Je Kuna Ukweli wowote hapa?...........

aisee we mwanajamiione kwanza SHKAOONG

mi swali langu ni huo ''muda unaopost''.....

inakuwaje unapost saa sita kasoro usiku wa giza nene wakati huo huwa nakuwa nishamaliza hata kumbembeleza SHANGAZI YAKO G?
 
Some balance is needed here...Mwanamke asiwe zuzu sana ndani, wala asiwe mkali sana...
Awe na guts kuhoji kwa busara, na si kubwatuka!
Nyumba haitakiwi kuwa ya tension 24hrs bana...yaani nikienda City-Garden na MJ1, na Acid nikute mtu kafura ka' kobe..wanini?..The thing is nampigia simu kumweleza niko mahali, thats all...!

Lakini, mind you people, heshima ndo nguzo kuu ya nyumba...Unapoona mwanamke hakuhoji kwenye mambo mambo yako yapasa ujenge heshima sana kwake, na usimwangushe kwa makusudi!
 
Ukweli upo na haupo nikiwa na maana ya kwamba katika hali au mazingira yote mawili unaweza ukawa na anecdotal situations ambazo unazijua.

Lakini ya kuwa absolute hapana maana kila uhusiano una dynamics zake tofauti.

Ila kwa mwanamke ambaye ni no-nonsense type lazima mwanaume atatanguliza heshima mbele kuliko yule aliye pushover na hivyo kupelekea kuwa na uwezekano wa uhusiano kudumu kwa sababu utajua hatakuchekeachekea ukileta ujinga.

Sijui nimeeleweka?

Kelvin nadhani wewe umenielewa hasa nilichokusudia kuandika-wengine tuna weakness katika kuexpress au explain kitu. Mara nyingi mahusiano ambayo mdada yuko strict yaani ukimkorofisha utajuta huwa wanalast longer na wapenzi wao kuliko wale wanawake wapole ambao wako ready to play by man's rule
 
Some balance is needed here...Mwanamke asiwe zuzu sana ndani, wala asiwe mkali sana...
Awe na guts kuhoji kwa busara, na si kubwatuka!
Nyumba haitakiwi kuwa ya tension 24hrs bana...yaani nikienda City-Garden na MJ1, na Acid nikute mtu kafura ka' kobe..wanini?..The thing is nampigia simu kumweleza niko mahali, thats all...!

Lakini, mind you people, heshima ndo nguzo kuu ya nyumba...Unapoona mwanamke hakuhoji kwenye mambo mambo yako yapasa ujenge heshima sana kwake, na usimwangushe kwa makusudi!

Aksante PJ haswaa nimekuelewa kabisa. Mtu mwelewa huijenga nyumba yake. Naamfahamu kaka mmoja alikuwa na girlfriend ambaye hakuwa anapenda ujinga yaani ilikuwa akimkosea yaani anapungua kilo kabla hata ya kumface nikasema hawatalast longer loh wakajaoana na mie nikiwa msimamizi wa arusi yao--- after ndoa ndo maama yangu zilikuwa zinapigwa hakuna mfano---- mdada alikuwa amejifunza ngumi huko kwenye mafunzo so yaani ilikuwa akimkuta mumewe angle ilikuwa ni vagi mpaka ikawa watu baki wakimwona jamaa yao anamisbehave wanamwambia kabisa ...hatutaki kesi.Nkajua hawatamaliza hata mwaka loh.....wanaukimbiza wa saba sasa...........
 
aisee we mwanajamiione kwanza SHKAOONG

mi swali langu ni huo ''muda unaopost''.....

inakuwaje unapost saa sita kasoro usiku wa giza nene wakati huo huwa nakuwa nishamaliza hata kumbembeleza SHANGAZI YAKO G?

Hahahahhhh TEamo.....nimekuja kumsabahi Osama huku Tora Bora bana lolh........G hajambo lakini? Namsubiri aloenda kwa wachina anletee zawadi tuje tumwone bana. Tufanye analisisi kama umefanana naye kisogo au utumbo
 
Kuna kaukweli
Mwanamke asiyetaka upuuzi mume "humuogopa" hawezi kumletea gozigozi waziwazi lakini kandokando huyo mwanaume ni mtundu kupitiliza!
Kisirisiri huwa anampenda sana mkewe lakini huo woga alio nao humfanya atafute mwanamke wa nje mwenye kumtetemekea.Kuachana hawaachani maana mume anajua huyo mamaa ni mkombozi wake kama mchungaji wa kondoo aliyepotea.

