Je, mahali panapoitwa Ngende ni pakusadikika?

Je, mahali panapoitwa Ngende ni pakusadikika?

Kubbra Hooda

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
208
Reaction score
297
Habarini wanajukwaa kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu nimekuwa nikisikia simulizi mabalimbali za kusisimua kuhusu mahali panapoitwa NGENDE(Maeneo ya Kusini)

Simulizi ambazo zimejikita katika mambo ya giza.. Ningependa kujua zaidi je ni kweli sehemu hiyo ipo au ni hadithi za kusadikika?

Je kuna ambao wamewahi kufika? Je mahali hapo kuna makaz ya watu nk kwa yeyote anayefahamu chochote kuhusu mahali hapo basi anaweza kuchangia.

Ahsanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio, hiyo sehemu ipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio, hiyo sehemu ipo, na ipo ktk Kijiji kiitwacho Mkwera ktk Mkoa wa Lindi ni mpakani mwa Mtwara na Lindi, kwa wale wanaoifahamu Nyangao basi ukitoka hapo unapta vjj km viwili au kimoja. NA HAYO MAMBO YAPO SANA TANGIA MIAKA MINGI, NA UKIKIUKA MASHARTI USISHANGAE WW MWENYEWENA EITHER FAMILY AKO MKAPOTEZA MAISHA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu hiyo ipo kweli inapatikana wilaya ya Liwale nkoa wa Lindi katikati ya msitu wa Selous,moja ya wataalam wahudumu katika kilinge hicho ni ukoo niliozaliwa Mimi so mababu zangu walihudumia Ngende miaka mingi tu,ila kwa sasa kilinge kimepungua nguvu,pale unapewa utajiri kwa sharti la kurudisha shukrani ukijifanya kusahau unatumiwa mnyama yoyote yule anakuja kukudhuru,pale ngende ukienda unapokelewa na nyani na wanyama wengine nao wanazungumza karibia lugha zote duniani

Karibu Ngende kwa Wamagingo au Wangindo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu hiyo ipo kweli inapatikana wilaya ya Liwale nkoa wa Lindi katikati ya msitu wa Selous,moja ya wataalam wahudumu katika kilinge hicho ni ukoo niliozaliwa Mimi so mababu zangu walihudumia Ngende miaka mingi tu,ila kwa sasa kilinge kimepungua nguvu,pale unapewa utajiri kwa sharti la kurudisha shukrani ukijifanya kusahau unatumiwa mnyama yoyote yule anakuja kukudhuru,pale ngende ukienda unapokelewa na nyani na wanyama wengine nao wanazungumza karibia lugha zote duniani

Karibu Ngende kwa Wamagingo au Wangindo

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuuuh hatari hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ipo wilaya ya Liwale mkoa wa Lindi, kuna mjomba angu mmoja alinisimulia aliwahi kwenda kwa shida zake sasa ikawa njianj akikutana na watu wakumuuliza unaenda wapi? Anajibu "tunaenda kusikiliza uongo wao kwa hawa jamaa"(anamaanisha huko Ngende kwa waganga yaani ni waongo hawaamini ila anakwenda kujaribu) Sasa alipofika akaulizwa umekuja kufanya nini huku na wakati sisi ni waongo? Ikabidi awe mpole na kuomba radhi akaambiwa usiniombe mimi kamuombe yule pale anaoneshwa chatu mmoja mkubwa sana kama Anaconda akawekewa unga kiganjani akamlambishe ndio msamaha. Sasa Anko akifikiria maneno aliyoyasema njiani na huyo jamaa wakuombwa radhi jinsi alivyo ule unga wa kiganjani atashiba kweli au ndio atakuwa yeye mwenyewe ni msosi?.

Ila ni sehemu maarufu kwa kusini inasadikia kwa kutoa utajiri na mambo mengine mengi ya kishirikina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngende ni maeneo karibu na sehemu inaitwa Nanjilinji na ni kweli kuna tamaduni za kishirikina sana hivyo kuna waganga wengi sana, na wengi hawataki pesa nyinyi zaidi ya sumni au shilingi kumi mpaka hamsini ya coin

Kwa hiyo Kazi kwako haina tofauti na Gamboshi

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu nimesikia unaweza kwenda huko ukatibiwa na mnyama kama simba yani mauza uza ila naskia watu wengi wanaenda huko na kunaoenda hawarudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom