Je, kwanini kuku ni wakorofi sana ?

Je, kwanini kuku ni wakorofi sana ?

chai ya rangi

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2026
Posts
1,039
Reaction score
3,084
Kuku angekua mkubwa kama n'gombe lazima tungeshika adabu kwasababu wana ubabe na ukorofi mwingi usio wa lazima.

ukiwaweka kuku pamoja lazima waonyeshane uwezo wa kupiga na anayepiga zaidi lazima aheshiniwe na bila hivo ata kua ana bonda tu wengine na muda mwingine ana bonda bila sababu.

kwa jogoo ubabe ndo mwingi kwasababu wanaweza kupigana hadi kufa. na jogoo hawapendi kuona jogoo mwingine anakaa kwa amani lazima wapigane labda moja akubali na akubali unyonge na kuishi kama digidigi.

pia wengine ubabe wao wanaupeleka hadi kwa binadamu ndo maana nikajiuliza wangekua na mwili mkubwa kama ng'ombe lazima tungepata shida kuwafuga kwasababu wangetutembezea kichapo hadi binadamu bila sababu
 
Back
Top Bottom