Je, Marekani ni adui wa ubinadamu?

Je, Marekani ni adui wa ubinadamu?

Haya maswali mie sikuyajibu na sijaona aliyejibu haya maswali yako,je unapoendelea kuzungumzia marekani nawe ungeeleza unazungumzia nini?
A complex behemoth that defies a simpletons categorization.
 
Tanzania ina uchumi gani na inaua watu wangapi kila siku?
Kwani Tanzania imewahi kuvamia nchi gani na kuua kwa kupiga mabomu mahospitalini, kuua watoto na wengi wasio na hatia kwa kisingizio cha regime change?
ukiachana na vita vya Kagera 1978 kupinga uvamizi wa Iddi Amin Dadaa ?
 
Nimekuuliza swali hujanijibu.

Na kwa nini niache vita vya Kagera?

Na kuua watu kwani lazima uvamie nchi na kupiga mabomu mahospitali kwa kisingizio cha regime change?
 
Tanzania ni adui wa ubinadamu kuliko Marekani.

Marekani serikali inakusanya kodi halafu mwananchi ukizidisha kulipa kodi, serikali inakurudishia kodi uliyoizidishia.

Jaribu kuomba kodi uliyoizidishia serikali Tanzania uone.

Marekani inathamini ubinadamu kuliko Tanzania. Ukiumwa Marekani ambulance inakuja mpaka mlangoni kwako, kabla hata hujalipa kitu.

Tanzania tunaambiwa ambulance mostly zinatumika kuhamisha wagonjwa kutoka hospitali moja kwenda nyingine tu.

Wakubwa wamenunua mashangingi mpaka aibu, lakini nchi haina ambulance za kutosha.

Marekani inathamini ubinadamu kuliko Tanzania.

Kila mji una zimamoto kufanya huduma za zimamoto ziwe karibu na wananchi.

Tanzania achilia mbali kutokuwepo zimamoto, nyumba zilivyojengwa sehemu nyingi hata zimamoto haifiki.

Na sehemu zinapofika zimamoto zinakwenda hazina maji.

Uwanja wa ndege wa Dar umeshushwa hadhi, moja ya sababu ni kukosa zimamoto ya uhakika.

Mmabo mengi sana ukiyaangalia kwa undani utaona nyie mnaosema Marekani ni adui wa ubinadamu ndio mnaokaa nchi yenye uadui na ubinadamu huko.

Viongozi wenu wanawaibia kila kitu, mnakosa elimu ya maana.

Mnabaki kulalamikia Marekani.

Na viongozi wenu wakiona hivyo wanafurahi sana. Kwa sababu wanahitaji ku channel hasira zenu sehemu ili wao waendelee kuwaibia.
 
Nimekuuliza swali hujanijibu.
Majibu utayapata kwenye majibu yako unayotakiwa utoe ya maswali hayo juu nilokuuliza.

Na kwa nini niache vita vya Kagera?
Sababu yule Nduli aliivamia Tanzania hivyo hakukuwa na namna tena zaidi ya kumchapa tu.
Tofauti na Marekani anavamia tu mataifa mengine na mara nyingine anavunja hata mikataba ya UN inayokataza taifa moja kuvamia taifa lingine.

Na kuua watu kwani lazima uvamie nchi na kupiga mabomu mahospitali kwa kisingizio cha regime change?
Siyo lazima iwe hivyo lakini unaeza kuua kwa makusudi au kwa kutokukusudia.
Marekani kule anakovamia anaua wengi wasio na hatia wakiwemo watoto wadogo mfano alifanya hivyo kule vietnam lakini hakufanikiwa kupata alichoikitaka zaidi ya kuua tu watu wengi kwa makusudi akarudia tena kwenye mataifa mengine mengi.
 
Unaposema "Marekani anakovamia" unamanisha nani huyo unayemsema "anakovamia" nani?

Ni muhimu kuwa precise. Marekani kuna taasisi ziko kuondoa roho za watu tu.