TM............hii haswa ndio maana yangu sasa najiuliza kumbe wanaume nao wanapendaga mwanamke anayewaongoza?? Maana akiwa mpole sana nahisi hapati changamoto sijui ? hata sielewi
 
Wangu akiwa mkali, nikitoka ndo sirudi. Nirudi kufanya nini wakati najua kutawaka moto?

Lukolo hata ukifanya ujinga yaani akikukuta na hali tata na akashuhudia au akajua unacheat basi asiwe mkali??........kuna mmoja aliwahisikia kuwa mumewe ana mwanamke nje (tena aliyekujamshika sikio alikuwa wifi yake yaani dada wa huyo mumewe) akafuatilia akaujua ukweli----- aligeuka mbogo, mume alilamba makofi (yeye mwenyewe alishangaa alipopata hizo nguvu)- ofcourse alimpigia chumbani kwao si hadharani. Akachoma nguo zote ambazo hazikuwa na maelezo ya kutosheleza za mumewe (ambazo alihidi zililetwa na huyo mdada kama zawadi). Kuna pesa mumewe alichukua kwenye account ya familia na ikagundulika kuwa alimpa yule mdada afanye biashara--- dada alichukua vitu vya thamani vya mumewe--- including chains, saa za maana, laptop na simu akapeleka mnadani... n.k. Mume alikuwa mpole na mpaka sasa wako wote.

But scenerio nyingine mke alikuwa mpole sana, mume akamnyanyasa akamshauri achukue mkopo benki pesa akapewa yeye akasema anajengea kumbe anatawanya na kujenga heshima bar--- mama alikuwa na gari zuri mume akamshauri wauze (,mama alikuwa ni wa yes na hakuwa akitaka kumwudhi mumewe) kumbe gari haikuuzwa alipewa hawara---- hata alipogundua alimwuliza mumewe na ushahidi akamwonyesha but akamwambia amemsamehe na anamwomba abadilike-------- ile ndoa haikulast hata three years.

Ndo mana nikawa najiuliza, so kama tulivyo sisi tunapenda wanaume ambao kidogo wanaonyesha uanaume wao kimabavu (bad boys), na nyie mnapenda wanawake aggressive?
 
MJ1..Mambo yangekuwa marahisi hivyo ndoa nyingi zingedumu kwa sababu wanawake wengi wangeamua kuwa wakali au kuwa kama askari wa kukodi ili kuwashikisha adabu waume zao. Siyo hivyo mdogo wangu. Taasisi ya ndoa iko complicated kuliko hata Ikulu ya Marekani!

Ila kuna dada yangu mmoja tulikuwa tunaongea juzi (yuko kwenye ndoa karibia 30yrs) na tumekubaliana kwa hoja kuwa kwa sehemu kubwa kudumu kwa ndoa au kutodumu kunamtegemea mwanamume zaidi kuliko role ya mama! May be right or wrong, wadau wengine wanaweza kumwaga mauzoefu yao!

DC aksante sana kaka yangu kwa post yako. Kusema ukweli umenigusa sana hapo kwenye RED............. unajua wengi wetu tunajua kuwa mjenzi wa nyumba ni mama na ndio maana kuna usemi wa mwanamke mpumbavu, huibomoa nyumba yake kwe mikono yake mwenyewe..... sasa hapo kwenye RED ningependa kupata more nyama please hebu tumegee alosema huyu dada yetu. 30 years kwenye ndoa si mchezo ati hebu atumegee kidogo tafadhali
 
MJ1,

Kwa sasa nimebanwa kidogo, lakini naomba unistue baadaye kidogo nitoe maelezo. Kwa ufupi ni kwamba wanaume ndio mara nyingi wanakuwa chanzo cha matatizo yanayovunja ndoa. Na kubwa katika hili ni ukosefu wa uaminifu. Pia wanaume wanapojifanya wababe na kutaka kuwathibiti wake zao kwa mtutu na ngumi mkononi, na kama mama ni ngangari basi hapo ndoa haiwezi kukatiza hata mwaka. Kwa ufupi, with my over 10yrs katika haya mambo, na kwa ushahidi wa huyo dadangu, ni kwamba mwanamume anachangia asilimia kubwa katika stability ya ndoa.
 
