Je, Mh. Rais katususia nchi?

Je, Mh. Rais katususia nchi?

Hivi Mnyika na elimu yake ya kubumba ulitegemea aseme nini? Nenda kwenye tovuti ya bunge hata shule alizosoma hazijaoneshwa?

Na wewe elimu ya kukariri na kukufanya kibaraka wa watawala huku mkishirikiana kuifisidi nchi imetusaidia nini? Heri Mnyika mwenye elimu ya kawaida lkn yenye faida kwa nchi yupo upande wetu, kuliko mliosoma mkamaliza madarasa na sasa mnashirikiana kubomoa nchi!
 
Inashangaza sana. Mambo makubwa anampa Salva aongee kama vile Salva ndiye mkuu wa nchi! Ni kama aliutaka urais kama fasheni bila kuwa la visheni kuwa anataka kuifanyia nini nchi!
 
Mimi nina swali kwa Mh. Raisi, hivi kaamua kutususia Nchi au, maana kuna matatizo lukuki hapa Nchini yanaendelea na yeye yupo kimya, mfano ni Mfumuko wa bei, wanafunzi kufeli kuliko kawaida, vurugu za kidini, bunge kugeuka kijiwe na mengineyo mengi tu, Mh. Raisi ndio kiongozi wa Nchi ameamua kukaa kimya, kwa sasa ni kama Nchi inajiendesha/inajiongoza yenyewe hakuna kiongozi.

Mmemchagua wenyewe. Halafu 2015 mtawachagua tena. Misiba ya kujitakia haina kilio. tutavuna tulichopanda
 
Back
Top Bottom