Je, Mahakama imekwepa wajibu wake kikatiba katika hukumu ya kesi ya Tundu Lissu?

Tulimsisikia Jaji Matupa wa mahakama kuu akitupilia mbali maombi ya kesi ya Tundu Lissu ya kutaka kurejeshewa ubunge wake, ambao alikuwa akidai kuwa amevuliwa kinyume cha sheria

Katika Shauri hilo Mbunge Tundu Lissu alimtaka Spika Ndugai aithibitishie mahakama hiyo kwa kauli aliyoitoa Bungeni kuwa yeye Spika hajui alipo Mbunge Tundu Lissu.

Hivi katika mazingira ya kumiminiwa risasi 38 katika gari lake na 16 ya risasi hizo kumwingia mwilini na hadi hivi sasa yupo hospitalini Ubelgiji ambako anapata matibabu huku Dunia nzima ikifahamu hivyo, iweje Leo Spika Ndugai adai kuwa hajui alipo Mbunge wake Tundu Lissu??

Katika hukumu hiyo Jaji Matupa alieleza kuwa kuendelea na kesi hiyo na hatimaye kuamua kumvua ubunge Mtaturu, itakuwa ni kuleta mgogoro wa kikatiba kwa kuwa tayari Mbunge Mtaturu ameshaapishwa kwa hivyo kutakuwa na wabunge wawili!

Hebu tumuulize huyo Jaji Matupa, si ndiyo yeye alipokuwa akiisikiliza kesi hiyo katika hatua ya awali alipokuwa akijibu maombi ya upande mashitaka walipotaka Mbunge Mtaturu asiapishwe kwanza kabla kesi ya msingi kuanza kusikilizwa, alijibu kuwa hiyo si hoja ya msingi kwa kuwa kuapishwa kwa Mbunge hakuizuii mahakama yake kuweza kumvua ubunge wake, ili mradi tu ithibitike kuwa kaupata ubunge huo pasipo halali??

Ndipo hapo ninapojiuliza iweje Jaji Matupa atoe kauli mbili zinazikinzana katika kesi hiyo moja??

Turudi kwenye mfumo wa uongozi bora, tunatambua wazi kuwa katika nchi yoyote iliyo na uongozi bora ni lazima iwe na "separation of power" katika mihimili mitatu ya uongozi ambayo ni Mahakama, Bunge na Serikali, katika kile kinachoitwa "check and balance" katika mihimili hiyo mitatu

Kila mhimili umepewa wajibu wake kikatiba, ambapo mhimili wa mahakama ndiyo umepewa wajibu wa kutafsiri sheria ili yule anayeona ameonewa basi atalipeleka Shauri lake huko ili lipate kuamriwa.

Hivi katika mazingira kama ya kesi ya Tundu Lissu Vs Spika wa Bunge, kwa serikali kuweka mawakili 15 dhidi ya 4 wa Tundu Lissu, kwa ajili tu ya kuweka tu mapingamizi ili kesi hiyo isianze kuisikilizwa, hatuoni kama serikali hii iliwekeza nguvu kubwa mno kwa kesi hiyo??

Inawezekanaje kwa serikali kuweka mawakili wengi kiasi hicho kwa kesi ambayo "haiwahusu" ambayo mshitakiwa ni Spika wa Bunge, ambao ni mhimili mwingine unaojitegemea, ambapo nao una mawakili wake??

Hivi katika mazingira haya wananchi tukimbilie wapi, iwapo chombo chetu cha mahakama, klichopewa wajibu kikatiba, kinakwepa wajibu wake??

Hivi sasa ndipo ninapoelewa kwa Rais Magufuli alipotamka huko nyuma, kuwa mhimili wake yeye ambao ni serikali kuwa ndiyo "supreme" kwa kuwa ndiyo umejichimbia zaidi chini!

Unaifahamu orodha nzima ya defendants kwenye hiyo kesi?
 
Yes but was not official kwa mwajiri boss. ..
Walizuia malipo yake kwa ajiri hiyo na tukampigania alipwe ndipo akalipwa.
Kwa sharti kwamba lete official info (Hospital & Doctors report) kwa mwajiri bunge.
He didnt do that.... wakapiga mtama...
Tunachosema ni kuwa Spika Ndugai alikuwa akijua alipo Tundu Lissu.......

Kama alikuwa hajui alipo, aliwezaje kumlipa mshahara kwa kipindi chote kinachokaribia miaka miwili kama alikuwa hajui alipo??
 
Tunachosema ni kuwa Spika Ndugai alikuwa akijua alipo Tundu Lissu.......

Kama alikuwa hajui alipo, aliwezaje kumlipa mshahara kwa kipindi chote kinachokaribia miaka miwili kama alikuwa hajui alipo??
Kwa maneno mengine ni kuwa; Ndungai kakiri kuwa yeye ni mzembe wa kukubuhu hata anastahili kutumbuliwa kwa kumlipa mshahara mtoro kazini.
 
Mleta hoja unayasahau yale maneno ya mwenye nchi kuwa, " siwezi kukulipa mshahara mnono, gari, nyumba na posho lukuki kisha utoe ushindi kwa wapinzani!"
Maneno haya yataishi hadi amalize ngwe yake! Na yataendelea kusimama kwa wateule wake wote hivyo usimshangae sana jaji kwani naye ni mteule!
Kizazi kipya cha "majaji" kimezaliwa.Tutashuhudia mengi na ya kukarahisha baada ya uchaguzi 2020!
 
Kizazi kipya cha "majaji" kimezaliwa.Tutashuhudia mengi na ya kukarahisha baada ya uchaguzi 2020!
Hakika huko tuendako kuna Giza nene sana.....

Hizi ni rasharasha tu.......

Kazi yenyewe itaanza katika kipindi cha pili cha Jiwe, cha baada ya 2020, ambacho tutashuhudua mambo ya hatari sana!
 
Katiba mpya n muhimu ili kutenganisha mihimili ya utawala wa nchi!!
Sio sawa wakuu wa mihimili wawe chini ya ubabe wa mtawala mkuu.
Mkombozi wa nchi yetu ni katiba mpya bora ya kidemokrasia.
 
Katiba mpya n muhimu ili kutenganisha mihimili ya utawala wa nchi!!
Sio sawa wakuu wa mihimili wawe chini ya ubabe wa mtawala mkuu.
Mkombozi wa nchi yetu ni katiba mpya bora ya kidemokrasia.
Ni kweli kwa kiasi fulani..........

Lakini hata Katiba hii ya sasa, pamoja na mapungufu yake, lakini jambo baya zaidi ni namna Jiwe anavyoamua kuisigina
 
Back
Top Bottom