Me nakubaliana kwa asilimia zote juu ya mwanamke akiwa na msimamo na mwenza wake ndio atafanya penzi lidumu.
 
Hapa wanazungumziwa mavuvuzela au wanawake ambao ni strict?
Kuna wanawake ambao sio wapiga tumba (makelele) ila wanakua wako very strict kwa misimamo yao ya kimaisha (kijamii?)....sasa hawa nadhani ni kweli wana nafasi kubwa ya kudumisha ndoa zao......

Ukizungumzia wanawake wakali kwa maana ya kelele, sidhani kama wanadumisha ndoa zao....
 
Kakaz, dadaz, wapwaz/binamuz na Babuz...........Nawasalimu kwa upendo na amani.

Nimekaa hapa nikiwaza na kujikuta napata kigugumizi cha mawaazo.......................mara nyingi nimeshuhudia couples mbalimbali zikizaliwa na nyingine kufa wakati nyingine zikisurvive....kuna kitu nimekinote sasa sijui ni mimi au ni mawazo yangu ninaomba msaada wenu katika kunielewesha .

............Mara nyingi zile couples ambazo mwanamke huwa ni aggressive--- kwa maana ya kuwa mnoko yaani asiyetaka mchezo na penzi akupalo.......... hudumu kwa muda mrefu than zile couple ambazo mwanamke ni mpole, ambaye hata kama mwenzi wake kakosea anaogopa kuuliza au hata akiuliza kile atakachojibiwa yeye atakikubali........... mfano umechelewa kurudi nyumbani au amekukuta na sms tata.............atakaa kimya au hata kama akiuliza ukitoa maelezo yoyote atakubali tu ....... tofauti na yule ambaye ni mkali anayeweza hata kukivunjilia mbali kinokia chako.... ambao wengine hudiriki hata kurefer kwa wenzako.... mh kiafabde changu noma!!

Je kuna ukweli wowote hapa?

MJ1 elewa kuwa binadamu wote ni kama vinyonga wanabadilika kulingana na mazingira husika
 
Hapa wanazungumziwa mavuvuzela au wanawake ambao ni strict?
Kuna wanawake ambao sio wapiga tumba (makelele) ila wanakua wako very strict kwa misimamo yao ya kimaisha (kijamii?)....sasa hawa nadhani ni kweli wana nafasi kubwa ya kudumisha ndoa zao......

Ukizungumzia wanawake wakali kwa maana ya kelele, sidhani kama wanadumisha ndoa zao....

Nadhani hapo ndipo tofauti ilipo,,hao strict ndo wenye nafasi angalau ya kudumisha ndoa,,ingawa nayo isiwe sanaaaaaaaaaaa
 
MJ1,

Kwa sasa nimebanwa kidogo, lakini naomba unistue baadaye kidogo nitoe maelezo. Kwa ufupi ni kwamba wanaume ndio mara nyingi wanakuwa chanzo cha matatizo yanayovunja ndoa. Na kubwa katika hili ni ukosefu wa uaminifu. Pia wanaume wanapojifanya wababe na kutaka kuwathibiti wake zao kwa mtutu na ngumi mkononi, na kama mama ni ngangari basi hapo ndoa haiwezi kukatiza hata mwaka. Kwa ufupi, with my over 10yrs katika haya mambo, na kwa ushahidi wa huyo dadangu, ni kwamba mwanamume anachangia asilimia kubwa katika stability ya ndoa.

Aksante kaka DC...... kwa kweli najiuliza sijui wanaume wote wanalielewa hili? Maana wapo ambao hawajui kama nao pia wanachangia katika kuvunja mahusiano wengi wao blames huzirushia kwa mwanamke.
 
Hapa wanazungumziwa mavuvuzela au wanawake ambao ni strict?
Kuna wanawake ambao sio wapiga tumba (makelele) ila wanakua wako very strict kwa misimamo yao ya kimaisha (kijamii?)....sasa hawa nadhani ni kweli wana nafasi kubwa ya kudumisha ndoa zao......

Ukizungumzia wanawake wakali kwa maana ya kelele, sidhani kama wanadumisha ndoa zao....

