Je lipa namba za mitandao zinaenda kufungwa?

Je lipa namba za mitandao zinaenda kufungwa?

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,902
Reaction score
15,928
Kwa wale Mawakala wa Mitandao ya simu wanaotumia Lipa Namba bilashaka watakuwa wamekumbana na kashkashi za matishio ya Mitandao ya simu kuhusu . Kwa sasa mawakala kwa asilimia kubwa wamekuwa wakitumia Lipa No kwa ajili ya kutoa pesa kutokana na demand ya wateja kupata unafuu wa Makato kiasi cha kuathiri mapato ya Serikali, je inawezekana Mitandao imebanwa na Serikali kuhusu Mawakala kutumia Lipa No?
 
Njia bora zaidi ni kushusha makato ya Wakala. Ama, kuongeza malipo kwenye Lipa.

Ili gharama ziwe sawa. Vinginevyo wateja wataendelea kukimbilia penye unafuu.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Lipa namba ndio habari ya mjini tunaelekea cashless economy watafute vyanzo vingine vya mapato, kama kuwakata kodi wabunge, mawaziri na raisi wao.
Wakiamua kuongeza makato ni rahisi.. ila haitokuwa na afya... Sema lipa imerahisisha sana. Sasa hivi naona ugumu kutoa hela kwenye wallet hata ninazo..ni mwendo wa lipa hapa
 
  • Thanks
Reactions: apk
Wakiamua kuongeza makato ni rahisi.. ila haitokuwa na afya... Sema lipa imerahisisha sana. Sasa hivi naona ugumu kutoa hela kwenye wallet hata ninazo..ni mwendo wa lipa hapa
Makato ya sasa bado ni makubwa sana hasa kwa mitandao tofauti, maana hizo hela tayari zimeshakatwa Pay as you earn na kama ni mfanya biashara zimeshalipiwa kodi ya mapato, na pia tunapolipa tayari zile bidhaa zinakatwa kodi, transaction fee kama operation cost ya mtoa huduma kwa nchi maskini kama Tanzania ilipaswa isizidi Tsh 30. Hii ni kutuongezea umaskini tu.
 
Wakikata huko tutahamia selcom
Noa nataka na kifurushi ya 10500 nafanya transactions mwezi mzima
Nikizodisha limit najiunga tena
 
Back
Top Bottom