Je kusudi la Mungu kumuunba mwanadamu ilikuwa ni lipi kati ya haya mawili?

Ndugu, katika hayo uliotaja hakuna hata moja,.
Kusudi la sisi kuumbwa ni kuzaliana na kujaza dunia.
Hakuna jingine. Sijaona.
 
Binafsi naona Binadamu aliumbwa ili ateseke tu kisha afe.
Ni kama experiment fulani hivi...
Imagine unazaliwa then unataabika na ujana baadae unataabika na uzee (ukibahatika kuufikia).
Baada ya hapo taabu za kifo na kaburi.
Hapo bado hujagusia kugeuzwa kuni.
 
Wanajamvi habarini wote.
Mimi ninaswali ambalo linanitatiza kiimani, kama kichwa cha habari kinavyo uliza.
Hivi kusudi la mungu kumuumba mwanadamu ilikuwa ni 1. Nikufanya kazi au 2. Kumwadundu mungu.
Kwa sababu ninaposoma katika kitabu cha mwanzo naona alimuumba adamu harafu akamkabidhi bustani aitunze but kitu kinachonitatiza sikuona mahara ambapo mungu anamuagiza kuwa adamu amuabudu. Sijajua kwa vitabu vingine kutoka imani tofauti kuhusu uumbaji wa mungu.
NAHITAJI KUELIMISHWA

JINSI YA KUTAMBUA KUSUDI LA MUNGU NDANI YAKO


Bwana Yesu asifiwe nipende kukukaribisha tena katika somo la jinsi ya kutambua kusudi la Mungu ndani yako. Moja ya maswali yanayowatatiza watu wengi duniani na wameshindwa kujua ni wao kutambua makusudi ya wao kuishi katika dunia hii. Wengi wamekua wakiishi katika maisha ambayo sio yao halisi bali wamekua wakiishi kwa kuiga iga maisha ya wengine jambo ambalo ni janga kubwa kwa mkristo kua hivyo. Ila nipende kukutia moyo usikate tamaa kwa maswali uliyonayo hebu fatana nami katika somo hili mwanzo hadi mwisho na nina Imani kua utapata kitu kikubwa cha kukusaidia.


NINI MAANA YA KUSUDI??

Watu wengi wameshindwa kuelewa maana halisi ya maisha yao jambo liliwapekea kuishi maisha ya wengine. Ngoja nikupe maana halisi ya kusudi


KUSUDI ~ Ni wazo au lengo lililowekwa ndani ya akili yako ili liwe kama malengo ambayo kwa hayo yataweza kuongoza maishani ili kutimiza lile ambalo Mungu ameweka katika maisha yako.


Hebu tuangalie Zaidi katika Biblia inasema nini juu ya kusudi la Mungu katika maisha ya mwanadamu aliyemuumba


Yeremia 1:4;10 4 Neno la Bwana lilinijia, kusema,

5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.


Na ule mstari wa 10 10 angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.


Mungu anamwambia Yeremia kabla sijakuumba nalikujua kwa maana nyingine Mungu anajaribu kumwambia Yeremia kwamba nalitambua kabisa nilichokua nafanya pindi nilipokuumba. Ukiendelea ule mstari wa kumi hapo juu Mungu anamwambia maana halisi yay eye kumuumba yaani kusudi lake ni nini hasa kwa kumwambia Yeremia kwamba amemuweka kua nabii wa mataifa hivyo kusudi kubwa la Yeremia kuwepo duniani yamegawanyika katika sehemu kuu mbili. Kusudi la kwanza Mungu anamwambia amemuweka kua nabii juu ya mataifa na kusudi la pili amewekwa kua juu ya mataifa na kazi yake halisi ni kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.


Lakini nikwambie siri kubwa iliyofichika hapa Mungu kabla hajamweka Yeremia kua nabii wake kwa mataifa kulishakua na kusudi ambalo Mungu alilokwisha kuliweka kabla ambalo aliliona kabisa halitaweza kufanikiwa pasipo kumuumba mtu ili alitimize.


