Adrian Moller
Nasikitikatika umeweka mbele upenzi na kuweka ufaham wako mfukoni.
Mkuu usinifanye niamini kwamba elimu yetu sasa imeshuka kiasi hiki.
a) Unaongea kwa kutumia elimu yako ya chuo kikuu? kama ndiyo ufahamu wako katika kuchanganua mambo umeishia hapa Taifa lipo katika hatari kubwa.
b) Unaongea kwa ushabiki? kama ndiyo basi hufai maana ushabiki mara nyingi huishia kwenye utetezi wa kitapeli na uwongo na hapa utakuwa umehifadhi akili zako mfukoni nakujifanya hamnazo.
kwa kutumia elimu yako ya chuo kikuu, hebu tufanyie uungwana nikatika lipi chadema wameteleza na walipaswa kuomba msamaha kwa uma? katika majibu yako hakikisha unabalace kwa kila kosa utaloliweka la chadema ccm wamefanikiwa vipi (Note, chadema hawamiliki dola wala kukusanya kodi-Zingantia katika mjadala wako)
Je wewe ni mmoja wa wanamipango ndani ya chadema?
Ilkuweka shauli lako vizuri weka mchanganuo wa mapato ya chadema yote na ya ya ccm yote kuanzia misaasada na ruzuku kama vyama vya siasa. Changanua mipango na matumizi kwa kila chama ilituamini kutoka uchanuzi wako kwamba CCM ni bora katika makusanyo na matumizi dhidi ya chadema.
Siku ya tukio la kifo cha mwangosi wakati chadema wanafanya mikutano yao iringa, CCM walikuwa na mkutano mkubwa sana zanzibar chini ya Ghalib Bilal. Mikutano ya chadema ilizuwiwa kwa kisingizio cha sensa.
a) Kwanini chadema walizuiwa na ccm wakaendelea jadili kama msomi tukio hili kwa uwiano wa haki kwa kila chama
b) Je kulikuwa na tishio lolote kiasi kwamba unadhani ilikuwa lazima chadema kuzuwia mikutano yao, jadili......
hapa ndipo unaponihuzunisha na kunitia aibu kwamba msomi wa chuo kikuu
a) kwa mauwaji ya mwangosi tishio ilikuwa nini na nani aliuwa?
b) Kwa tukio la bom juzi arusha, wakaazi wa arusha waliadhibiwa kwa tishio gani hasa? nani alikuwa muwaji?
c) Je ni haki na halali kuwazuia watu kuaga marehemu? nakunakifungu gani cha katiba kwamba mtanzania-mwanasiasa, mkulima, masaani nk akifa tunatakiwa kuwa na kibali cha mkusaanayiko?
a) Report ya jukwa la siasa imejitoshereza? kama ndiyo kwanini hawaendi mahakamani? umewahi kujiuliza hili swali?
b) Wanaomba tume huru iundwe nani (JM Kikwete) umeshawahi jiuliza kwanini kikwete anakwepa kuunda tume huru?
c) Lwakatale hana kesi ya ugaidi ni mbumbumbu wa elimu kama wewe mnaotuchafulia sifa ya vyuo vyetu vikuu kwa uelewa wa ovyo kama kwa chagonja.
d) Nchemba anashutumiwa na kutuhumiwa kwasababu ndiye source ya kila jambo kuhusiana na hiyo video uchwara, Je umejiuliza kwanini Polisi wanamzunguuka wala hawamhoji?
e) wewe wasema Lema jambazi lakini, umeshawahi kulipoti polisi na kuwapa ushahidi au ni ujinga wa fikra msomi
wangu?
a) Neno kukopa linamaanisha amepewa kihalali (usomi wako wa ovyo kwelikweli) amefuata taratibu kapewa tatizo lako ni umbeya na kukubali kutumika kumchafua huyu Dr.
Huu ndiyo naita ujinga, kama unaushahidi peleka polisi kuna million 100. Huoni unajiaibisha kujiita msomi wa chuo kikuu?
Hakuna aliye mkamilifu ila mungu mwenyewe, kwetu wanadamu kinachoangaliwa ni ukubwa wa makosa, mara ngapi, kwanini na kivipi tukilinganisha na pande zingine zenye mwelekeo na malengo yanayofanana. Makosa yaliyo/yaanayofanywa na ccm ni makubwa na yanatisha hivyo kufanya vijimakosa vidogovidogo kwa vyama vingine kuwa negligible/ insignificant.