Je, kuna uwezekano hapo

Je, kuna uwezekano hapo

Amon Lisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2018
Posts
464
Reaction score
1,169
Wakubwa shikamooni, wadogo zangu mambo vipi?

Ndugu zangu nimekuja tena baada ya kuingia mtaani kupambania kombe

Nakumbuka mara ya mwisho nilipitia msoto mkali sana nikaja humu kwa ushauri na msaada wowote nilimwagiwa matusi hadi nikajichukia ilibaki kidogo nijiondoe kwasababu sikuona thamani ya kuishi ukizingatia sina wazazi na kuzaliwa kwenye umaskini anyway Mungu ni mwema nipo hai

Leo nimekuja hapa kuomba msaada wenu kutokana na mishe niliyobahatisha imesimama na hatujalipwa bado tunapigwa kalenda huku unadaiwa kodi na bill zingine napata depression kubwa kwasababu hata kula changamoto ni mateso ngumu mtu kuelewa ila ndio uhalisia wangu

Hivyo ninaomba ndugu zangu mnipe mchongo
Mimi ni kijana muaminifu na mpambanaji pia nilipata bahati kufika chuo kikuu mlimani ila course niliyosomea ( psychology) sijapata ajira, kwa mwenye kuwa na msaada wa kazi iwe kuuza duka, part time jobs, biashara na zingine nipo tayari.
Nipo Kilakala Dar es Salaam
 
Pole sana mkuu

usikate3 tamaa ingali unaishi bado una lengo la kutimiza
 
Back
Top Bottom