki relate na ule Uzi.
N. B siku zote kwenye mahusiano tutimize malengo yetu kuliko malengo ya wapita njia loh
 
Mods wa JF hawakumtendea haki huyo mleta mada kabisa hafu hawakumfungia huyo member had akafungua Uzi kuwa kafiwa Ili aonewe huruma na asisakamwe kwa utapeli wake, and it seems huyo kaka ana mwanamke mwingine ndo yakazaa hayo, eeh bidada akamloge au asante mazima, ila ingekuwa Mimi angezitapika hizo hela wallah
 
Nyie ndo mnafanya wachaga tunaonekana bahili Sasa imagine huyo mwanamke akutane na Mimi ambae naulizia chenchi akirudi kufanya manunuzi si ndo utasikia "Loooh mwanaume husahau??" nisahau nini? embu naomba chinchi yangu nisije nikakuzabua vibao Hadi unukie stonetangawizi.
 
hahahahahaha you nailed her sorry a55
 
Kofi la Mpenzi haliumi.

Haina haja, alikutapeli mapenzi yalipokuwa motomoto.

Kesi hakuna hapo
 
Hapo hakuna jinai, hata ukienda kushitaki utaambiwa mkamalizane kindugu. Kumalizana kwenyewe ni kufufua penzi, upo tayari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…