Je kuna wenye upendo uliotukuka

Je kuna wenye upendo uliotukuka

QEEN ADEMU1

Senior Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
134
Reaction score
324
Kuna baba mmoja alihukumiwa kifo asile hadi afe.

Binti yake tu aliruhusiwa kwenda kumuangalia gerezani.

Masiku yalisogea bila yule baba kufa. Watawala wakajiuliza kwanini hafi wakati hali chakula?

Yule binti yake alikuwa akikaguliwa sehemu zote ili asiwe anampelekea baba yake chakula lakn yule baba aliendelea kuishi.

Ikabidi yule binti achunguzwe akagundulika alikuwa ananyonyesha. Kumbe kila alipokwenda kumtazama baba yake gerezani alikuwa akimnyonyesha ziwa baba yake ili apate kuishi.

Akashtakiwa kwa kosa alilofanya na hukumu yake ilibidi iwe kifo.

Hakimu akabatilisha hukumu na kuamuru yule binti na baba yake waachiwe huru na kumwambia yule binti;

"Upendo wako kwa baba yako haujapata kutokea nenda kamtunze baba yako." Watu Hufa Upendo Huishi

Tuache kujisahau unanua jinsi ya sh 60, 000, baba yupo kijijin shati limechanika ...suruali ina miaka ile ile ww upo mjini tu unapost mipicha insta fb ..unategemea baba akuoende hata kijisimu hujamnunulia

Dada zangu na nyinyi mkichuma majanga mnarudi kijijini sasa kwenda kuwasumbua wakufunge pampasi ...ukisubiri siku zifike baba na mama walipo kuwa wanahitaji msaada hukufika kuwaona

Tuwapende wazazi wetu huu ni mwezi wa kushooo love # anza na wazazi kwanza halafu maliza na beby nikwambie kitu ....mjibu tu sina kitu
FB_IMG_1578077232138.jpeg


Sent using i phone x
 
Mimi nilidhani unatafuta mume mwenye upendo wa dhati!🙇🙇🙉😚😚😒🚶🚶🚶🚶
 
Mimi nilidhani unatafuta mume mwenye upendo wa dhati![emoji144][emoji144][emoji86][emoji9][emoji9][emoji19][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
Hahaaha unawaza ngono tu , mume ninaye tena kishoka haswaaa

Sent using i phone x
 
Back
Top Bottom