Aksante Babu RR hapa nazungumzia wale walio strictly yaani yule ambaye ukimkosea awezalala na kisu chini ya mto akikusubiri- au kukufungia njema na ukamwelewa kwa kuwa ni kweli umemkosea sana.......................... yule ambaye akikuta ujinga kwenye simu yako na ukashindwa kuutetea anaikutanisha na sakafu au ukuta mchezo unakwisha.

Vuvuzela mara nyingi huwa si strict...........sometimes hupuliza hata pasipohitaji filimbi
 
Me nakubaliana kwa asilimia zote juu ya mwanamke akiwa na msimamo na mwenza wake ndio atafanya penzi lidumu.

Aksante meddymjili .........nadhani hata kwa wanawake hawapendi mwanaume aliye mpole sana ambaye hawezi hata kudefend maslahi yake. Ingawaje tupo wale ambao tunakwenda kwenye extremes .....yaani tunachagua wale ambao ni strict kupitiliza na wagomvi "Bad Boys"
 
Lukolo hata ukifanya ujinga yaani akikukuta na hali tata na akashuhudia au akajua unacheat basi asiwe mkali??........kuna mmoja aliwahisikia kuwa mumewe ana mwanamke nje (tena aliyekujamshika sikio alikuwa wifi yake yaani dada wa huyo mumewe) akafuatilia akaujua ukweli----- aligeuka mbogo, mume alilamba makofi (yeye mwenyewe alishangaa alipopata hizo nguvu)- ofcourse alimpigia chumbani kwao si hadharani. Akachoma nguo zote ambazo hazikuwa na maelezo ya kutosheleza za mumewe (ambazo alihidi zililetwa na huyo mdada kama zawadi). Kuna pesa mumewe alichukua kwenye account ya familia na ikagundulika kuwa alimpa yule mdada afanye biashara--- dada alichukua vitu vya thamani vya mumewe--- including chains, saa za maana, laptop na simu akapeleka mnadani... n.k. Mume alikuwa mpole na mpaka sasa wako wote.

But scenerio nyingine mke alikuwa mpole sana, mume akamnyanyasa akamshauri achukue mkopo benki pesa akapewa yeye akasema anajengea kumbe anatawanya na kujenga heshima bar--- mama alikuwa na gari zuri mume akamshauri wauze (,mama alikuwa ni wa yes na hakuwa akitaka kumwudhi mumewe) kumbe gari haikuuzwa alipewa hawara---- hata alipogundua alimwuliza mumewe na ushahidi akamwonyesha but akamwambia amemsamehe na anamwomba abadilike-------- ile ndoa haikulast hata three years.

Ndo mana nikawa najiuliza, so kama tulivyo sisi tunapenda wanaume ambao kidogo wanaonyesha uanaume wao kimabavu (bad boys), na nyie mnapenda wanawake aggressive?

Mwanajamii1,

Inaonekana kama unatafuta base on how to act towards your husband/boyfriend. Usijidanganye kwamba kuwa mkali au kuwa strict ndio utapendwa au mwanaume ndio atakua anakuheshimu. Kumbuka kwamba mwanaume ndio kichwa cha nyumba. Usije ukajifanya au ukaweka ubabe kwa ili kumfanya mwanaume awe anakuheshimu na kukuogopa.

Mapenzi ya kuogopana na kuheshimiana kama mtu na bosi wake wala sio matamu kabisa. Hata hivyo, ni vyema ukaelewa kwamba kuna kiwango cha mtu kuvumilia baadhi ya tabia. Pia ni vyema kutumia busara zaidi katika kutatua mambo kuliko kutumia ubabe, nguvu ili tu kuonyesha kwamba wewe mwanamke ni strict. Ukiwa na huo ustrict sana utajikuta unaachwa na hakuna mwanaume atakaesubutu kukusogelea. Nani anataka mwanamke wa kumuabisha kwa kumpiga makofi?

Pia ukumbuke kwamba, mwanamke alie na busara hapendi vurugu wala kugombana, sifa bora ya mwanamke ni kubembeleza na kutumia busara zaidi...! Kuwa strict ni vyema lakini pia ukumbuke ukitaka kumfaidi mwanaume mfanye awe na freedom lakini sio kuwa strict kwa kufuatilia kila hatua, lasivo utaishia kufa bachelor....!
 
Back
Top Bottom