Je mnalijua shamba la miili ya watu…….?


Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Shamba hili lilianzishwa miaka 31 iliyopita huko nchini Marekani wakati Dk. William Bass alipokuwa akitafuta namna ya kuchunguza mwili wa mtu baada ya kufa. Mnamo mwaka 1981, Daktari huyu alimuuliza mkuu wa kitivo cha sayansi cha chuo kikuu cha Tennessee kama anaweza kutumia sehemu ndogo ya chuo hicho kuweka miili ya watu waliokufa kwa ajili ya kuifanyia utafiti na huo ndio ukawa ni mwanzo wa kuanzishwa kwa shamba hilo ambalo lilikuja kujulikana kwa jina la Anthropology Research Facility.

Kilichofanyika ni kwamba, kituo hicho kiliomba watu wajitolee kukubali miili yao kutumika na kituo hicho pale watakapokuwa wamekufa na baada ya makubaliano hayo watu hao wanapokufa miili yao huchukuliwa na kutupwa katika shamba hilo kwa namna tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya utafiti.

Ipo miili inayotupwa kwenye maji yasiyo na kina kirefu, kutelekezwa kwenye nyumba au nyuma ya gari, kutupwa sehemu ya wazi na mingine inafukiwa kwenye kaburi fupi tu na utafiti hufanywa siku nne tangu mtu huyo afariki. Kwa kutumia sayansi ya wadudu, wataalamu hao wanaweza kugundua kwa usahihi kabisa siku mtu huyo alipofariki kutokana na aina ya funza watakaokutwa katika mwili huo.

Kwa kawaida mtu anapokufa mwili wake hushambuliwa na funza. Wale funza wa awali wanaposhambulia mwili huo pia huutayarisha kwa ujio wa funza wengine na hutofautiana kwa muda maalum, kutoka aina moja kwenda nyingine na hapo ndipo wanasayansi hao kwa kutumia aina ya funza na wadudu wengine waliowakuta katika mwili huo hujua kwa usahihi kabisa kwamba mtu huyo alikufa kipindi gani au mwili wake ulitelekezwa mahali hapo wakati gani. Pamoja na utafiti wa wadudu, pia mazingira ya eneo husika (Scene of crime) na hali ya hewa ya eneo hilo kijiografia kulingana na msimu, kwa mfano msimu wa baridi, joto nk, huzingatiwa ili kufanikisha utafiti huo.

Leo hii kupitia shamba hilo la miili ya watu, wataalamu wa kisayansi wa kutatua sababu ya vifo visivyo vya kawaida wamefanikiwa sana kufanya tafiti mbalimbali ambazo zimetumika kutatua kesi nyingi za mauaji nchini Marekani. Kupitia utafiti huo hivi sasa, bila kujali mtu amekufa lini, mwili wa mtu unaweza kutoa majibu sahihi sawa sawa na mwili wa mtu aliyekufa hivi punde.

Mpaka sasa kuna watu 300 ambao wamejitolea miili yao ili kusaidia kituo hicho kufanya utafiti na inaelezwa kwamba zaidi ya miili 120 hupokelewa na kituo hicho kila mwaka. Kutokana na mafanikio ya kituo hicho, hivi sasa kuna vituo vingine vinne vimeanzishwa katika majimbo mengine kwa lengo hilo hilo la kutatua vifo visivyo vya kawaida na kesi za mauaji nchini humo, vituo hivyo ni:

-Texas University kilichopo San Marcos

-Western Carolina University kilichopo Cullowhee kituo hiki pia hutumika kwa ajili ya mafunzo kwa mbwa wa kunusa (Cadaver dogs).

-Sam Houston University kilichopo Huntsville

-Southwestern Pennsyvania ambacho kinatumiwa na watafiti wa Chuo kikuu cha Carolina huko Pennsylvania.
 
