Je, makampuni ya simu yamepunguza Mb/sec?

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
12,902
15,330
Naomba anayefahamu atueleze, kuna kitu gani kinachoendelea katika hii mitandao ya simu kwa sababu inaonekana ni wizi wa dhahiri kabisa.

Kwa mfano, kwa sasa ukinunua GB moja ambayo ni sawa na MB 1,000 na kama hutumii kwa kupakua ila kwa ku-browse tu pale ambapo ulikuwa ukitumia kwa takriban siku 5 sasa utatumia kwa siku moja na nusu tu na sio zaidi ya hapo na huu mchezo umeanza kama siku mbili tu zilizopita!

Je, haya makampuni hasa Airtel na Vodacom ambazo ndizo ninazitumia zaidi wanaweza wakatueleza kuna nini hapa kabla hatujafuatilia TCRA?

Maanake ni wazi kabisa kwamba huu ni wizi wa wazi kabisa.
 
Waziri mwenyewe ni Nape. Unategemea nini? Kilaza aliefail hata masomo ya sciences ndio anaongoza wizara inayohusika na teknolojia.

Wewe post tu kama taarifa hakuna chochote kitakacho shughulikiwa.. kila mtu anakula kwa kamba yake

Wizara kama hizi wangepewa watu wenye maono ya mbali kama maxence melo nadhani tungepiga hatua, tatizo ni wizara zinazoihusisha siasa moja kwa moja katika teuzi
 
Aiseeeh ni Majizi kweli kweli ama watuambie wamepata idhini ya kutukamua kimya kimya.

Imagine mtu hupakui chochote wala kuangalia online videos lakini ndani ya muda mfupi tu mb zako zimeisha.
Nimekata tamaa ya kutumia internet kwakweli.
 
Sasa hivi tuko 4G na 5G, wewe bado uko 3G, spidi ni kubwa na bando inalika hivyohivyo.

Halafu, huku ndio kuna mapato ya kodi, si mmelimbia mashamba ya kahawa, pamba, na katani mmehamia kwenye mitandao, serikali ipo mlipo.

Ukitumia muda mwingi kumuangalia mwijaku, lazima tozo iwe kubwa, unaangalia wema sepetu anajibinua, tozo
 
Imebidi ni 😂😂😂 japokuwa hakuna uhalisia wa kile umeandika na anayetafuta jibu la wizi wa mb
 
Nilifikiri labda ni mimi tu pekee yangu ndio simu yangu inakula MB kwa kunikomoa. Maana unakuta wakati mwingine najibana sanaa ili nisifungue hata video lakini unakuta nikienda kuangalia salio la MB nabaki nashangaa tu nakubaki nawaza tu namna ya kununua tena MB.

Ila mimi kwa upande wangu ambapo nimekuwa mtumiaji wa mtandao wa VODACOM katika shida na raha nimebaini ya kuwa kwa sasa kasi ya mtandao wa VODACOM upande wa internet ni mzuri sana tena sana tena sana tena sana .yaani popote napokuwa nikiwasha tu data nakuta unafanya kazi vizuri sana na kufungua na kusoma kila kitu nachotaka.

Kuna maeneo nilikuwa nikiwa mtandao wa intaneti ulikuwa unasumbua sana na speed ilikuwa ndogo sana .lakini kwa sasa speed ya internet Ni kubwa sana na ya kasi sanaa .kwa hiyo ubora wa mtandao wa VODACOM umeongezeka sana na wala sina deni nao hata kidogo.

Mimi naona ni bora hata kama MB zinakwisha haraka lakini kasi ya internet ikawa kama ilivyo sasa ni jambo jema sana kuliko unakuwa na ni MB mingi halafu hakuna unachofanya chochote kile. kutokana na mwendo wa kobe wa mtandao.

VODACOM endeleeni na ubora wenu huo huo wa mtandao na mimi Mwashambwa Nitaendelea kuwa mteja wenu mwaminifu na mtiifu wa wakati wote na nitawateteeni mitaani nitakapoona mtu analalamika juu ya hilo la kuisha haraka kwa MB kwa kuwa nimejionea kasi ya mtandao ilivyo bora na nzuri sana kwa sasa.ambapo najuwa ni lazima MB ziishe haraka.

Tupeni kasi hii hii nzuri ya internet mliyotupatia kwa sasa maana inaleta furaha katika kutumia simu na laini yenu. Ni bora MB ziishe haraka kuliko mtandao na kasi ya internet ikawa mwendo wa kobe.
 