N akuna taasisi ziko kuokoa roho za watu.

Kuna mwanajeshi wa Marekani nilikuwa naongea naye, analalamika kwamba jeshi la Marekani lina sheria nyingi sana za kuhakikisha wanajeshi wanapigana vita kwa sheria.

Anasema wakitaka kuvamia sehemu nyingi na kufanyizia wanaweza kirahisi sana, tatizo jeshi linafuata sana sheria kiasi kwamba hata kupigana na ISIS inakuwa tabu.

Analaumu kwamba wanajeshi wanataka kufanyizia lakini sehemu nyingine mpaka wanatishiwa uhai, wanashindwa kujihami kwa kuangalia sana "rules of engagement".

Nenda Arabuni huko angalia ISIA wanavyochinja watu bila kitu cha msingi.

Halafu unakuja hapa unatuambia Marekani ji adui wa ubinadamu.

Uarabuni unaweza kuuawa kwa kuwa dini tofauti na Muislamu tu.

Marekani kuna uhuru wa kuabudu dini yoyote. Ni moja kati ya sababu watu walikimbia Ulaya kuja Marekani na mpaka leo wapenda uhuru tunaondoka nchi zenye majungu huko serikali inakwiba kuanzia kodi mpaka rambirambi.

Halafu Mmarekani anaibuka tu na kusema nitachukua watoto hawa nikawapeleke hospitali Marekani na wakipona nawapa scholarship.

Let that sink in.

Serikali imeiba mpaka rambirambi za wafu. Mmarekani kachukua watoto kawapeleka Marekani wakatibiwe. Na scholarship katoa juu.Mpaka chuo kikuu.

Halafu unaniambia Marekani ni adui wa ubinadamu?

Marekani ni pana kuliko kona moja unayoisema wewe.
 
USA wana tabia ya kung'ata na kupuliza. Ni waharibifu no. 1 WA amani ya dunia. Anayem-support USA ajitafakari Mara mbilimbili akili yake.
 
Lakini sijawahi kusikia marekani inamlazimisha mtu kutumia ARV.
zile kitu hulazimishwi,ukishapata ngoma tu wewe mwenyewe ktk kutapatapa kwako kusogeza siku za kuishi,unajikuta tu "automatikale" unaunga tela kwenda kugaiwa ARVs.
 
USA wana tabia ya kung'ata na kupuliza. Ni waharibifu no. 1 WA amani ya dunia. Anayem-support USA ajitafakari Mara mbilimbili akili yake.
Unaposema "USA" una maana gani? Nani?

Kuna Wamisionari wamekuta ajali imetokea tu huko Arusha. Hawakuwa na sababu ya kusimama na kusaidia.

Tena walikuwa na sababu kibao za kukimbia bila kusaidia.

Wageni. Hawajui sheria za nchi. Hawajui tamaduni etc.

Hawakukubali kukimbia bila kutoa msaada.

Hawakuishia kutoa msaada hapo tu.

Watoto wengine wamechukuliwa na kupelekwa Marekani kwa matibabu.

Hawajaishia hapo.

Wametoa scholarship mpaka Chuo Kikuu.

Hawa si Wamarekani?

Mnaweza kutueleza mnaposema "Marekani hivi" au "USA vile" mnqchomaanisha ni nini?

Nashindwa kuwaelewa mnapolundika nchi nzima yenye watu zaidi ya milioni 320 kama vile ni nyumba ya mtu mmoja.

Hata hiyo nyumba ya mtu mmoja unaweza kuwa na watoto wengi wenye tabia tofauti.
 
Maarabu yalisema yanapambana na Marekani pamoja na wanaomsaidia marekani kuwaonea na kuwanyanyasa waarabu.
 
Una hakika sijaelezea au hujasoma / hujaelewa tu?
Hujaeleza,unachofanya ni kueleza mambo kibao yasiyo na msingi mfano unaeleza kuna bara linaitwa marekani ndiyo nini sasa? suala hilo lilikuwa linahusiana nini na wakati nilishakwambia hapa tunazungumzia marekani kama nchi.

