Je, maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au vitu? Wachumi tusaidieni, uchumi wa Awamu ya 5, unalisaidia Taifa au utaliangamiza?

Tatizo ni moja tu ambalo ndio litatukwamisha kufukia maendeleo ya watu nalo ni uwekezaji mkubwa sana kwenye maeneo ambayo hayawagusi watu walio wengi kwa maana ni watanzania wachache sana wanaojishughulisha na sekta ya ujenzi ambako ndio kila siku billions of money zinaelekezwa huko na hivyo kufaidisha watu wachache ingawa lengo kufanya hivyo inaweza kuwa ni kuchochea ukuaji wa haraka wa biashara lakini bado ni kwa watu wachache na itachukua muda mrefu pia kuleta matokeo chanya kwa uchumi

Watanzania wengi wanajishughulisha na kilimo uwekezaji huu unaofanywa sasa hivi kama ungeelekezwa huko hasa kwenye mazao ya kibiashara hata chakula pia maana tumezungukwa na nchi jirani zinazokumbwa na tatizo la njaa kwa kiasi kikubwa watu wengi sana wangefaidika na hata Tanzania ya viwanda ingekuwa ya uhakika maana sekta ya kilimo na viwanda ni sekta zinazotegemeana sana na ndizo sekta zinazoweza kuajiri watu wengi kwa wakati mmoja kuliko sekta nyingine na hayo maendeleo ya watu yanaweza kufikika
 
Maendeleo ni Uhuru
Hatua zozote zifanywazo na mwanadamu lazima zilenge kumuweka huru, kama hatua hizo hazimuweki mtu huru dhidi ya umasikini, Ujinga, Maradhi na Kutawaliwa kimabavu basi hatua hizo hazina maana
 
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali, ambalo linatakiwa kujibiwa na wachumi wetu, Mwalimu Nyerere alituhusia "Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu na Sio Maendeleo ya Vitu". Wachumi wetu tusaidieni kutuelimisha, huu Uchumi wa Magufuli, Unalisaidia Taifa Kupata Maendeleo ya Watu, au Utatupatia Maendeleo ya Vitu Huku Uchumi wa Mtu Mmoja Mmoja Ukiangamia?.

Kama kawaida yetu kutumia the right to expression kuuliza, Jee awamu hii ya 5 ya rais Magufuli, inatumia falsafa gani ya kiuchumi?, jee uchumi huu wa Magufuli, unalisaidia taifa au unaliangamiza?. Kwa vile mimi sio mchumi, wachumi wetu, tusaidieni, tuelimisheni tunakwenda wapi?, are we heading to the right direction?.

Ili Tuendelee Tunahita Vitu Vinne, Vyote Tunavyo, Tumekwama Wapi?
Tulifunzwa, ili tuendelee tunahitaji vitu vinne,
  1. Watu-tunao
  2. Ardhi- tunayo
  3. Siasa Safi- tunayo?
  4. Uongozi bora-?
Kama vitu hivi vyote vinne tunavyo, sasa sisi Tanzania tumekosa nini?, kwa nini bado ni masikini?.

Kupanga ni kuchagua.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea.
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...
Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed ...
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza ...

Ni swala la yai na kuku, bila ya vitu kwa vitu nafikiri ulimaanisha Miundo mbinu kama Reli, barabara, Umeme, n.k. hakuna maendeleo ya watu, na ukianza na watu bila ya Miundo mbinu hkn mahali utaenda, hivyo kwangu Raisi Magufuli yuko sawa isitoshe hawezi kuleta maendeleo ya kila mtu ndani ya miaka 5-10 tu, hivyo kama akituacha na fast train Dar-TBR-MZ/KGM, Umeme wa zaidi ya 5000 MW, kupunguza foleni Dar, wengine watakakuja sasa wanaweza hata kuwa chadema watawekeza kwa maendeleo watu lkn yeye hawezi kufanya yote!
 
You have said it well..
 
