Je, Mjamzito kupata hedhi kuna tatizo?

Je, Mjamzito kupata hedhi kuna tatizo?

Baadhi ya wanawake hill linatokea. Wakati mimba inatungwa na inaendeleea ... Kuna vimishipa ambavo huachia ili kueza kujishika kwenye kizazi hivyo hupelekea mwanamke kuona siku ambazo hazifanani na siku zake za kawaida yaani huwa pungufu.

Kuliko kawaida dalili hizo zinatokea kwa baadhi ya wanawake. Ni vizuri kumpima ili kuhakikisha kweli ..Kama ndio mjauzito au la ili kuchukua tahadhari za kiafya Kama kweli atakua mjauzito.
 
Hata kama uwezekano upo Lakini kisitumike kama kigezo cha kutudanganya wanaume
 
Nasikia inawezekana
Kuna best yangu alikuwa anayo ila hakugundua kama anayo(kwa madai yake miezi mitatu ya mwanzo wa preg alikuwa anaenda period kama kawaida)
 
Ni abnomality hiyo na inabidi aende hospitali... Ukizembea atapoteza hiyo mimba
 
Na mimi nilitaka nianzishe uzi kama huu..nimepata shida kama hii..mwezi wa tatu sikuona siku zangu nikapima nikaona nina mimba...ila tangu jana nimeanza kuona damu na leop asubuhi bado kama inaanza kuongezeka.nitaenda hosp ,manake naona maajabu
 
Huwa inatokea mara chache na ni huwa mtu anapata na tatizo na ni muhimu kumkimbiza hosptal
 
Na mimi nilitaka nianzishe uzi kama huu..nimepata shida kama hii..mwezi wa tatu sikuona siku zangu nikapima nikaona nina mimba...ila tangu jana nimeanza kuona damu na leop asubuhi bado kama inaanza kuongezeka.nitaenda hosp ,manake naona maajabu
Wahi hospitali mkuu
 
Nenda hospitali. Uchunguze maendeleo ya mtoto kwa kipimo cha ultrasound. Kwa experience wanawake ambao wanaokuja kwa kipimo cha ultrasound wanaotaka kuangalia umri wa ujauzito, unakuta mtoto tumboni umri wake ni mkubwa kuliko tarehe ya mwisho ya hedhi yake ambayo anapopenda clinic wanamwambia. Mama anapokua mjamzito huwa wengine damu huwezi kuiona mpaka kujifungua ila kunawengine unakuta ni mjamzito anapata sport za damu.

Kwa mama ambaye ni mjamzito anapaswa anapoona sport lazima aende kuangalia maendeleo ya mtoto tumboni. Hvyo ukiona unapata sport na ni mjamzito wakati mwingine ni kawaida ila ukiona heavy bleeding tafadhali nenda ukafanyiwe kipimo cha ultrasound huenda kondo la nyuma yani placenta liko kwenye mlango wa kizazi au limekaribia kwa kitaalam tunasema (placenta praevia ) au unakuta labda kondo linaweza limengofoka kusababisha heavy bleeding kwa kitaalam tunaita (placenta abraption)
 
inategemea kuna baadhi damu huwa inatoka kidogo kidogo wahini hospital
 
Yes upo uwezekano mkubwa, muonane na wataalamu kujua usalama wa Mtoto.
KIFUPI AAMBIWE KUWA kama mwanamke wake anaingia hedhi wakati ni mjamzito, basi ni tatizo, aonane na daktari....

Maana nilivyomuelewa anataka ajuwe kama ni kawaida au kuna tatizo
 
mkuu mke wangu alikua mjamzito wa miezi sita ila ilipofika tarehe 5 mwezi huu alisikia maumivu ya tumbo alipoenda kukojoa akaona na damu kidogo kama bleed na muda huo maumivu ya tumbo yakawa yanaongezeka tukaamua kwenda hospital huku akilia maumivu makali.

Tulipofika hospital mimi madokta wakanitoa nje wakaa kama dk 5 wakatoka wakasema mtoto ameshafariki inabidi waokoe maisha ya mama, wakampa madawa akajifungua mtoto aliyefariki, hiyo kitu kiukweli imetuathiri sana na hadi leo hii mke wangu yuko so traumati muda mwingine anajifungia unakuta analia tu, jitahidi yasikukute yaliyonikuta mimi!
 
Na mimi nilitaka nianzishe uzi kama huu..nimepata shida kama hii..mwezi wa tatu sikuona siku zangu nikapima nikaona nina mimba...ila tangu jana nimeanza kuona damu na leop asubuhi bado kama inaanza kuongezeka.nitaenda hosp ,manake naona maajabu
ni vyema ukatafute ushauri wa mtaalamu manake hii leo nimeandamana na mke wangu na tukapata kufaham mengi...kuna mambo kadhaa ambayo yaweza kuwa visababishi vya jambo hili..mengine ni very serious na mengine kawaida tu..kama ikizidi siku mbili na iwe imekolea ni vyema ufanye mpango wa kuonana na daktari au ukitembelee kituo chako cha kliniki manake yaweza kuwa hatari sana...
 
kayaman,
samahani mkuu...pole sana kwa kufikwa na hayo..hili jambo huenda watu wasilichukulie la maana ila adhari zake niza kuatua moyo..
 
Baadhi ya wanawake hill linatokea ... Wakati mimba inatungwa na inaendeleea ... Kuna vimishipa ambavo huachia ili kueza kujishika kwenye kizazi hivyo hupelekea mwanamke kuona siku ambazo hazifanani na siku zake za kawaida yaani huwa pungufu. Kuliko kawaida dalili hizo zinatokea kwa baadhi ya wanawake.... Ni vizuri kumpima ili kuhakikisha kweli ..Kama ndio mjauzito au LA ili kuchukua tahadhari za kiafya Kama kweli atakua mjauzito
hili ni kweli mkuu..ni jambo la haja sana wanawake wajawazito kutembelea vituo vyao vya kliniki kwa muongozo katika utunzaji wa mimba..
 
Sayansi niliosoma Mimi, inasema hivi mwanamke akipata mimba cervix yake inafunga hadi siku akijifungua, ikitokea imefunguka ndipo na mimba hutoka, kumbuka na hiyo damu ya hedhi inapitia mlango huo huo, kingine matokeo ya hedhi ni kupevuka kwa yai na kupasuka hii huchochewa na hormone inayoitwa estrogen,

akipata mimba hiyo hormone ya estrogen hushushwa chini na hormone nyingine inayoitwa progesterone hii husaidia uleaji wa mimba na kuzuia mwanamke kupata hedhi na huwa juu kipindi chote cha mimba.

hayo mengine ya kuingia siku akiwa na mimba sio jambo la kawaida ujue kuna tatizo kisayansi hatakiwi kupata hedhi tena akipata mimba tu.
 
Back
Top Bottom