Hivyo basi tambua kabisa kabla Mungu hajakuleta hapa duniani alikwisha kuumba kusudi lako ili uweze kuishi kwalo. Yaani wewe kuishi kwako sio kwa sababu ya kitu kingine ila unaishi duniani kutokana na kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako. Kwa maana nyingine ni kama hakuna kusudi hakuna mtu pia, maana Mungu hawezi kumuumba mtu bila kuweka kazi yake kabla ya kumuumba


KUWEPO KWAKO NI KWAAJILI YA KUSUDI AMBALO MUNGU ALILIUMBA HATA KABLA YAKO WEWE KUUMBWA; PASIPO KUSUDI HAKUNA MTU.

Nipende pia kukwambia kua Mungu alimpa Yeremia uwezo hata kabla hajazaliwa ili aziangushe falme na huu uwezo si kwa ajili ya Yeremia ila ni kwaajili ya kusudi la Mungu. Jifunze hapa kuwa upo uwezo ulionao juu ya maisha yako si kwa sababu Mungu alikupa ili uwe wako ila ni kwaajili ya kusudi lake kwa maana Mungu hawezi kumpa mtu kusudi pasipo kumpa uwezo na mamlaka juu ya falme na mazingira anayoishi


TAMBUA NDANI YA KUSUDI LAKO UPO UWEZO NA MAMLAKA YA KUAMURU NA KUBADILISHA MAZINGIRA PINZANI JUU YA MAISHA YAKO NA HII SI KWA SABABU YA WEWE MWENYEWE ILA NI KWAAJILI YA KUSUDI LAKE MUNGU MWENYEWE.

Ngoja nikwambie kitu tambua kwamba mazingira unayoishi hata kabla hujazaliwa Mungu alishapanga uwepo hapo ili kufanikisha mpango wake mahali hapo.wengi wamekua wakiogopa mazingira wanayoishi kwa kuyaona ni magumu nipende tu kukwambia kwamba kukimbia mazingira unayoyaishi sasa sio njia ya wewe kufanikiwa bali ni kukimbia kusudi na majukumu ambayo Mungu alikuumbia kwayo.

Mungu alifahamu kabisa mazingira ambayo atakuweka kwamba utakutana na falme na ngome za adui, anaelewa mapepo, vita ambavyo utapambana navyo, mapepo ambayo utambana nayo lakini nikwambie kabisa ni lazima ushinde iwapo utajifunza kuishi na kukaa ndani ya kusudi la Mungu haijalishi majaribu ni makali kiasi gani ila mwenye kusudi unao upako ndani yake hata kabla yay eye kuumbwa maana lilianza kwanza kusudi la Mungu ndani yake hata kabla yake, hivyo ndani yako ipo nguvu na uwezo ambao una uwezo wa kutosha kupambana na kila aina ya changamoto unazopitia.

Hebu anza kujiangalia sasa kwa upya tena katika maisha yako, vitu vinavyokuzunguka, vita pamoja na mapambano ya Ibilisi unayokumbana nayo kila siku hayataweza kukushinda ila utayashinda wewe, hayataweza kukumaliza bali utayamaliza wewe kwa sababu upo kwenye kusudi lake.


JINSI YA KUTAMBUA KUSUDI LAKO

Pamoja na yote hayo niliyokufundisha apo awali hayataweza kukusaidia vizuri kama hadi sasa hujajua kusudi la Mungu juu ya maisha yako. Tunapokuja katika swala la kutambua kusudi lako sio kazi rahisi sana, wengi wetu wamekua wakifanya kila aina ya huduma lakini bado wanaona wanapwaya, wengine wamejaribu kufanya biashara lakini bado wanapwaya, kila wanachojaribu kukifanya katika maisha yao wanaona bado kuna kitu kinawadai ambacho bado wanatakiwa kukifanya (kusudi) lakini pamoja na jitihada zao zote bado wameshindwa kujua ni nini hicho ambacho kimekosekana kwao

Wengine wanaona kupata pesa pamoja na mafanikio ndio kujua kusudi lako kwenye maisha yako kitu ambacho si sahihi. Ngoja nikwambie pesa na mafanikio ni matokeo ya ujira baada ya mtu kufanya kazi Fulani aliyopewa. Hivyo huna haja ya kujisumbua sana juu ya hayo hebu anza sasa kutimiza kusudi lake kwanza ndani yako alafu utaona kama mungu hatalipia kusudi lake

KAMA UKITUMIKA KWA UAMINIFU JUU YA KUSUDI LA MUNGU KWAKO BASI KUA TAYARI KWA MAFANIKIO MAANA KUSUDI LA MUNGU KWAKO LINALIPA KWA YULE ALIYELITAMBUA NA KULIISHI.


