Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,250
- 3,451
Tulipata fununu huko JamiiForums na kuambiwa kama mambo yakiharibika kabisa basi pataitishwa baraza la siri la wazee na makachero wabobezi wenye siri za Taifa hili na ndani ya kikao hicho yatasemwa mengi mepesi na mazito baada ya hapo kachero wa siri ambaye amewahi kuwa katika vyumba vya siri vya Taifa atakuwa amekabidhiwa karatasi ya siri kutoka katika vyumba vya siri vya Taifa, ndipo itasomwa wenye nguvu watalia na kufuta machozi wenye imani ndogo watazimia na kukimbizwa hospital za siri za Taifa.
Baada ya hapo atachaguliwa mzee mmoja ambaye anaheshimika sana katika michakato mbalimbali kama ule wa Katiba Mpya mwenye kukubalika na Chama tawala, atapanda kwenye mimbari na kutoa mwelekeo mpya wa Taifa la Tanzania, na hapo litapatikana Taifa jipya la haki na amani.