Huwezi kuwa na maendeleo ya WATU bila kuwa na maendeleo ya VITU. Na huwezi kuwa na maendeleo ya VITU bila maendeleo ya WATU. It is that simple.
 
huyu mshamba wetu kuna tatizo mahali
mimi naamini kuwa ukiendeleza watu ni rahisi sana vitu kuendelea.
ukiendeleza vitu ni ngumu sana kwa watu kuendelea
watu wakiwa na hela watajenga ila majengo bila watu kuwa na hela ni sawa na kazi bure
Mahaba kwako mkuu...neno lako la mwisho naomba niliboreshe hivi: NCHI YENYE BARABARA ZA LAMI NA FLYOVERS ILHAHI WATU WANATAABIKA KIUCHUMI NI SAWA NA MAKABURI YALIYOPAMBWA NA ALMASI. Yana manufaa gani mapambo kwa marehemu? Fahari ya marehemu au mtunza makaburi?

Ethiopia ni mfano mzuri. Si yasifiwa kwa madaraja na reli, lakini ndio wanakotoka wahamiaji haramu...wanaondokea nini nchini mwao ikiwa mambo ni safi? Na haya mambo hayaji hivi hivi, utazame uongozi wa Ethiopia, shida ipo. Wanahama kwa kuwa utu wao umepimwa vs maghorofa.

Pascal Mayalla , waambie 'wateule wa mungu' kwamba, Mungu ametupa nafasi moja tu ya kuishi duniani (potelea mbali hata kama dunia yenyewe 'sio yake') basi watuache tuishi (badala ya kudumu) maana if we live well, once is enough. Tusitamanishwe kuifikia Ethiopia maana baadaye tutaitwa WAHAMIAJI HARAMU ambao Baba Yao anamiliki Sheba Miles lakini wanasafiri ndani ya Fuso na kupoteza maisha...YaRabbi tupe moyo wa ustahimilivu au mshana jr anisaidie kugeuka msukule nisijisikie vibaya kukaa 'makaburini'.
 
Ukitaka kujua namna watanzania wengi ni zero brains soma huu uzi.

Wengi wanamshambulia Magufuli kwa ujenzi wa miundombinu nafarijika kwa hili sababu muda mwingine mpumbavu anaongea point ila muerevu tu ndio atazing'amua

Nyie wapumbavu mnaona miundombinu sio chochote sababu akili zenu ni finyu kwenye kuchambua mambo lakini mwerevu hilo ndio la msingi kwenye maendeleo.

Naona msimuhusishe Baba wa taifa kwenye huu upuuzi wenu sababu TAZARA, viwanda, ndege za ATCL, Bandari na miundombinu mingi yeye ndio muasisi na wengine hapo katikati waliyavurunda hayo yote lakini JPM anavirejesha vile vya Baba wa taifa hivyo tafuteni chaka lingine la kujadili huu upuuzi lakini sio Nyerere
 
Kitu gani kimempoteza Ben Saanane? Labda kuhoji sana kemistri ya baba J? Au alikuwa na bifu zake zingine?
NB: 1. Hata wanasayansi kama akina Pepsin wasingefanya anayofanya.
2. Mtu mwenyewe haeleweki,analosema leo atalipinga kesho na la kesho atalipinga keshokutwa. Huyu utamfanyiaje tathmini?
 
Ukitaka kujua namna watanzania wengi ni zero brains soma huu uzi.

Wengi wanamshambulia Magufuli kwa ujenzi wa miundombinu nafarijika kwa hili sababu muda mwingine mpumbavu anaongea point ila muerevu tu ndio atazing'amua

Nyie wapumbavu mnaona miundombinu sio chochote sababu akili zenu ni finyu kwenye kuchambua mambo lakini mwerevu hilo ndio la msingi kwenye maendeleo.

Naona msimuhusishe Baba wa taifa kwenye huu upuuzi wenu sababu TAZARA, viwanda, ndege za ATCL, Bandari na miundombinu mingi yeye ndio muasisi na wengine hapo katikati waliyavurunda hayo yote lakini JPM anavirejesha vile vya Baba wa taifa hivyo tafuteni chaka lingine la kujadili huu upuuzi lakini sio Nyerere
Soma hoja ya Mwana mtoka Pabaya hapo juu. Kama unazo utaelewa ila kama hamna,basi tena!
 