Ili uweze kujua upo ndani ya kusudi la Mungu ni lazima kiwango cha Amani yako kiendane na kiwango cha kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako.

Ngoja nikwambie kwamba lipo jambo umewahi kulifikiria kulifanya au tayari umekwishalifanya na ukasikia Amani ndani ya moyo wako hata kama unaliona kama dogo tambua kua hilo ndilo kusudi la Mungu kwako, na uwe na uhakika si kwamba Mungu atakupa Amani peke yake bali atakupa pia uwezo, nguvu na mamlaka ya kuweza kupambana na mazingira unayoyapitia na hajalishi ni magumu kiasi gani lakini ni lazima utayashinda maana Mungu hakuumba kusudi ndani yako ili lishindwe.


KUSUDI LAKO LINATEGEMEANA SANA NA KIWANGO CHA AMANI UNAYOISIKIA MOYONI MWAKO NA KWA LOLOTE UNALOLIFANYA KWENYE MAISHA YAKO

Je unasikia Amani kiasi gani unapofanya ilo unalolifanya sasa? Kama kiwango cha Amani yako ni kidogo kwa unalolifanya sasa au hapo nyuma basi tambua bado hujatambua kusudi la Mungu ndani yako. Anza kubadilisha sasa ilo unalolifanya sasa ambalo linakunyima Amani na fanya kile ambacho unapata Amani moyoni mwako n ahata kama kwa mazingira ya nje watu wanaweza kuliona ni dogo we jitahidi kulifanya maana katika hilo Mungu ataanza kukubariki katika hilo.

Nipende tu kukwambia zipo hatua kuu mbili ili mwanadamu aweze kufikia makusudi ya Mungu kwenye maisha yake ambayo ni kama ifuatavyo;

1. Ni lazima mwanadamu ampokee Yesu maishani mwake kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Ilo ndilo jambo kuu muhimu zaid katika maisha ya kila mwanadamu kwasababu unapompokea Yesu kwenye maisha yako huo ndio mwanzo wa wewe kutambua kusudi lako kwa maana Yesu ndiye aliyetuumba pamoja na Mungu baba (Mwanzo 1:26) sasa endapo tutarudi kwake kwa njia ya toba tutafungua mlango wa yeye kuingia ndani ya maisha yetu na kuanza kutufundisha nini kusudi lake katika maisha yetu. Kumbuka wewe hukujiumba wewe ila Mungu ndiye aliyekuumba na hakukuumba tu ila alikupa kazi na makusudi yaw ewe kuwepo ila kitu ambacho kimekupotezea kusudi lako ni dhambi unazofanya, hivyo basi hatua ya mwanzo ya wewe kutambua kusudi ni wewe kurudi kwa Mungu kwa njia ya toba ili Mungu aweze tena kukuonesha kusudi lako katika maisha yako ni lipi hasa.


Barikiwa



 
Msweet
Mungu akubari ila naomba kwenye thread inayofuata ambayo nitatoa nikikutag uje tujadiriani kuhusu MADHABAHU. Kwa nini watu wengi wamefungwa kuhusu madhabahu na je kuna aina ngapi ya madhabahu. Kama Yesu alisema yote yameisha inakuaje leo tunaugua au kupitia ktk majaribu
 
