Hapana, IDE ni kitendea kazi kinachokuwezesha kuandika codes na ku-run codes zako, vingine unaweza usivitumie mpaka siku utakapovihitaji, you learn as you go.
Ni kama gari, kazi yake ni kukufikisha kutoka point A kwenda point B, kuna vitu basic unatakiwa uvijue ili uweze kukaa barabarani, ndio maana ukienda kwenye driving school utafundishwa vitu muhimu ili utimize malengo (kuendesha kutoka point A kwenda point B) huwezi ukafundishwa kila kitu kilichomo kwenye gari, unavyozidi kuliendesha utapata matatizo na utajifunza jinsi ya kujinasua na kujua mengi zaidi.