Je, kuna ulazima wa kutoa pesa ya chakula kwa wakwe kama hujaamua?

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,774
3,460
Habari za majukumu wakuu..

Nimekuja na swali langu hapa ambalo limetokana na mke wangu..
Ishu ni hivi..

Wife nimemwambia sikukuu inakaribia na mishahara hatuwezijua itatangulia au sikukuu ndo itatangulia?
Nimemwambia ikiwa bado siku moja nenda benk katoe mahitaji watumie nyumbani na kwa bibi yangu mzaa mama (maana anajitegemea).

Sasa alichonijibu ni kwamba "Inamaana nyumbani kwetu hakuna thamani?" Sijamjibu kitu chochote..
Ifahamike kwamba nyumbani kwao ana mdogo wake anajipata tena sana. Maana ni mfanya biashara na ana uwezo wa kulisha nyumbani kwao na pia bado hajaowa..

Na lingine ana kaka yake ni mfanyakazi wa serikali na pia hajaowa na anajipata.. Sasa mimi kinachonikera mimi nihudumie nyumbani na kwangu na istoshe nihudumie na kwao ilihali ndugu zake wana kipato kunizidi mimi?

Hapo wakuu hili limekaaje? Nasubiri michango yenu sijakataa kutoa kwao ila kawa na haraka sana.. Swali hili angeniuliza pale tu ambapo alikua anaenda kutekeleza hayo.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyumbani hakuna hata mmoja anaeweza kuhudumia mimi tu ndo ninaeangaliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, haya yote naona kama unatuchosha tu. Na ninacho kiona hapo ni kwamba mkeo ana power ndani ya famila yenu kuliko hata wewe...... yaani hadi nimepata hasira ghafla, hivi kweli mimi kabisa mimi mke anijie na ushindani wa kipuuzi wa aina hiyo...... *****, kweli mkuu wanaume tunatofautiana aiseeeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, haya yote naona kama unatuchosha tu. Na ninacho kiona hapo ni kwamba mkeo ana power ndani ya famila yenu kuliko hata wewe...... yaani hadi nimepata hasira ghafla, hivi kweli mimi kabisa mimi mke anijie na ushindani wa kipuuzi wa aina hiyo...... *****, kweli mkuu wanaume tunatofautiana aiseeeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hajawahi kunishinda na wala hawezi kuwa na nguvu zaidi yangu.. Ameniuliza tu na wala sio kunikomand.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jibu ni kwamba, huyo mkeo anapenda sana pesa kuliko anavyo kupenda wewe.
Na siku ukiishiwa pesa ama ukifukuzwa kazi, hesabu tu hauna mke.


Sent using Jamii Forums mobile app
Yeye hajwahi kunipendea pesa.. Nilikuwa nae tangia sina kazi yeyote alikua mchumba na bado alinipenda na walikuepo wenye pesa wakimtaka ila alivutiwa na mimi na umasikini wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kusaidia familia ya mkeo ni sahii japo siyo lazima ni sehemu tu ya upendo kwa maana hata ukiwapelekea mchele kilo 2kwa ajili ya sikukuu siyo mbaya kwa upendo maana hapa duniani siyo lazima kumpa mtu msaada btw kwenu mama yako akiugua huwezi mwambia mkeo akamuuguze na akaenda so acha ubinafsi
 
Back
Top Bottom