Hii ndoto yangu inamaanisha nini?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,225
103,839
Hii ndoto nimetoka kuiota hivi punde saa 10 hii ya usiku.

Nimeota nipo masomoni sekondari. Baadhi ya watu niliota kuwa nao katika mazingira ya shule ni madogo tuliowahi kusoma nao mimi nikiwa Advance wao wakiwa O-Level, wengine ni mdogo wangu wa kike mtoto wa Mama Mkubwa ni mtu mzima na maisha yake. Mwingine ni jamaa yangu tulisoma naye chuo kikuu zaidi amebaki kuwa jamaa yangu sana mpaka leo. Huyu ijumaa niliwasiliana naye kupeana mitikasi maana amenizidi uwezo wa mafanikio.

Sasa pale shuleni kulitokea msiba kuna mwanafunzi alifariki. Ule msiba ulikuwa chini ya usalama wa taifa ilisemekana kuna tukio dogo kafanya ikabidi usalama wamdhibiti. Kwa hiyo pale shule palijaa usalama kila kona.

Tulikuwa tunajua aliyefariki ni dogo fulani, lakini ghafla marehemu akajifunua kwenye shuka ikawa siyo yule tuliyeambiwa,kumbe ni dogo mwingine. Tukiwa pale kwenye jeneza marehemu ananyanyuka na kuzua taharuki.

Pale pale msibani yule mdogo wangu akanipa simu yake(nimesahau alinipa ili kufanya nini). Baadae kidogo nikawa na yule jamaa yangu niliyesoma naye chuo, tukawa tunapiga stori na washikaji.

Ghafla nikashtuka toka kwenye ndoto kuchek simu ni saa 10.40 asubuhi. Nikafikiria kuandika hii ndoto. Kidogo tu nikasikia alarm ya gari nje,nikachukua upinde na mshale na panga kwenda sitting room. Kumbe kulikuwa na kibaka kafungua mlango wa gari.

Kutaka kufungua mlango kibaka akaruka fensi akakimbia. Nikatoka nje kufunga mlango na gari. Nimemsikilizia pale sebuleni, bado kimyaaa nadhani amesepa.

Hii ndoto ina maanisha nini?
 
Nikupongeze kwa kuiandika. So far hiyo ndoto haina maana yoyote. Subiri kama ikijirudia ndio tunaweza fikiria mara mbili mbili.

Angalizo: watakuja kukudangaya na kukwambia kuwa kuota ndoto ya secondary ni ishara ya kurudi nyuma kimaendeleo. WAPUUZIE
 
Hii ndoto (similar na hii yako) imejirudia kwangu zaidi ya mara 100 for the past 15 years, najua ina jambo. I AM YET to learn
 
Mara nyingi ukiwa unafanya Uzinzi Basi utaota ndoto Ambazo Hazina maana

Tafsiri. Sahihi ya ndoto yako ni kuwa unaishi katika uchafu (Uzinzi) so roho chafu za watu uliogonoka nao zinaishi na wewe
Njia ni kufanya Deliverance
 
Back
Top Bottom