Je, maandamano yataruhusiwa siku za kuchukua na kurejesha fomu wagombea wa Urais?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,874
Mwaka 2015 tulishuhudia usumbufu wa kiwango fulani hasa wakati wa kurejesha fomu kwa wagombea wa urais, barabara zilifungwa na baadhi ya shughuli kulazimika kusimama.

Safari hii zoezi hili linafanyikia Dodoma na kuna chama kimeshawatangazia wafuasi wake " watata watata" kuwa mgombea wao atatimba Dodoma siku ya nane nane kuchukua fomu, ndio nauliza maandamano yanaruhusiwa?

Eti wenyewe wanapaita Dodoma golgota, Ufipa bhana.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwani sheria ipo ambayo inakataza maandano, tatizo lako mshazoe kufanya mambo kiubaba, sasa unafikir ubabe nao ni sheria, na ndiyo mana mnakwama sana kwenye mambo yenu, na hiyo ndo tafaut kubwa sana kati yenu na chadema, mataga mnatumia nguvu sana basipo akili, wakati chadema wanatumia akili sana na ndiyo mana mpaka leo wamefunika kila eneo
 
Ruksa. Maandamano ya amani ruksa. Huu ni msimu wa kampeni za uchaguzi mkuu. Ruksa.
Mimi nasema sio maandamano,
Ni msafara. Kwani kunapokuwa na harusi, misiba, kumpokea kiongozi nk. Hayo ni maandamano au ni msafara? Hivyo Chadem awatakuwa na msafara wa kwenda tume kuchukua fomu ya mgombea. Maandamano hufanyika kuashiria kulazimisha/ kupinga au kupongeza jambo fulani..
 
Yohana mbatizaji mbona mambo ya Cdm yanakulaza bila usingizi ?!.

Kila chama kina taratibu zake. After all NEC watoe muongozo ili kutoleta usumbufu
 
Mimi nasema sio maandamano,
Ni msafara. Kwani kunapokuwa na harusi, misiba, kumpokea kiongozi nk. Hayo ni maandamano au ni msafara? Hivyo Chadem awatakuwa na msafara wa kwenda tume kuchukua fomu ya mgombea. Maandamano hufanyika kuashiria kulazimisha/ kupinga au kupongeza jambo fulani..
Kumsindikiza mgombea ndio kupongeza kwenyewe bwashee!
 
Back
Top Bottom