Mahaba kwako mkuu...neno lako la mwisho naomba niliboreshe hivi: NCHI YENYE BARABARA ZA LAMI NA FLYOVERS ILHAHI WATU WANATAABIKA KIUCHUMI NI SAWA NA MAKABURI YALIYOPAMBWA NA ALMASI. Yana manufaa gani mapambo kwa marehemu? Fahari ya marehemu au mtunza makaburi?

Ethiopia ni mfano mzuri. Si yasifiwa kwa madaraja na reli, lakini ndio wanakotoka wahamiaji haramu...wanaondokea nini nchini mwao ikiwa mambo ni safi? Na haya mambo hayaji hivi hivi, utazame uongozi wa Ethiopia, shida ipo. Wanahama kwa kuwa utu wao umepimwa vs maghorofa.

Pascal Mayalla , waambie 'wateule wa mungu' kwamba, Mungu ametupa nafasi moja tu ya kuishi duniani (potelea mbali hata kama dunia yenyewe 'sio yake') basi watuache tuishi (badala ya kudumu) maana if we live well, once is enough. Tusitamanishwe kuifikia Ethiopia maana baadaye tutaitwa WAHAMIAJI HARAMU ambao Baba Yao anamiliki Sheba Miles lakini wanasafiri ndani ya Fuso na kupoteza maisha...YaRabbi tupe moyo wa ustahimilivu au mshana jr anisaidie kugeuka msukule nisijisikie vibaya kukaa 'makaburini'.
Mkuu, hongera kwa kujaliwa hekima na uelewa wa kiwango hichi. Fahari ya marehemu au mtunza kaburi?
 
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali, ambalo linatakiwa kujibiwa na wachumi wetu, Mwalimu Nyerere alituhusia "Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu na Sio Maendeleo ya Vitu". Wachumi wetu tusaidieni kutuelimisha, huu Uchumi wa Magufuli, Unalisaidia Taifa Kupata Maendeleo ya Watu, au Utatupatia Maendeleo ya Vitu Huku Uchumi wa Mtu Mmoja Mmoja Ukiangamia?.

Kama kawaida yetu kutumia the right to expression kuuliza, Jee awamu hii ya 5 ya rais Magufuli, inatumia falsafa gani ya kiuchumi?, jee uchumi huu wa Magufuli, unalisaidia taifa au unaliangamiza?. Kwa vile mimi sio mchumi, wachumi wetu, tusaidieni, tuelimisheni tunakwenda wapi?, are we heading to the right direction?.

Ili Tuendelee Tunahita Vitu Vinne, Vyote Tunavyo, Tumekwama Wapi?
Tulifunzwa, ili tuendelee tunahitaji vitu vinne,
  1. Watu-tunao
  2. Ardhi- tunayo
  3. Siasa Safi- tunayo?
  4. Uongozi bora-?
Kama vitu hivi vyote vinne tunavyo, sasa sisi Tanzania tumekosa nini?, kwa nini bado ni masikini?.

Kupanga ni kuchagua.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea.
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...
Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed ...
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza ...
NAONA SASA UMEANZA KURUDI KWENYE MSTARI! KAMA MWANDISHI MWANDAMIZI.MAANA YA MAYALA KWA KISUKUMA NI NJAA HE HE!!!
 
Hii ni moja kati ya tafakari nzuri kwa wiki hii, maendelea yatakuja ikiwa unaendeleza watu, vitu na mifumo. Yaani vyote kwa pamoja, kiongozi mzuri ni yule anayejitahidi ku strike balance. Najua zipo theories mbali mbali za ki-uchumi ambazo zinaweza kutumika ku justify maamuzi mbali mbali lakini ni lazima maendeleo ya watu, vitu na mifumo yafanyike kwa pamoja.
 
Nimemkumbuka Hon Prof Shukrani Mbiringenda (udsm) katika lectures ya "HUMAN CENTRED DEVELOPMENT "
Hakika sio Nyerere tu ambaye walibadilisha msimamo wa socio-economic systems(ujamaa policy -African sociolism,ISI policy from latin ) bali alikuwepo Kwame Nkurumah pia
Kuna transformation za economics,politics etc baada ya European kuuharibu uchumi wetu kipindi cha ukoloni na baadae kuzitambulisha sera za IMF na World Bank yaani SAPs

In short kuna haja ya kuwa na sera ya maendeleo ya taifa (bila kuzingatia vyama) ndio maana bwana mkubwa kila uchwao anatunga zake tena kwenye globalised world tutaendelea ku float sana
 
Wewe!wewe! Angalia usijeukawa mchochezi,kwani wewe huoni maendeleo yatokanayo na Tanzania ya viwanda?
 