Voda wanakunywa bundle sana. Sema na speed inachangia
Hakuna wizi wa MB ila utafiti niliofanya nimegundua ni kwa kuwa kwa speed imeongezeka sana ya internet ambapo inafanya kazi vizuri sanaa hata yale maeneo ambayo awali mtandao ulikuwa unasumbua sana ukitaka hata kuingia JF au kufanya chochote kile mtandaoni. Kwa hiyo mimi kwa upande wangu ni bora tuwe na kasi hii ya sasa hata kama MB zinakwisha haraka kuliko kuwa na na MB mengi halafu muda wote unahangaika na mtandao mpaka hasira zinakushika.

VODACOM wapewe pongezi kwa maboresho makubwa waliyoyafanya ambayo kwa sasa kiukweli huduma zao zimekuwa nzuri sana.
 
Aiseeeh ni Majizi kweli kweli ama watuambie wamepata idhini ya kutukamua kimya kimya.
Imagine mtu hupakui chochote wala kuangalia online videos lakini ndani ya muda mfupi tu mb zako zimeisha.
Nimekata tamaa ya kutumia internet kwakweli.
Hapana na hakuna wizi wa aina yoyote ile. jaribu kufanya utafiti utagundua kuwa speed imeongezeka sana ya mtandao kwa sasa. Mfano mimi ambaye ni mtumiaji wa VODACOM kuna maeneo ambayo nilikuwa nahangaika sana juu ya kasi ndogo ya mtandao lakini siku hizi speed Ni kubwa nikiwa mahali popote pale hadi mashambani Vodacom inachapa kazi kwa kwenda mbele .hata kuwe na mvua au baridi au jua kali au vumbi Vodacom ni kazi kazi tu.hata uwe mlimani au mteremkoni au vichakani au mbugani Vodacom inakasi ileile kukupa raha ya kufurahi unachotaka kukipata mtandaoni
 
Vodacom wako vizuri sana hujakosea wapewe maua yao tu.
 
Hili jambo litakuwa na ukweli kwa 100%!! Yaani siku hizi ukijiunga kifurushi cha wiki, ndani ya siku 2 tu kwisha!!! Haya makampuni ya simu yanatuumiza sana aisee.
 
Hakuna wizi wa MB ila utafiti niliofanya nimegundua ni kwa kuwa kwa speed imeongezeka sana ya internet ambapo inafanya kazi vizuri sanaa hata yale maeneo ambayo awali mtandao ulikuwa unasumbua sana ukitaka hata kuingia JF au kufanya chochote kile mtandaoni. Kwa hiyo mimi kwa upande wangu ni bora tuwe na kasi hii ya sasa hata kama MB zinakwisha haraka kuliko kuwa na na MB mengi halafu muda wote unahangaika na mtandao mpaka hasira zinakushika.

VODACOM wapewe pongezi kwa maboresho makubwa waliyoyafanya ambayo kwa sasa kiukweli huduma zao zimekuwa nzuri sana.
Hivi unaweza kukuta hivyo vifurishi vyenyewe unaungwa juu kwa juu tu na akina Tulia, ili uje uwasifie humu jukwaani!
 
Hapana na hakuna wizi wa aina yoyote ile. jaribu kufanya utafiti utagundua kuwa speed imeongezeka sana ya mtandao kwa sasa. Mfano mimi ambaye ni mtumiaji wa VODACOM kuna maeneo ambayo nilikuwa nahangaika sana juu ya kasi ndogo ya mtandao lakini siku hizi speed Ni kubwa nikiwa mahali popote pale hadi mashambani Vodacom inachapa kazi kwa kwenda mbele .hata kuwe na mvua au baridi au jua kali au vumbi Vodacom ni kazi kazi tu.hata uwe mlimani au mteremkoni au vichakani au mbugani Vodacom inakasi ileile kukupa raha ya kufurahi unachotaka kukipata mtandaoni
Wewe umekua wakala wao!? Unatumia nguvu nyingi sana kuwa_prove wrong wanaolalamika. Sijui unafaidika vipi!?
 
Speed inachangia sana kutumika kwa bando
Maeneo mengi kwa sasa tayari Kuna 5g kwahiyo simu yako kama Ina uwezo wa 5g punguza weka 4g Speed itapungua na bundle halitoenda sana
 
Tena wewe chawa ilitakiwa ukatwe mb nyingi maana huna akili kazi kusifia sifia
Asali hulambi na huwez pata teuz kunguni wewe
 
Back
Top Bottom