Gunda66

Gunda66

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
507
Points
225
Gunda66

Gunda66

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
507 225
Sina usemi, zaidi ya kuwapongeza watafiti,, bigup nyingi kwao :A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up:
 
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Messages
7,464
Points
1,250
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined May 21, 2012
7,464 1,250
nakiri hivi tanzania hii huwezi pata madactari wenye kuona mbali namna hiii wengi hubeba kile tu wlichofundishwa basiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,thinking outside the box never ever and ever

lakini tukitafuta madactari wenye kubuni njia za kutoa mimba bila kupata madhara utawapata wengi tuuuu
 
rosemarie

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Messages
6,826
Points
2,000
Age
43
rosemarie

rosemarie

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2011
6,826 2,000
The Research Facility, opened at its present location in 1980 by Dr. William M. Bass, provides an ideal setting to scientifically document postmortem change. This outdoor field laboratory enables the investigation of parameters which are crucial in time since death estimates. Donated remains make this research possible and simultaneously provide a modern osteological teaching collection. Presently, this demographically-rich collection consists of almost 650 skeletons and growing. These individuals are essential for providing education and training in forensic anthropology and skeletal biology for students and law enforcement agencies. They are also invaluable for updating demographic and biological standards. Please contact Dr. Dawnie Steadman regarding use of this facility.
 
piper

piper

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2012
Messages
3,257
Points
1,195
piper

piper

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2012
3,257 1,195
Ama kweli kua uyaone mengi, thanx Mtambuzi kwa kutuhabarisha
 
Nicas Mtei

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Messages
11,566
Points
1,250
Nicas Mtei

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2010
11,566 1,250
mkuu Mtambuzi ahsante kwa article hiyo
 
Last edited by a moderator:
M

mwimbule

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2009
Messages
520
Points
225
M

mwimbule

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2009
520 225
hawa wamejitambua hata viongozi wao hawafichi pesa ulaya au afrika.
 
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
12,185
Points
2,000
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
12,185 2,000
Mtambuzi, Big up mkuu!! Yaani wewe ni sawa na wale wanasayansi kabisa maana unatuwekea nyuzi nyingi za akili sana. Wanapokea na wa huku? Ningejitolea tu.
 
Paloma

Paloma

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2008
Messages
5,336
Points
1,195
Paloma

Paloma

JF-Expert Member
Joined Jan 22, 2008
5,336 1,195
thank you sana Mtambuzi

je kuna hata kimoja bongo? au africa?

aysee......
 
Last edited by a moderator:
majany

majany

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2008
Messages
1,225
Points
1,225
majany

majany

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2008
1,225 1,225
Mi nakwambia vingeanzishwa huku bongo,ndo ungeona wenye dini zao,wangeongea weeee...na hata hicho kituo kuhusishwa na FREEMANSONS......au mkakati wa wakristu kumaliza watu!!!!
Thanks kwa information!!
 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
thank you sana Mtambuzi

je kuna hata kimoja bongo? au africa?

aysee......
@Paloma

Yeah kipo kituo kimoja na kinapatikana huko MSITU WA MABWEPANDE

Unaruhusiwa kukitembelea kwa ajili ya kujifunza, ni PM nitakupa namba ya simu ya wahusika................LOL

 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Mi nakwambia vingeanzishwa huku bongo,ndo ungeona wenye dini zao,wangeongea weeee...na hata hicho kituo kuhusishwa na FREEMANSONS......au mkakati wa wakristu kumaliza watu!!!!
Thanks kwa information!!
Umesema kweli, nakumbuka miaka ya 1990 chuo cha kitabibu cha IMTU kilichopo Mbezi Beach kiliwahi kuzua kasheshe baada ya kuchukua mwili wa mtu aliyekufa sina uhakika kama ilikuwa ni Muhimbili kwa ajili ya wanafunzi kuufanyia utafiti, kama sikosei.

Jambo hilo liliandikwa kwenye vyombo vya habari kukazuka malumbano makubwa sana, hata siju yaliishia wapi.
 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Mtambuzi, Big up mkuu!! Yaani wewe ni sawa na wale wanasayansi kabisa maana unatuwekea nyuzi nyingi za akili sana. Wanapokea na wa huku? Ningejitolea tu.
Unaweza kuwasiliana nao lakini kwa mfano kituo cha Chuo Kikuu cha Tennessee kimependekeza kwamba mtu yeyote anayetaka kujitolea mwili wake utumike kwa utafiti hatakiwi awe anaishi umbali wa maili 200 kutoka katika mji wa Knoxville nchini Marekani, mji ambao ndipo kilipo kituo hicho cha utafiti.

Anuani yao hii hapa:

[h=3]Forensic Anthropology Center
Department of Anthropology
[/h] 250 South Stadium Hall
Knoxville, TN USA
37996-0760


Phone: 865-974-4408
Fax: 865-974-2686
Email: fac@utk.edu
 

Forum statistics

Threads 1,285,256
Members 494,502
Posts 30,855,589
Top