Je, Mawaziri Mulamula na Mbarouk watakula kiapo kabla ya kuwa Wabunge?

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,494
37,787
Nianze kwa kumpongeza Mh Rais Samia kwa jinsi alivyoisuka Wizara ya mambo ya nje kwa mustakabali diplimasia ya taifa letu. Lakini Jana baada ya kutangaza uteuzi wao aliahidi kuwaapisha leo saa 4 asubuhi vuwanja vya Ikulu.

Ninachoomba kujua, Je wataapa Uwaziri kabla ya kuwa Wabunge kamili? Au wataapishwa haraka haraka bungeni kisha kukimbilia Ikulu kuapishwa?
 
Nianze kwa kumpongeza Mh Rais Samia kwa jinsi alivyoisuka Wizara ya mambo ya nje kwa mustakabali diplimasia ya taifa letu. Lakini Jana baada ya kutangaza uteuzi wao aliahidi kuwaapisha Leo saa 4 asubuhi vuwanja vya Ikulu.

Vyovyote itakavyokuwa ila Mimi Kuteuliwa Balozi Libarata Mulamula kwa hiyo Wizara Muhimu kwa nchi na ya Kimataifa nimefurahi mno kwani huyo ni Mtaalam na Mbobezi hapo kama ilivyo kwa Mchezaji ' Playmaker ' wa Simba SC Mzambia Clatous Chota Chama.
 
Mawaziri wanaapa kuanzia saa tisa mchana mkuu. Hiyo ratiba ya saa nne asubuhi sio sahihi.
Nadhani asubuhi kwenye kipindi cha bunge wataapa kuwa wabunge.
 
Huyu Mbarouk ni Mzenj?Naona mama kaongeza idadi ya wazenj kwenye baraza la mawaziri. Katibu mkuu kiongozi origin yake siyo Zenj kweli?
 
Ndio tatizo lenu Hilo
Kwani wazenji sio watanzania?
CS sio mzenji usiogope
 
Huyu Mbarouk ni Mzenj?Naona mama kaongeza idadi ya wazenj kwenye baraza la mawaziri. Katibu mkuu kiongozi origin yake siyo Zenj kweli?
Mama kaweka wazenji kwenye Wizara za Muungano ambayo ndio practice ya siku zote. Katanga ni Mbara, Amewahi kuwa Mhasibi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni nadhani, Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Mtendaji Mkuu wa Mahakama post aliyotumikia kabla ya kuwa Balozi.
 
Huyu Mbarouk ni Mzenj?Naona mama kaongeza idadi ya wazenj kwenye baraza la mawaziri. Katibu mkuu kiongozi origin yake siyo Zenj kweli?
Wazenj ni watu wema sana hasa ukute kafia dini na msomi hawanaga makuu ukiolewa au ukioa huko zenji hata muda wa kuishi unakuwa mrefu sijui kwann? Kama hujaolewa tafuta mwanaume wakizanzibar wenye hizo sifa uje huku uanzishe uzi wako wa hao watu.
 
Akiwa mzenji au bara we inakusaidia nin... Sisi tunaangalia ufanisi wake katk kazi na sio wawapi... Miaka hii 6 ya mwendazake dhambi ya ubaguzi ilikuwa kubwa sana... Sasa hivi MTU akipata tu nafasi wajinga lazma waulize wawapi mzenji au bara, kabila lake ni lipi!? Anatoka mkoa UPI!? Yani awamu ya mwendazake bora imeenda mana umoja wa kitaifa ulikuwa unakwenda kupotea kabisa.. Mambo ambayo Nyerere alikataza kuhubiri miaka 50 iliyopita na akayaona ya kijinga Leo hii karne ya 21 mtu anahoji ukabila...
 
Wazenj ni watu wema sana hasa ukute kafia dini na msomi hawanaga makuu ukiolewa au ukioa huko zenji hata muda wa kuishi unakuwa mrefu sijui kwann? Kama hujaolewa tafuta mwanaume wakizanzibar wenye hizo sifa uje huku uanzishe uzi wako wa hao watu.
Je kusukuma top....
 
Nianze kwa kumpongeza Mh Rais Samia kwa jinsi alivyoisuka Wizara ya mambo ya nje kwa mustakabali diplimasia ya taifa letu. Lakini Jana baada ya kutangaza uteuzi wao aliahidi kuwaapisha Leo saa 4 asubuhi vuwanja vya Ikulu.
Ninachoomba kujua, Je wataapa Uwaziri kabla ya kuwa Wabunge kamili? Au wataapishwa haraka haraka bungeni kisha kukimbilia Ikulu kuapishwa?
Wataenda bungeni kwanza
 
Vyovyote itakavyokuwa ila Mimi Kuteuliwa Balozi Libarata Mulamula kwa hiyo Wizara Muhimu kwa nchi na ya Kimataifa nimefurahi mno kwani huyo ni Mtaalam na Mbobezi hapo kama ilivyo kwa Mchezaji ' Playmaker ' wa Simba SC Mzambia Clatous Chota Chama.
ewaa!!!,namna ulivomaliza hapo mwishoni umenikosha sana....

Hata hivo nakubaliana nawe kwamba sasa tunaweza kurejesha mahusiano yetu na hadhi ya nchi yetu kimataifa
 
Back
Top Bottom