Je, Lowassa anapaswa kuwaomba msamaha watanzania kama Uhuru Kenyatta alivyofanya kwa wakenya?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,962
141,961
Rais wa Kenya mh Uhuru jana aliwaomba msamaha wakenya wote kwa sintofahamu ya kisiasa iliyojitokeza baada ya uchaguzi. Aidha amewataka wakenya wote kuwa wamoja na kuifanya nchi ya Kenya kuwa bora zaidi.

Ndipo sasa najiuliza, Lowassa ambaye pia ni rafiki mkubwa wa Kenyata hapaswi kufanya vivyo hivyo kwa watanzania.

Ni Lowassa aliyezusha taharuki CCM kwa kutaka kulazimisha ateuliwe kuwa mgombea urais 2015 hali iliyopelekea 75% ya wanec waimbe kuwa wana imani naye.

Ni Lowassa huyu huyu baada ya mikakati yake kubuma kule CCM akakimbilia CHADEMA ambako amesambaratisha kile kilichoitwa UKAWA na sasa ameielekeza CHADEMA kibra.

Kiukweli siasa za Tanzania zimevurugika kabisa sababu ya wafuasi wa mtu huyu, Je, Lowassa hapaswi sasa kuwaomba radhi watanzania na kushiriki kikamilifu katika kuijenga Tanzania mpya yenye uchumi wa viwanda?...Ahsante!
 
hapana, wala sipanic, sasa wewe asubuhi yote hii na mvua hizi ya Lowasa wapi na wapi? Sema ya Jiwe ndiye anatawala nchi hii.... sema Jiwe aongeze mishahara! Haya ndiyo ya maana, siyo Lowasa
Anajua kama mnamuita JIWE?
 
hapana, wala sipanic, sasa wewe asubuhi yote hii na mvua hizi ya Lowasa wapi na wapi? Sema ya Jiwe ndiye anatawala nchi hii.... sema Jiwe aongeze mishahara! Haya ndiyo ya maana, siyo Lowasa
Tunaimarisha uchumi kwanza then automatically mishahara itaanza kupanda bila kusubiri Mei mosi!
 
Tunaimarisha uchumi kwanza then automatically mishahara itaanza kupanda bila kusubiri Mei mosi!
You are too ambitious with no direction. Hakuna nchi ya kiafrica ilifanya biashara ya abiria wa ndege ikapata faida! Uchumi upi mnajenga wakati viwanda vinafungwa, wawkezaji wamekata tamaa etc... kilimo ndio kimekufa kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Rais wa Kenya mh Uhuru jana aliwaomba msamaha wakenya wote kwa sintofahamu ya kisiasa iliyojitokeza baada ya uchaguzi. Aidha amewataka wakenya wote kuwa wamoja na kuifanya nchi ya Kenya kuwa bora zaidi. Ndiposa najiuliza, Lowassa ambaye pia ni rafiki mkubwa wa Kenyata hapaswi kufanya vivyo hivyo kwa watanzania. Ni Lowassa aliyezusha taharuki CCM kwa kutaka kulazimisha ateuliwe kuwa mgombea urais 2015 hali iliyopelekea 75% ya wanec waimbe kuwa wana imani naye. Ni Lowassa huyu huyu baada ya mikakati yake kubuma kule CCM akakimbilia Chadema ambako amesambaratisha kile kilichoitwa UKAWA na sasa ameielekeza Chadema kibra. Kiukweli siasa za Tanzania zimevurugika kabisa sababu ya wafuasi wa mtu huyu, Je, Lowassa hapaswi sasa kuwaomba radhi watanzania na kushiriki kikamilifu katika kuijenga Tanzania mpya yenye uchumi wa viwanda?...ahsante!
ni lowasa aliyesababisha baraza/serikali isivunjwe mpaka baada ya uchaguzi.
ni lowasa aliyepata kura nyingi kuliko aliyetangazwa mshindi.
ni yeye aliye sababisha komputer za kuhesabia kura zikaibwa na mapolisi pale haki za binadamu.
huyu ndio aliyesababisha UKAWA/ cuf kuwa na wabunge wengi bara kuliko wakati wote.
ni yeye aliyesababisha kupigwa marufuku mikutano ya hadhara na bunge live.
 