Au ndiyo katika harakati zako kujionesha unajua vitu vingi?
 
A complex behemoth that defies a simpletons categorization.
Ungetumia muda huo kueleza tu ni marekani gani ambayo unaizungumzia humu maana nakumbuka ulisema bila hivyo huu mjadala utakuwa hauna maana.
 
Tanzania ni adui wa ubinadamu kuliko Marekani.

Marekani serikali inakusanya kodi halafu mwananchi ukizidisha kulipa kodi, serikali inakurudishia kodi uliyoizidishia.

Jaribu kuomba kodi uliyoizidishia serikali Tanzania uone.

Marekani inathamini ubinadamu kuliko Tanzania. Ukiumwa Marekani ambulance inakuja mpaka mlangoni kwako, kabla hata hujalipa kitu.

Tanzania tunaambiwa ambulance mostly zinatumika kuhamisha wagonjwa kutoka hospitali moja kwenda nyingine tu.

Wakubwa wamenunua mashangingi mpaka aibu, lakini nchi haina ambulance za kutosha.

Marekani inathamini ubinadamu kuliko Tanzania.

Kila mji una zimamoto kufanya huduma za zimamoto ziwe karibu na wananchi.

Tanzania achilia mbali kutokuwepo zimamoto, nyumba zilivyojengwa sehemu nyingi hata zimamoto haifiki.

Na sehemu zinapofika zimamoto zinakwenda hazina maji.

Uwanja wa ndege wa Dar umeshushwa hadhi, moja ya sababu ni kukosa zimamoto ya uhakika.

Mmabo mengi sana ukiyaangalia kwa undani utaona nyie mnaosema Marekani ni adui wa ubinadamu ndio mnaokaa nchi yenye uadui na ubinadamu huko.

Viongozi wenu wanawaibia kila kitu, mnakosa elimu ya maana.

Mnabaki kulalamikia Marekani.

Na viongozi wenu wakiona hivyo wanafurahi sana. Kwa sababu wanahitaji ku channel hasira zenu sehemu ili wao waendelee kuwaibia.
"Tanzania ni adui wa ubinadamu kuliko marekani"

Sasa umekubali kuwa marekani ni adui ila unasema uadui wa Tanzania ni mkubwa kuliko marekani.
 
Hujaeleza,unachofanya ni kueleza mambo kibao yasiyo na msingi mfano unaeleza kuna bara linaitwa marekani ndiyo nini sasa? suala hilo lilikuwa linahusiana nini na wakati nilishakwambia hapa tunazungumzia marekani kama nchi.

Au ndiyo katika harakati zako kujionesha unajua vitu vingi?
Hujajibu Marekani ni nini.

Ungejibu ungemaliza habari zote hizo nyingine.
 
Unaposema "Marekani anakovamia" unamanisha nani huyo unayemsema "anakovamia" nani?

Ni muhimu kuwa precise. Marekani kuna taasisi ziko kuondoa roho za watu tu.

N akuna taasisi ziko kuokoa roho za watu.

Kuna mwanajeshi wa Marekani nilikuwa naongea naye, analalamika kwamba jeshi la Marekani lina sheria nyingi sana za kuhakikisha wanajeshi wanapigana vita kwa sheria.

Anasema wakitaka kuvamia sehemu nyingi na kufanyizia wanaweza kirahisi sana, tatizo jeshi linafuata sana sheria kiasi kwamba hata kupigana na ISIS inakuwa tabu.

Analaumu kwamba wanajeshi wanataka kufanyizia lakini sehemu nyingine mpaka wanatishiwa uhai, wanashindwa kujihami kwa kuangalia sana "rules of engagement".

Nenda Arabuni huko angalia ISIA wanavyochinja watu bila kitu cha msingi.

Halafu unakuja hapa unatuambia Marekani ji adui wa ubinadamu.

