Kwanini mitume na manabii huishiwa upako baada ya muda? Je, hizi pako zao ni za kweli au za mchongo?

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,793
18,216
Jambo wadau?

Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha na maneno mengi. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia upako wa manabii na mitume jinsi wanavyoanza huduma zao kwa pako za hali ya juu sana lakini baada ya muda zile pako huanza kufifia taratibu na kuisha kabisa. Nabaki najiuliza maswali kadhaa yasiyokuwa na majibu:
  1. Kwanini pako za hawa manabii zinapanda na kushuka ghafla kiasi hiki?​
  2. Je, hizi pako ni za kweli au ni za mchongo?​
  3. Kama ni za kweli kwanini zinaisha na kama ni za mchongo kwanini zikiisha wasirudi tena kuchukua nyingine kule wanakozitoa?​
Yaani najiuliza maswali mengi bila majibu. Ndipo nikaamua kuanzisha huu uzi kwa kuwa humu JF kuna wabobevu wa masuala ya theology akina Mshana Jr wanaweza kutusaidia kujibu baadhi ya maswali haya.

Hebu jaribu kufikiria nguvu za upako alizokuwa nazo Askofu Kakobe enzi zile anafungua kanisa lake la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) halafu ulinganishe na hali aliyo nayo sasa hivi utagundua kuna kitu hakiko sawa. Si huyu tu bali walikuwepo Mitume na Manabii wengi hapa nchini wakiwemo Mzee wa Upako, Mch Antony Lusekelo ukiangalia jinsi alivyokuwa akikusanya mtiti na mabasi yake kila kona ya nchi halafu leo ukienda kule kanisani kwake unakuta mabasi yote yamepaki unabaki unashangaa. Hapa lazima kuna tatizo sio bure.

Ukitoka kwa hawa wawili njoo kwa Mtume Mwingira na Mtume Gwajima ujiulize zile nguvu walizokuwa nazo zamani zilipotelea wapi hadi sasa wamebaki na waumini wa kuungaunga. Tatizo ni nini hasa?

Manabii na mitume waliovuma siku za nyuma na kupotea kimuujiza ni wengi lakini nimetoa mifano ya hawa wachache kama msingi wa kujenga hoja yangu. Sasa hivi Mtume Mwamposa ndiye yupo juu lakini naye atakuja kuporomoka baada ya muda mfupi.

Njooni wajuzi wote tujadiliane hili jambo mpaka tupate jawabu la pamoja.

Nawasilisha.
 
Gwajima sio mtume, na bado yupoyupo sana, Mwingira anamiliki shekeli za kutosha, makanisa kila Kona, benki, mashamba, kimsingi ana mihela, Kakobe serikali ilimtapeli mabilioni yake halafu wakampelekea mamluki wampindue!!! wa upako umesema magari yamesimama yote duh, hii sijui
 
Jambo wadau?

Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha na maneno mengi. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia upako wa manabii na mitume jinsi wanavyoanza huduma zao kwa pako za hali ya juu sana lakini baada ya muda zile pako huanza kufifia taratibu

Nawasilisha.
Asante sana na asante kwa mada hii iliyokuja wakati sahihi kabisa .. Naomba nitarejea na maoni yangu
 
Jambo wadau?

Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha na maneno mengi. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia upako wa manabii na mitume jinsi wanavyoanza huduma zao kwa pako za hali ya juu sana lakini baada ya muda zile pako huanza kufifia taratibu na kuisha kabisa. Nabaki najiuliza maswali kadhaa yasiyokuwa na majibu:

Nawasilisha.
Asante sana na asante kwa mada hii iliyokuja wakati sahihi kabisa .. Naomba nitarejea na maoni yangu
 
Back
Top Bottom