You are too ambitious with no direction. Hakuna nchi ya kiafrica ilifanya biashara ya abiria wa ndege ikapata faida! Uchumi upi mnajenga wakati viwanda vinafungwa, wawkezaji wamekata tamaa etc... kilimo ndio kimekufa kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Faida siyo lazima itoke kwa abiria na mizigo bali ndege hizo ni bango la vivutio vya utalii huko duniani. Mkuu usikariri kama mhasibu utadumaa!
 
ni lowasa aliyesababisha baraza/serikali isivunjwe mpaka baada ya uchaguzi.
ni lowasa aliyepata kura nyingi kuliko aliyetangazwa mshindi.
ni yeye aliye sababisha komputer za kuhesabia kura zikaibwa na mapolisi pale haki za binadamu.
huyu ndio aliyesababisha UKAWA/ cuf kuwa na wabunge wengi bara kuliko wakati wote.
ni yeye aliyesababisha kupigwa marufuku mikutano ya hadhara na bunge live.

kaua ukawa mkuu

kaua upinzani

mjifunze kuwa wakweli
 
Yeye kutekeleza haki yake ya kikatiba na kidemokrasia imekuwa kosa ati aombe radhi? yeye kutoka chama kimoja kwenda kingine ama yeye kutaka kuchaguliwa ama kugombea kwa tiketi ya chama fulani wala hakupaswi kuombwa radhi, labda kama hatujui dhana ya mfumo wa vyama vingi ni ni nini?
 
kaua ukawa mkuu

kaua upinzani

mjifunze kuwa wakweli
kauwa ukawa na upinzani ndio lakini mbona wapinzani wanakamatwa kamatwa? kura ziliibiwa pale kinondoni nk? unaweza kukiandama kitu kilichokufa? yeye ndio aliyemrejesha lipumbavu pale buguruni? acha kuwa na akili za kitoto wewe ukweli unaujua unashupaza kiuno na shingo tu. kama kweli kaua UKAWA . Mruhusuni akawashukuru wapiga kura wake mikoani
 
Faida siyo lazima itoke kwa abiria na mizigo bali ndege hizo ni bango la vivutio vya utalii huko duniani. Mkuu usikariri kama mhasibu utadumaa!
Eh, kwa hiyo utalii utalipa gharama za kuendesha ATCL, ndivyo mnavyomshauri! Ethiopia ingelikuwa kama Norway kama ni hivyo! Kweli Lumumba ni hasara! Ndivyo mnavyomshauri! Mna uhakika watalii watakuja? wa kutosha?
 
ni lowasa aliyesababisha baraza/serikali isivunjwe mpaka baada ya uchaguzi.
ni lowasa aliyepata kura nyingi kuliko aliyetangazwa mshindi.
ni yeye aliye sababisha komputer za kuhesabia kura zikaibwa na mapolisi pale haki za binadamu.
huyu ndio aliyesababisha UKAWA/ cuf kuwa na wabunge wengi bara kuliko wakati wote.
ni yeye aliyesababisha kupigwa marufuku mikutano ya hadhara na bunge live.
Dah..wapenda demokrasia hatutamsahau yeye na Mbowe kwa kuua demokrasia iliyojengwa kwa Zaidi ya miaka 20 ya damu na jasho...Kama si Lowasa na pesa zake za kifisadi..Tanzania ingekuwa na kasi kubwa Zaidi ya sasa....na ccm wasingekuwa na nguvu kubwa hivi ...:cool:
 
Tujifunze mazuri ya Uhuru,anapatana na safu ya juu upinzani,kisha wanaungana kujenga taifa. Laira katoa somo miongoni wasemaji Governors conf. Kenya wiki hii .Sisi huku tunaanza siasa za fitina kununua viongozi ngazi ya chini, na chaguzi za kibabe.Mzee Kinana ibuka uliko waambie polex2 na ngenge lake wanamshauri vibaya mkuu.
 
Back
Top Bottom