wanaosema mbowe asisakamwe kwa sasa, wanashangaza sana. Ni mbowe huyuhuyu alishiriki kujenga imani kwa wafuasi wake kuwa CDM, ndio chama mama kwa matumaini mapya.
Roho nyingi za waja, zikateketea kwa ajili ya harakati zake na chama kama taasisi. damu zikamwagika kwa ajili ya vita watu kuwa upande wake.
Ni vibaya Mbowe kujitenga kwenye mchakato huu, maana damu za akina akwilina zinamdai jambo. jambo lenyewe ni Tanzania mpya ambayo watoto wa wataifa moja watasoma shule bora, ambazo hazitoleta ubaguzi wa kipato.
Nchi ambayo, watu wake hawatashindia mlo, nchi ambayo famalia fukara hazitoishia kuzishangaa familia tajiri za kisiasa.
Binafsi sio fundi wa elimu za kiroho, ila nina imani kwa vita ambayo mbowe aliianzisha, bado ana deni kubwa sana akikikwepa kikombe hiki.
Sawa, anaweza kujiona ameshinda kwa macho ya nyama na akaamua kuuchuna asijue nini kinaendelea. anaweza kuitazama misukosuko ya kina Heche na Lissu, kupitia kwenye side mirror, akiona nyakati zake pia zilishapita, ila kiroho bado ana deni linalomkata maini.
kimsingi, kama anaitwa mwamba wa siasa za kipinzani, basi afanye hayo hadi tone lake la mwisho. ajifunze kusamehe kama ambavyo walimpokea lowasa na kugombea urais. ajifunze kukubali mwanzo mpya, ikumbukwe hata yeye walimvumilia.
Sidhani huko aliko anafurahia kina lissu kuswekwa ndani, kama anafurahia, sioni kama ni siha njema kwa mustakabali wa damu ziizokwisha kumwagika kwa ajili yao.
Aidha nijuavyo, mwanasisa shupavu huenda na dira ya msimamo wake hadi mwishoni.
Hayo ya kulambwisha mlungura, hatuyafahamu, tunachojua ni kwamba mbowe una haja kumaliza kazi.ulioanzisha na kuaminisha wanazengo kuwa CDM, ndio kimbilio lenu.
kama waswahili hunena, kila mmoja atabeba msalaba wake, mimi naamini msalaba wa CDM, Pia utaubeba. haiwezekani watu waingizwe kingi kisha waache solemba.