Je, Kusoma combination ya PCM ni sawa na kujichosha?

Kwanza nikwambie tu mkuu sasa hivi hakuna combi wala kozi yenye ajira nje nje labda millitary science monduli au polisi moshi..

Lakini kombi nyingine na kozi nyingine zote (hasa kipindi hiki cha magu) ni kupambana tu ..Kwahiyo chagua comb inayokuwezesha kupambana mfano PCM na PCB
 
Nakumbuka kwamba kombi hiyo inakupa wigo mpana wa uchaguzi kama utapenda kuendelea na elimu zaidi
 
Labda niiweke mada hii vizur ndugu zangu wa JF nimesikia maneno mengi kwa baadh ya watu ati Kusoma PCM ni kujichosha kwani suala la ajira hapa nchini kwetu ni ndoto
.
.kwa walio pitia njia hii nikimaanisha PCM naomba clarification juu ya mada hii
.Aaante
Ajira za nchi hii zinabadilika badilika mithili ya kinyonga/pweza. Soma kombi unayoweza au unapenda au inayokupa wigo mpana. Kwa mfano mtu heasabu na chemistry yuko poa lakini biology haipandi-hapo ukitaka F5 unakwenda PCM. Mwingine yeye anataka juwa engineer-hapo uruke tu na PCM. Mwingine hajui kabisa anataka aje kuwa nani-hapo unachagua combi zenye wigo mpana kwa mfano EGM, PCB au PCM.
 
Sio kweli,nchi gani hiyo?

Kuna Uzi umu jaribu kuufukua kuna madogo wanasoma Harvard university ni mapacha wote walipiga PCM ilboru
Mmoja anapiga udaktari mkuu
Nchi nyingi tu marekani n.k unaruhusiwa tu ili mradi performance yako uko vizuri wana consider biology ya o level huu mfumo wa kuangalia biology ya advance kwetu tumeuzoea
Ndo maana wewe unabisha ila nchi zingine siyo kigezo fuatilia
 
Kuna Uzi umu jaribu kuufukua kuna madogo wanasoma Harvard university ni mapacha wote walipiga PCM ilboru
Mmoja anapiga udaktari mkuu
Nchi nyingi tu marekani n.k unaruhusiwa tu ili mradi performance yako uko vizuri wana consider biology ya o level huu mfumo wa kuangalia biology ya advance kwetu tumeuzoea
Ndo maana wewe unabisha ila nchi zingine siyo kigezo fuatilia
Ni zaidi ya kweli,mkuu afatilie tu
 
Nataka kusoma PCM lakini performance yangu ya F4 ni DDC, je naruhusiwa kusoma F5 na je nitaruhusiwa kufanya mtihani wa F6 kwa matokeo hayo?
Naomba ushauri
 
Kusomea chochote??? VP kuhusu afya na kilimo ngazi ya degree?
Mkuu kuna irrigation and water resources pia kuna agricultural engineering anapiga kama kawaida upande wa kilimo .Technicians or machines operators wapo wengi tu wamepiga pcm
 
Kusoma PCM alafu ukaenda Advanced level then ufaulu college ni kweli unajichosha, Labda ukapige Education,

Namaanisha nini,
Ukifanikiwa kupasua PCM form 4 mapema sana tafuta Engineering school yoyote ukapige Diploma (NTA LEVEL 4,5 &6) hapo ndio utakuwa umewini kwa wakati huu,

PCM ukienda nayo advanced unakuwa umesoma mavitu mengi sana, alafu utakapo kuja kwenda degree zitakuwa hazikusaidii kitu,

Ofcn tuna Civil engineers kutoka UDSM hawa ndio mfano wa hiyo mada yako, hawa jamaa ni poor sana kwenye attendant ya IN SITU, wao wanajua theories tu,

Ila kutana na mtu kutoka MUST, ATC, DIT hawa wanakuwaga vizuri hata wakiwa diploma tu, kwasababu wanasoma Math in practically na Physics in practically,

Nakosa mda wakukupa data kwa kina ahsante
 
piga pcb ,pcm michosho kipind iki utaishia kusoma computer science tu,piga pcb inauwanja wa ajira za uhakika
 
HV huwa mnasomaje wazee??

Mie niuavyo kabla ya kuwaza ajira mbele nilichagua combination ambayo NAIPENDA,NAIWEZA,NA NAHIMILI VEMA

nilipo maliza form4 hata ningeshikiwa bunduki nisingeWEZA WALA NISINGE FAULU COMBINATION YEYOTE YENYE HISTORY NA geography MAANA NI SERIOUS NILIKUWA SIYAWEZI NA SIYAPEND


Sasa mkuu HV utasomaje kitu usicho kipenda si mateso hayo yakujitakia??

Ndio nyie mnao kuja mtaa kueahadhisia watoto kuwa HESABU NGUMU,ENGINEERING NGUMU NK

KUMBE KILA MASOMO NA WABABE WAKE


BINAFSI NAWAPA SALUTE SANA WATU WANAOSOMA MASOMO NILIOJITAIDI NIWEZE ILA NIKAWA BADO NASHINDWAA TENA VIBAYA SANA
 
Leo ni mwaka wa tatu serikali haijaajiri daktari au nesi,unaleta habari za vijiweni,kuna madaktari manesi wengi tu wako mtaani wanasaka ajira kama kada zingine
Acha uwongo madaktari wameajiriwa japo sio wote waliohitimu.
Maafisa tabibu na manesi kwa ngazi ya diploma na cheti pia wameajiriwa japo sio kiasi kikubwa kama tulivozowea.
 
Mimi nilisoma PCM na sijawahi kukaa kijiweni. Issue sio PCM...issue ni kichwani kwako kukoje. Kama umeanza hofu mapema huku ukiwazia ajira wakati hata form V yenyewe hujaanza, kuna shida.
 
Back
Top Bottom