Je, kuna siri gani kati ya siasa na matajiri wa Tanzania?

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Habari za kushinda wakuu,

Je, ushawahi waza kati ya siasa na utajiri? Na kwa nini matajiri wengi wa Tanzania wanaingia katika siasa.

Asilimia kubwa ya Matajiri wakubwa Tanzania washawahi kuingia kwenye siasa au wapo tayari kwenye siasa. Je, kunanini kwenye siasa? Licha ya hayo yote matajiri si kwamba wanaingia kwenye siasa tu, bali wapo chama kimoja yaani CCM

Kwa nini wanaingia CCM nasi vyama vingine?
Hapa kunaweza kukawa na sababu nyingi sana.
1- matajiri wanaingia CCM ili wasisumbuliwe (Yaani kua free na Biashara) Hapa inaonyesha Endapo ukiwa chama tawala issue ya kusumbuliwa na serikali ni mdogo sana sababu wao wapo serikalini na serikali ndio inawaandama wao. Hivyo hawawezi kujiandaa.

2- kwa shauku ya kwamba ndani ya CCM watapata pesa zaidi
Hii nayo inaweza kua sababu ya kuwafanya wawe ndani ya chama tawala sababu chama hicho kinaweza kua kinatoa tender mbalimbali na wao kuchukua nafasi kwa mfano matangazo ya chama, uzalishaji wa bidhaa zake na tender mbalimbali.

3- CCM huwalipa zaidi ya vyama vingine
Pengine hilo nalo linaweza kua sababu ya wao kua upande wa CCM Bila shaka CCM ni chama chenye pesa kati ya vyama vyote vya siasa Tanzania, hivyo pengine ndani ya CCM wanalipwa na kuwafanya waipende zaidi na kua ndani ya CCM.

4- pengine nje ya CCM watakaribiwa na michango mingi ya kuinua chama. Nje ya kua CCM pengine wanahofia wakiwa chama kingine wanaweza kupatwa na ombwe la kukichangia chama ili kujiinua na kusababisha wao kua nyuma kimaendeleo.

Pia kwa nini mtu akiwa nje ya CCM hushambuliwa sana na endana akiwa CCM hatashambuliwa sana na serikali?
Pengine Matajiri wengine huingia ndani ya siasa kama silaha ya kujilinda ili serikali isimuandame.

Nini kitatokea baada ya tajiri kutojihusisha na siasa?
Je, pengine Matajiri hawataki kua sehemu ya siasa ila inawalazimu tu. Endapo tajiri ataamua kutojihusisha na siasa itamulazimu kutoka hata mkosoaji wa serikali hata kama serikali inafanya vitu kandamizi kwa sababu akifanya hivyo itazidi kufuatiliwa sana.

Je, matajiri walio kua wanadaiwa na taasisi za serikali kwa mfano TRA kwa nini akiwa ndani ya CCM ni kama hatafuatiliwa zaidi au kuingia ndani ya CCM ni mija ya kulipia madeni hayo? Au pengine kuna vipenyo vya rushwa ndani yake?

•Hapa jibu linaweza kuibua mengi sana kwa sababu tumewaona walio andamwa mwanzo kulipa Pesa za serikali wakiwa nje ya CCM lakini baada ya kuwa ndani ya CCM hakuna tena habari za madeni hayo.

Suluhisho
Najua ndani ya serikali kuna watu ambao ni wazalendo na wengine ni vyama pinzani na CCM. Hivyo wasaidie kuziba mianya na kuweka usawa kati ya matajiri wa CCM, wasio na vyama pamoja na mataji kutoka vyama pinzani
 
Ukikuwa kiuchumi utaelewa na kupata majibu ya maswali yako yote. Kiufupi ili ufanye biashara zako kwa amani na faida unahitaji connection, kwa maana ya kwenye kila sector utakayokuwa na uhitaji nao uwe na mtu anaeweza kukurahisishia mchakato kwa mfano , TRA, TBS, POLICE, DOCTOR, nk. So hawa wote ni watumishi wa serikali ambao wanatumikia ilani ya chama tawala ko kuwa against nao utawapoteza.

Pia wafanya biashara wanahitaji Ulinzi na usalama ko ukiwa tofauti na chama tawala kwa siasa za kiafrika una tangaza vita na serikali ko huwezi ukatoboa. Utafatiliwa nukta Kwa nukta na ukizubaa utapewa uhujum uchumi
 
hakika mkuu
 
Back
Top Bottom