Uarabuni unaweza kuuawa kwa kuwa dini tofauti na Muislamu tu.

Marekani kuna uhuru wa kuabudu dini yoyote. Ni moja kati ya sababu watu walikimbia Ulaya kuja Marekani na mpaka leo wapenda uhuru tunaondoka nchi zenye majungu huko serikali inakwiba kuanzia kodi mpaka rambirambi.

Halafu Mmarekani anaibuka tu na kusema nitachukua watoto hawa nikawapeleke hospitali Marekani na wakipona nawapa scholarship.

Let that sink in.

Serikali imeiba mpaka rambirambi za wafu. Mmarekani kachukua watoto kawapeleka Marekani wakatibiwe. Na scholarship katoa juu.Mpaka chuo kikuu.

Halafu unaniambia Marekani ni adui wa ubinadamu?

Marekani ni pana kuliko kona moja unayoisema wewe.
Na kwa upana huo wa marekani ndiyo maana hujaeleza hata yale matukio ya wazi tu ambayo dunia nzima tuliyaona ya wamarekani weusi kupigwa shaba,achilia mbali matukio mengine ambayo yanayowakuta hao wamarekani weusi ambayo hayatangazwi.

Pengine marekani kubwa.
 
"Tanzania ni adui wa ubinadamu kuliko marekani"

Sasa umekubali kuwa marekani ni adui ila unasema uadui wa Tanzania ni mkubwa kuliko marekani.
Hapana.

Wewe ndiye hujui hesabu. Hujui mantiki. Hujui lugha. Hujui maana ya neno kuliko.

Mtu akisema "Tanzania ni adui wa ubinadamu kuliko Marekani" hilo halimaanishi Marekani inahitaji kuwa na uadui wa binadamu wa aina yoyote.

Nikisema "Mama Juma ana sukari jikoni kwake kuliko Mama Hamisi" haina maana Mama Hamisi ana sukari yoyote. Inawezekana mama Hamisi hana sukari kabisa na Mama Juma ana kilo moja ya sukari.

Nitaweza kusema Mama Juma ana sukari kuliko Mama Hamisi.

Hujui hesabu. Hujui lugha. Hujui mantiki.

Ndiyo maana unabwabwaja "Marekani hivi, Marekani vile".

Ukiulizwa Marekani ni nini? Hujui. Huwezi kujibu.
 
Ungetumia muda huo kueleza tu ni marekani gani ambayo unaizungumzia humu maana nakumbuka ulisema bila hivyo huu mjadala utakuwa hauna maana.
Tatizo hujui kusoma.

Nieleze mara ngapi?
 
Unaposema "USA" una maana gani? Nani?

Kuna Wamisionari wamekuta ajali imetokea tu huko Arusha. Hawakuwa na sababu ya kusimama na kusaidia.

Tena walikuwa na sababu kibao za kukimbia bila kusaidia.

Wageni. Hawajui sheria za nchi. Hawajui tamaduni etc.

Hawakukubali kukimbia bila kutoa msaada.

Hawakuishia kutoa msaada hapo tu.

Watoto wengine wamechukuliwa na kupelekwa Marekani kwa matibabu.

Hawajaishia hapo.

Wametoa scholarship mpaka Chuo Kikuu.

Hawa si Wamarekani?

Mnaweza kutueleza mnaposema "Marekani hivi" au "USA vile" mnqchomaanisha ni nini?

Nashindwa kuwaelewa mnapolundika nchi nzima yenye watu zaidi ya milioni 320 kama vile ni nyumba ya mtu mmoja.

Hata hiyo nyumba ya mtu mmoja unaweza kuwa na watoto wengi wenye tabia tofauti.
Yale Yale niliyosema.

Watu wakieleza mabaya ya marekani ndiyo unaleta story hizo ila wewe ukiizungumzia marekani kwa mazuri unaizungumzia kama kitu kimoja.
 
Back
Top Bottom