Je nahitaji kujua sababu ya kumsamehe????

TaiJike

JF-Expert Member
Dec 14, 2011
1,483
667
Hello JF,
Ninapokuwa nimeudhiwa na mpenzi wangu nahitaji kujua sababu ya kwamba kwanini kafanya hivi ama vile au kumweka masharti ya msamaha?
 
Kama unaona ni muhimu kwako uliza, kama sio muhimu samehe tu mpaka siku utakapochoka.
 
Ni vizuri kusamehe, na pia ni vizuri kujua sababu ya mtu kutenda kosa ...
Kujuwa sababu inaweza kukusaidia kufahamu source ya tatizo na kumshauri kubehave in a way ambayo hawezi kufanya kosa tena. Sabubu zingine zinaweza kuwa hata zimesababishwa na wewe mwenyewe kutokuwa karibu naye ....
Tafakari ....
 
Asanteni wote kwa ushauri, lakini hii saba mara sabini hamuoni ndo itakuwa lift yake kuwa kila akikosea atasamehewa?
 
Asanteni wote kwa ushauri, lakini hii saba mara sabini hamuoni ndo itakuwa lift yake kuwa kila akikosea atasamehewa?

Dini ndivyo inavyoshauri.

Binafsi nakushauri samehe (as in kupotezea na kuendelea na mahusiano) pale tu unapoona mhusika anastahili. Zaidi ya hapo utakua unacheza rumba wakati mwenzio kaweka kanda ya bongo fleva na hayuko tayari kubadilisha.
 
Hapo umenena my dia.
 
Ni vizuri kusamehe, na pia ni vizuri kujua sababu ya mtu kutenda kosa ...
Kujuwa sababu inaweza kukusaidia kufahamu source ya tatizo na kumshauri kubehave in a way ambayo hawezi kufanya kosa tena. Sabubu zingine zinaweza kuwa hata zimesababishwa na wewe mwenyewe kutokuwa karibu naye ....
Tafakari ....

HorsePower, umbali si kigezo cha mtu kumkosea mwenzie inategemea ni kipi kinawaweka mbalimbali, pengine ni kutokana na majukumu ya kikazi kwa hili sikubaliani nalo hata kidogo.
 
ni vizuri kufahamu sababu ya kosa kisha kusamehe kama unaweza, wengine wanafanya makosa ya makusudi sijuwi kwa lengo gani, :embarassed2::embarassed2:
 
Jee wewe ukikosea unataka upigwe kibuti kwa mara ya kwanza tu?

Mtenda akitendewa..........
 
Samehe ukiwa tayari kusamehe kuliko kusamehe usoni moyoni una kinyongo.
 
Hakuna binadamu aliekamili kila mmoja ana mapungufu yake, lakini kuna mengine hayabebeki kila mara kosa ni lile lile miaka nenda rudi, kama ni uwongo hapo ni warehouse, uzinzi fisi maji cha mtoto najaribu kutoa mifano tu.
 
TF,
Nshasamehe sana swali langu ni kuwa je nahitaji kuendelea kujua sababu za yeye kukosea kila kosa? maana ishakuwa tabia je kuhitaji sababu si ndo kuruhusu kupewa uongo?
 
Hello JF,
Ninapokuwa nimeudhiwa na mpenzi wangu nahitaji kujua sababu ya kwamba kwanini kafanya hivi ama vile au kumweka masharti ya msamaha?

...kwanza jiulize mwenyewe; kwanini uudhike kwa jambo usilolijua (?)
 
@ Mbu, unajua wengine kiswahili tumekutana nacho shule labda niseme kwanini nihitaji utetezi wake. badala ya kwanini kafanya hivi ama vile.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
@ Mbu, unajua wengine kiswahili tumekutana nacho shule labda niseme kwanini nihitaji utetezi wake. badala ya kwanini kafanya hivi ama vile.

...usijali, hata mie ni hivyo hivyo.

...hapo kwenye kuhitaji utetezi utajuaje anakudanganya au anakwambia kweli?
kumbuka, sikio lako pekee ndilo linalochagua maneno ya kukubalika au la...

...unless unajifarijisha kwa maneno hayo, otherwise huna haja ya kujua sababu.
 
Samehe tu Ndugu....
Japo wakati mwingine inauma...
Ila hamna njia nyingine zaidi ya kusamehe..
SAMEHE!
 
Asanteni wote kwa ushauri, lakini hii saba mara sabini hamuoni ndo itakuwa lift yake kuwa kila akikosea atasamehewa?

usichoke kusamehe,maana tumeumbwa kukosea sisi siyo malaika,samehe kila unapokosewa bila kuweka moyoni rafiki
 
Back
Top Bottom