Je, kuna siri yoyote kuhusu ndoto?

THE JAGGERS

JF-Expert Member
Apr 3, 2023
444
292
Je, kuna ukweli wowote kuhusu ndoto zinazojirudia?

Wakuu uzi huu ninaouleta kwenu unahusu mengi kuhusiana na ndoto ikiwemo ndoto za kujirudia pamoja na ndoto zengine tusizozielewa zina maana gani kwani mimi pia nasumbuliwa na ndoto za ajabu nikiwa sielewi zinahusu nini.

Katika usiku wanane usiku wa kuamkia leo nikiwa katika kitanda nimejifunika blanketi, kutokana na hali ya hewa kuwa na ubaridi katika kipindi hiki cha masika ghafla ikanijia ndoto ambayo nilishawahi kuiota na hii ni mara ya tatu.

Nikiwa katika misere yangu ya hapa na pale nikafika mahali ambapo ni karibu na nyumbani sehemu ile ilikuwa na hewa safi hii ni kutokana na uwepo wa miti mingi katika eneo hilo. Mara ghafla nikaona mti ukiwa na matunda ya malimao ila cha ajabu mti huo haukuwa mlimao. Nikatamani sana kuchuma yale malimao kwani mimi huwa napendelea sana malimao hasa hasa kwenye vyakula vyangu. Wakati najitahidi kutungua yale malimao ghafla nikasikia sauti za vicheko.
 
Sauti za vicheko vitokavyo kwa wanyama juu ya miti. Wakiwemo ngedere ,mijusi nyoka hadi ndege. Nikapatwa na mshtuko nikiwa nawatazama wale wanyama ilhali kiuhalisia ninavyofahamu mjusi,ndege na nyoka hawacheki sasa mbona wananicheka? Ngedere wengine walinicheka huku wakinitupia matawi na baadhi ya majani. Kusema ukweli roho iliniuma sana mpaka ikapelekea kushtuka kutoka usingizini .
*********************
Sikujua hii ndoto ina maana gani sikulala kabisa isitoshe hii ni mara ya tatu ndoto hii hii imejirudia
WAKUU WA JF NAOMBA MAONI YENU
 
Kwa uelewa wangu hapo unaoneshwa ubadili mtaZamo wako hasa katika maswala yanayo kuingizia kipato kwamaana sio sahihi au ayataleta matokeo chanya. Ndio maana unaoneshwa unataka chungwa kwenye mnazi(kitu ambacho akiwezekani) nainaonesha ukiendelea kukaza kichwa utaaibika... Kaa chini tafakari maamuzi yako, acha shotikati, usitegemee watu sana... acha kubeti(utaniii☺
 
sawa nitajitahidi mkuu
 
Wakuu Hivi kuna muunganiko kati ya fikra ya mtu halisi na fikra ya mtu kwenye ndoto?
Yaani akili ya mwanadamu katika maisha halisi anaweza kuitumia katika ndoto mpaka kuweza kuwasiliana by each other kwa mfano
Katika maisha halisi unaweza ukasoma kitabu fulaani alafu ndotoni ukaota upo kwenye mtihani basi kuna kama connection flaani inatendeka pale
mnakuwa kama mnawasiliana au inanitokeaga mwenyewe maana naona ni ajabu sana
 
Hakuna tofauti kati ya ndoto na maisha haya( unaweza kusema ndoto ndio alisi) kifupi ni hivi, ndoto ni kiroho na ndio ulimwengu alisi... kwasababu wewe(mtu) ni roho... na ndio maana unaweza kuta mtu ni kipofu akakwambia nimeota nachambua mchele au napika au babu amenitokea jana nikala nae n.k. upofu au ulemavu hauko rohoni bali mwilini kwasababu mwili ni nyumba ya mtu(roho) na ndio maana mkiwa mnaenda kwenye mazishi mnasema tunaenda kuaga mwili wa flani (sio roho) ,,, Ukiona umeota unapigana au unapaa, unafany mtihani yule ndio wewe(roho) kwahvo niwewe kujua inamaana gani..
notabene: nimtazamo wangu tuu sio sheria👆👆
 
Wakuu samahanini kwa usumbufu nina kaswali hapa kananitatiza kila kukicha
hivi katika maisha ya binadamu anaweza kuota mambo mfumo wa series?
maana me hunitokeaga naweza nikaota jambo leo alaf kesho au kesho kutwa pale nilipo ishia kwenye ndoto yangu inaendelea ujue naona ajabu sana alafu nakosa mtu wa kumueleza haya matukio dah
hivi hii kitu ni hutokea kwangu tu au ?
 
Back
Top Bottom