Je mawaziri wetu wana mgomo baridi?

Wangepinga wangejiuzuru tu,otherwise hayo ni maneno tu ya kwenye kisutu cha kanga,maiti anakoshewa na biharusi anapambiwa hizo hizo na mtoto hubebewa.
 
Nchi inaendeshwa kama lori la maji taka
Hahahahaha umenikumbusha lile lori linalobeba kinyesi, siku lilipita pale ubungo wahuni wakajua ni wese, kufungua koki wakakuta kimba linadondoka tuuu
 

Sijaona bado tatizo la Rais wetu Mpendwa Magufuli na Mkuu wetu wa Mkoa Kipenzi cha wengi Paul Christian Makonda na nadhani utendaji wao ni mzuri mno na kama ikiwezekana Wote wanaweza kutuongoza maisha Watanzania.
 
Ukweli upo mkuu, mawaziri ni kama wapo wapo tu, hakuna hats wanalofanya likathaminika.
Katika mazingira ya sipangiwi fomu nilienda kuchukua mwenywe,na ukiniingilia ndio umepoteza kabisa waziri mwenye tafakuri sahihi anajua hii ngoma ina mwenywe, tu mwache aicheze, lakini siku zote ngoma ya mtu mmoja haidumu na wala hainogi.
 
Raisi bado anaimani na rc wa DSM, Hivo atuna budi kumusupoti. Hakuna namna nyingine.
 
Bashite ana nguvu zaidi ya PM....shangaa pia ana nguvu zaidi ya Mama wa Kwanza!!! Kijana wa kwanza amzidi Mama wa Kwanza!!!

Nadhani wale jamaa walioenda kolomije mganga kawaambia mkifika tu mkuu anawachamba wananchi maana baada ya kurudi south kawa na nguvu mpya
 
Acha hizo propaganda zisizo na Msingi mfano tu Jana pale Ubungo Prof Mbarawa ametoa maelezo mengi kuhusu mradi wakati Rais akiweka jiwe la msingi na ndiye aliyemkaribisha Mkuu wa Nchi.

Na hata ziara ya Rais kusini mwa nchi mikoa ya Lindi na Mtwara mawaziri zaidi ya 6 waliongoza na Rais na ndiyo walikuwa wakitoa Maelezo ya miradi mbalimbali,mfano maji,umeme,barabarani n.k

Tusiandike tu mradi tunataka kumkosoa Rais basi ni kulaumu tu kila kitu wakati si kweli na ndiyo maana sometimes tunaweza kuwa na vitu vya maana ktk mitandao lakini kwasababu tunabase ktk kubeza tu basi kila mada zinaonekana haina maana.

Mawaziri wapo na wanafanya kazi zao kama kawaida ktk Wizara zao.
 
Lazima mkubali kwamba kuna makabila si ya kupewa madaraka makubwa na nyerere aliliiona hilo lakin ccm wakalipuuza maana hawajui hulka za makabila .wengine wanatakiwa waachwe waendelee kuwa wa majarubani tu.
Hakuna cha kabila wala nini - ni hulka ya mtu binafsi. Kwanza huyu amejipachika kabila kubwa wakati kakabila walikofikia wazazi wake walipokimbia vita ya Burundi ni kadogo sana, kama sio wazinza ni wasubi hapo Biharamulo. Kwa hivyo, akili ndogo na elements za udikteta havina mahusiano na kabila. In fact, wasomi wa Kisukuma wangefanya utafiti na kuuweka kwa uwazi kuwa huyu sio msukuma bali anawaharibia tu sifa nzuri waliyo nayo ya upendo na usikivu.
Kutetea vitendo vya Bashite kukosa maadili, sijonze amethibitisha kuwa ni a notorious abuser of power!
 
Rc kawaficha mawazir wote....hadi ipg!
Kimya.....rc ni kilaka

OvA
 
Kwa sasa kiitifaki anaanza
Sizonje anafuatia Makonda

Kingne Makonda ana hudumia wizara zote unazozijua
Na ana nguvu za kujipachika kuliko PM. Na wala yeye mwenyewe hajidhtukii. Kuna watu wana roho ngumu, hata tafakari hawana.
 
Wanapata mishahara ya bure. .kz zote kuna anae wafanyia so mmeona bw, nape kaunda tume asubuhi saa 4.majibu tayari. Mwakyela kapiga marufuku ndoa bila cheti akapewa za uso. Sasa yupi tena. Wa chakula kasemewa kipo tatizo nn tena ?
Leo(jana 20-3-2017),nmeshuka stendi nikakuta watu yaani normal people ambao ungehisi wana upeo mdogo kabisa walikua wanaongelea issue ya Dr Mwakyembe na hii ya pale Ubungo. Walisema hata nyumbani kwenye familia mambo ya ndani hayafanyiki kwa style ile hasa kama ilivyotokea kwa Dr Mwakyembe. Wakalaumu aina hii ya utendaji. Kwa kweli Watanzania hawa hawa wa kawaida kumbe wako makini kufuatilia mienendo. Natabiri 2020 kipute kuwa kigumu mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…