Soma hoja ya Mwana mtoka Pabaya hapo juu. Kama unazo utaelewa ila kama hamna,basi tena!
Wewe na genge lako ndio zeroooos hivi unaanza vipi kupinga miundombinu ambapo vifo vingi vya akina mama wajawazito na wagonjwa nawakufa tu kisa barabara ni mbovu za kuwawaisha vituo vya afya au hao watu mnaowasema ni nani?

Huduma mbovu za kijamii zinatokana na miundombinu mibovu kama ukosefu wa umeme.

Nendeni kasome social economic development ndio mtajua huu upuuzi unatakiwa uongelewe vipi?

Hao watu wanapataje ajira kama hakuna miundombinu ya kusapoti viwanda? Huyo mkulima anauzaje Pamba yake usipomuwekea miundombinu bora ya kilimo na usafirishaji?

Pathetic
 
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali, ambalo linatakiwa kujibiwa na wachumi wetu, Mwalimu Nyerere alituhusia "Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu na Sio Maendeleo ya Vitu". Wachumi wetu tusaidieni kutuelimisha, huu Uchumi wa Magufuli, Unalisaidia Taifa Kupata Maendeleo ya Watu, au Utatupatia Maendeleo ya Vitu Huku Uchumi wa Mtu Mmoja Mmoja Ukiangamia?.

Kama kawaida yetu kutumia the right to expression kuuliza, Jee awamu hii ya 5 ya rais Magufuli, inatumia falsafa gani ya kiuchumi?, jee uchumi huu wa Magufuli, unalisaidia taifa au unaliangamiza?. Kwa vile mimi sio mchumi, wachumi wetu, tusaidieni, tuelimisheni tunakwenda wapi?, are we heading to the right direction?.

Ili Tuendelee Tunahita Vitu Vinne, Vyote Tunavyo, Tumekwama Wapi?
Tulifunzwa, ili tuendelee tunahitaji vitu vinne,
  1. Watu-tunao
  2. Ardhi- tunayo
  3. Siasa Safi- tunayo?
  4. Uongozi bora-?
Kama vitu hivi vyote vinne tunavyo, sasa sisi Tanzania tumekosa nini?, kwa nini bado ni masikini?.

Kupanga ni kuchagua.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea.
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...
Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed ...
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza ...
MUUNDOMBINU BORA UNAYO NAFASI CHANYA YA KUWAJIBU WATANZANIA WENGI KTK MADHIRA WALIOMO SASA IN A LONG RUN....NANI AFANYE HILO AMBALO KWELI SASA NI SO EXPENSIVE KWA WANANCHI....LAZIMA WAWEPO WA KUJITOA SADAKA FOR TOMORROW GREATER CAUSE ......

KILIMO BILA BARABARA HAKINA MAANA INGAWA NAPINGANA NA FLY OVER YA UPANGA MASAKI BUT STILL ROADS AND RAILS ARE SUPPOSED TO BE RELIABLE ENABLERS KTK KUKUZA UCHUMI WETU MTU MMOJA MMOJAAA....BARABARA HIZI MKULU AZISOGEZE SONGEA RD VIA IFAKARA MALINYI....MLIMBA KILOLO NA KADHALIKA HAPA DSM ATANUE HII MWENDO KASI NA KUFUNGUA HUB YA CHALINZE DSM ...CHALINZE MORO -DODOMA...LAKINI SASA VIJIJINI WATU WAIONE LAMI......WAONE UMEME....

KILA LA HERI
 
njia tunayopitia ni sahihi kabisa.
yoyote mvumilivu, akiwepo mwenye kuona mbali, Atayaona maendeleo ya watu yanayoliliwa nyuma ya kinqchoendelea sasa.
wanachokililia wengi ni maendeleo ya watu ya pupa na volatile ili wapate furaha ya muda kitambo bila misingi yoyote.
 
Back
Top Bottom