Ironbutterfly
JF-Expert Member
- Feb 5, 2023
- 3,044
- 8,165
Habari za asubuhi wanaJF, hope tumeamka salama kwa uweza wa manani🙏
Wiki kama mbili nilikuwa nasumbuliwa na ndoto za kuhusu wazee wangu (RIP, manake wote walishatangulia mbele za haki), walikuwa wananijia ndotoni wakiomba niwapatie vinywaji, sehemu nyingine niliota napeleka vyakula,wakaniomba na vinywaji, specifically soda, aliniomba Bibi mzaa mama.
Yani nilikuwa naona ndoto za kuwahusu wao na ndugu wengine walio hai katika familia. Ni wiki niliyokuwa najihisi huzuni na upweke sana bila sababu.
Basi Jumatatu nilipotoka job nikaenda kwenye msikiti wa jiran Kuna duka la dawa za kisuna nikanunua udi flan hivi huwa unatumika kuombea watu waliotangulia mbele za haki. Nikarudi nyumbani nikaoga, nikala then nikauchoma nikiwaombea pumziko hasa Bibi na mama, then kwenye saa kumi na moja nikalala,nimejiwekea utaratibu wa kulala mchana nikiwa free.
Ndani ya nusu saa toka nilale nikaota mwanamke mmoja mtu mzima kavaa upande wa kanga kajifunika Hadi kifuani, kasimama dirishani mwa chumba changu lakini kanipiga mgongo, hivyo sikumwona sura,then nikastuka toka usingizini, nikabadil upande nikarud kulala, this time kama nusu saa baadae nikaota nakabwa pumzi na mtu nisiyemwona huku amenikandamiza kichwa chini,nikawa napambana kujinasua huku nikitaja damu ya Yesu niokoe, nilihangaika kwa muda then akaniachia na nikaamka ghafla. Sikulala tena, nikaamka na kuendelea na ratiba nyingine ya kumalizia siku.
Kulipopambazuka, nikajiandaa, nikachoma udi then nikaingia mzigon, then saa 11 baada ya muda wa mkoloni, nikaenda sokon nikanunua chumvi ya mawe nikarudi home nikaipigia deki chumbani na sebuleni. Nikachoma na udi ule wa kuwaombea wazee wangu, nikaendelea na ratiba nyingine na hali ikaendelea kuwa shwari hata zile ndoto zikakata.
Kimbembe nimeamka leo nikajiandaa niende job, kabla sijatoka natafuta udi zangu zilizobaki nichome sizioni, nimekagua kote sijaziona, na ninaishi peke yangu, hii nyumba Ina usalama wa kutosha, nimebaki na bumbuwazi. Hapa nimepanga nikitoka job nikanunue za kutosha pamoja na ubani, manake hii nyumba nina wiki tu toka nihamie. Maoni yenu wadau.