Je, Mchungaji/ Askofu Gwajima anakaribia kufifia na kupotea kwenye majukwaa?

Mugabe one

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
2,327
1,684
Wana JF,

Ingawa yameandikwa katika Bibilia kuwa Siku za mwisho yatatokea mambo mengi sana pamoja na watu kupenda Pesa zaidi kuliko neno la Mungu, kuliko hata wazazi wao nk. Narudi kwenye hoja yangu fupi katika kujua kuna baadhi ya viongozi wa dini kama Askofu Kakobe, Mchungaji Maboya, nk wamepotea kabisa au kufifia.

Inawezekana kweli kwamba kuna baadhi ya wachungaji/ maaskofu wa kilokole huvuma sana kwa nguvu za ziada na baadaye wanafifia hasa baada ya kuanzisha mivutano na serikali. Je hata Mchungaji Gwajima karibu atafifia na kupotea? Je ni sababu zipi zinawafanya wafifie na kupotea kwenye majukwaa ya ubabe wa makanisa yao?
 
Aisee sababu ziko nyingi inategemea mkuu ila huko kujiingiza kwenye siasa kubaya...Usishangae akapotea
 
Wana JF Ingawa yameandikwa katika bibilia kuwa Siku za mwisho yatatokea mambo mengi sana pamoja na watu kupenda Pesa zaidi kuliko neno la Mungu, kuliko hata wazazi wao nk.
Narudi kwenye hoja yangu fupi katika kujua kuna baadhi ya viongozi wa dini kama Askofu Kakobe, Mchungaji Maboya, nk wamepotea kabisa au kufifia. Inawezekana kweli kwamba kuna baadhi ya wachungaji/ maaskofu wa kilokole huvuma sana kwa nguvu za ziada na baadaye wanafifia hasa baada ya kuanzisha mivutano na serikali. Je hata MCHUNGAJI GWAJIMA Karibu atafifia na kupotea? Je ni sababu zipi zinawafanya wafifie na kupotea kwenye majukwaa ya ubabe wa makanisa yao?
Leo ndio unamuona ''shujaa' Gwajima atapotea na wakati akimsakama Mh Makonda mlimsifia na kumpamba kwa kila mapambio hakika Mungu huwaonyesha wanafiki ,leo hii kamponda mwendawazimu wenu mumeshaanza kumuona tena Gwajima si wa maana,sisi tuliposema Gwajima ni tapeli wengi mlitoa viroba vya matusi kama ilivyo kawaida yenu nyie wenye vinasaba vya Ufipa,si hata Nape hivi sasa mnamuona mtu wa maana wakati ni siku chache tu hapo nyuma mlimpa kila aina ya majina na matusi ya kila aina.Nyie watu wanafiki sana.
 
Nadhani waumini wake wengi labda ni wa kundi la walioitwa KULIPOTI CENTRAL POLICE!
 
Back
Top Bottom