Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Watanzania tumekuwa tukililia sana kuwa na Tume huru ya Uchaguzi. Hivi majuzi Kenya wamefanya uchaguzi wao na karibu asilimia kubwa tumewapongeza kwa kufanya uchaguzi wa wazi kabisa na kushirikisha vyombo vya habari kwa kila hatua
Wengi wameipongeza Tume iliyosimamia uchaguzi huo. Hata hivyo tumeshuhudia dakika za mwisho kabisa tume hiyo hiyo ikigawanyika
Makamu mwenyekiti ametofautiana na Boss wake hadharani jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi kwasababu huu mgawanyiko utaenda hadi kwa mashabiki na wafuasi wa wagombea
Kitendo hiki kimenifikirisha sana. Najiuliza, hii ndo definition sahihi ya kuwa na Tume huru!?
Hivi inawezekana kumbe tukawa na Tume huru halafu ndani yake kukawa na viongozi au wajumbe huru kupita hata tume yenyewe!?
Muhimu ni kuwa na Tume huru au watu huru ndani ya tume!?
Kuwa na Tume huru Kuna maanisha watu ndani ya tume wafanye chochote muda wowote au wanatakiwa waifuate tume muda wote?
Hivi tume huru hasa ni ipi!?
Kama ni ile isiyoweza kuingiliwa na wanasiasa katika maamuzi, hii ya Kenya tuna uhakika gani huyu makamu mwenyekiti na hao wajumbe walio kana matokeo kabla hata hayajatangazwa hawana shinikizo la wanasiasa nyuma ya pazia!?
Mwenyekiti kushindwa kuzuia wajumbe wake wasigawanyike, tuamini kuwa ndo Uhuru wenyewe wa tume au tuamini yeye ndo alikuwa imara kukataa mashinikizo ya wanasiasa?
Kwa mfano hao waliogawanyika na kukana matokeo bila kutoa sababu zaidi ya kusema "wasihusishwe na hayo matokeo" baadae wakawa chanzo cha vurugu na machafuko tuamini ndo Uhuru wenyewe wa Tume?
Mwisho kabisa, nawaombea wakenya wote wayapokee matokeo na wadumishe amani! Wakiliweza hilo hakika dunia nzima itajifunza kwao.
UHURU KENYATTA atabaki kuwa nyota wa mchezo kwa kuamua matokeo kijasusi zaidi maana kibongo bongo mgombea hata wa udiwani tu aungwe mkono na Rais halafu tume isimtangaze nyasi zingechimbika kuanzia kwa mgambo kupiga virugu hadi mwenyekiti kuambiwa hajulikani alipo na amevamiwa na watu wasiojulikana.
Wakenya wakibaki na amani yao Uhuru Kenyatta atakuwa amepindua meza ya kijasusi kibabe na Odinga atakuja kushituka baadae kabisa huu mchezo uliochezwa kijasusi.