WAIDH-QAALA RABBUKA LIL-
MALAAIKATI INNII JAAILUN
FILL ARDHWI KHALIFAH,
QAALUU-ATAJ-ALU FIIHAA
MANYUFSIDU FIIHAA
WAYASFIKU DDIMAA-A,
WAQAALA - LMALAAIKATI
INNY AALAMU MAALAA
TAALAMUUN(SURATUL-
BAQARAH).
TAFSIRI: Na alipowaambia
mwenyezi mungu malaika
wake kuwa mimi nataka
niumbe mwanaadamu ili
akawe kiongozi katika
ulimwengu, malaika
wakamkatalia
wakamwambia kuwa huyo
atakwenda kufanya ufisadi na
kumwaga damu katika
ulimwengu, mwenyezi
mungu akawaambia mimi
najua zaidi ya munayoyajua.
Haya ni majadiliano kati ya
Allah na malaika zake wakati
Allah anataka kumuumba
Adam. Na kupitia uthibitisho
huu ni wazi kuwa Allah
kuwaambia malaika halikuwa
shauri na mwenyewe alikuwa
anataka kutimiza malengo
yake juu ya kuumba kiumbe
ambacho ni bora kuliko
viumbe vyote alivyoviumba,
na ili kiwe bora ni lazima
akipe hadhi ya juu zaidi kuliko
viumbe wengine, na malaika
kukataa kwao kuumbwa kwa
mwanaadamu ndio mwanzo
wa wao kujishusha mbele ya
adam kwani aya zinazofuatia
zinaonesha mwisho wa siku
Allah anawaamuru malaika
wamsujudie adam, na Ibilisi
alikataa kwa sababu yeye
alikuwa ni part of the plan,
alikuwa ni kama messenger
ambae atafuatana na adam
kuja duniani kwa kumpa
majaribu adam na kizazi
chake, na ukiangalia ni wazi
adam hakuumbwa kwa ajili
ya kukaa peponi na ibilisi
kumshawishi adam ale tunda
yote ni part of the plan, kwani
mwanzo kabisa Allah
alivyowaambia malaika kuwa
anataka kuumba adam
akawe khalifa ktk ulimwengu
ilikuwa hata adam
mwenyewe hajaumbwa. So
majibu ya maswali yako yote
kayaangalie suratul- baqara
hapo nimekupa kwa ufupi tu.
Pia nataka nitoe angalizo
kuwa mwenyezi mungu
hapangiwi na anajua
anachokifanya kuna mambo
anayafanya kwa sababu zake
na kuonyesha utukufu wake,
mungu hapingwi na amri
zake lazima zitekelezwe, na
anajua mwanzo na mwisho
wa kila alichokiumba. Back to
the topic binaadamu lazima
atambue thamani na utukufu
wake kwa viumbe vyote
kuanzia malaika, wanyama
na kila kilichomo ktk mbingu
na ardhi kimeumbwa kwa ajili
ya kumtumikia yeye, kwa
hiyo kama unataka urejeshe
ufalme wako wewe mwana
wa adam lazima utambue
nafasi yako kwanza kama
kiongozi, na hii ni kwa
wanaadam wote bila kujali
rangi, dini au kabila kila
binaadamu ni kiongozi na
anapaswa kuishi kiuongozi,
dini ni mifumo tu ya maisha
lakini mwisho wa siku
hukumu zote ni kwa mungu
alietuumba kabla ya kukejeli
imani za wenzako jiangalie
wewe kwanza imani yako
inakupa uhuru wa kuitambua
nafsi yako ya kiuongozi na
kwa kiasi gani inakupeleka
karibu na mola wako bila ya
kuwa na khofu ya viumbe
wenzako wanaokurudisha
nyuma na kukukatisha tamaa
kila siku wakiongozwa na
muovu mkuu ibilisi.
 
Lengo la Mungu kutuumba sisi halijulikani na halitokaa lijulikane. Lengo la yeye kutuumba analijua yeye.
Kuna mtu aliwahi kuandika humj kwa kutolea mfano wa mkulima na mmea wa karanga. Mkulima akipanda karanga yeye ndiye anayejua ni kwa nini amepanda karanga lakini ule mmea wa karanga hauwezi jua chochote hadi unanyauka. Ubongo wako umekuwa programed kuelewa vitu kwa ukomo. Hilo unalotaka kulifahamu wewe liko nje ya uwezo wako. Hayo mengine sijui kufanya kazi sijui kumuabudu ni sisi kujipendekeza kwetu tu.
Wewe ishi tu mzee baba.
hilo ndilo jibu sahihi .malengo ya mungu kwa viumbe vyake anayajua yeye mungu.full stop.
 
Back
Top Bottom