Je, kuna penzi la milele? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, kuna penzi la milele?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tausi Mzalendo, Nov 12, 2011.

 1. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuanza penzi ni raha, kwisha kwa penzi nako raha?
  Wengi watasema ni machungu, kilio na simanzi
  hasa kwa yule ambaye bado anapenda.

  Wengi hutamani penzi liwe la milele.....
  wengi hutamani kama ni ndoto basi wasiamke ili iendelee.

  Wengine huona kama penzi lao ni njama kutoka juu!
  Wengine , wenye kupenda kuangalia mambo kwa jicho la tatu watakuambia
  Penzi lenye mwanzo, halina budi kuisha!
  Kwanini basi wengi hufikiria kuwa penzi lao litakuwa la milele?


  Je, ni vibaya uwapo mapenzini kuwazia kuwa kila chenye mwanzo hakikosi mwisho ?
  Je ni vibaya kujiandaa kwa mwisho wa penzi?
  Hebu tupe uzoefu wako ewe mwenzetu.
   
 2. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,978
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  wajua ukiwa waanza mapenzi hisia hujaa mwili kiasi cha kwamba tunatarajia mema tuu na hta chembe chembe za kuwa mahusiano yanaweza isha hayapo kabisa....mwili unafuraha sasa wewe kweli utakuwa na akili ya kuwaza mabaya...ebo!!!
  sasa kaa unajiaanda kwa mwisho wa mapenzi uju kweli hapo hujapenda...ni kwamba wewe upo kistarehe zaidi...kuchachuana tuu
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,492
  Trophy Points: 280
  napita njia. nitarudi
   
 4. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  KIPI BORA...kujidanganya kuwa hayawezi fikia ukingoni au kukubali kuwa kuna uwezekano huo?
   
 5. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,978
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kipi boro inategemea na madhumuni yako ya kuingia katika mapenzi na mpendwa wako....wewe kama unaingia kabisa ukiwa na nia ya kujuakuw mke au mume basi mwanzani kabisa utakuwa makini na uchaguzi wa huyo mpenzi.....mara nyingi mapenzi yanaisha kwa sababu watu wanakuwa wapo hapo kimwili zaidi na ulimwengu wa sasa tunaoishi unalifanya jambo la kuchachuana kitu cha kawaida na perhaps jabo ambalo lazima ujiingize kama wewe ni kijana .....hapo basi ndipo tatizo lilipokuwepo...so kuanzia mwanzoni msingi imara wakwamba haya mapenzi yaishie kudumu hajajengwa.
   
 6. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mapenzi ni taamuli * Si kila mtu hujua
  Mpendanapo kwa kweli * Bila ya kusuasua
  Penzi hua la ukweli * Mkaishi kwa murua
  Bali kwa ndumakuwili * Hufa likishachanua
  Mapenzi ni pande mbili!

  Sumu ya pendo maudhi * Iwapo yatatokea
  Au kama halikidhi * Lile ulotarajia
  Na mwengine kutoridhi * Maovu kumtendea
  Ingawa kuna baadhi * Waweza kuvumilia
  Mapenzi ni pande mbili!

  Mpende akupendae * Shauri langu natoa
  Yule akudanganyae * Huyo hapendi tambua
  Ya nini kukaa nae * Akutese ukijua
  Tafuta akufaae * Kupanga ni kuchagua
  Mapenzi ni pande mbili!
   
 7. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 837
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Lipo penzi la milele nalo ni la Bwana Yesu tu! Penzi lake ni la Alfa na Omega.
   
 8. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mzabzab na wewe!!
  Hebu edit kidogo basi ili tukuelewe.....nashindwa hata kukuuliza maswali
   
 9. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hakuna penzi la milele leta thread ingine
   
 10. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Hapa imetulia...
  huu ni upendo wa AGAPE na siyo 'mapenzi'.......nazungumzia zaidi ya huu ...ikiwemo EROS
   
 11. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Nimekumbuka wimbo wa afande Sele, wanaimba mambo yasiyo na maana, na yenye maana hayana vina.........lol! Ila jitahidi unaweza ukafanikiwa, haya mambo yana wenyewe mkuu
   
 12. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Lipo kwa mwenye bahati bana!Kama una bahati yako unaweza kulibahatisha.
   
 13. M

  Munira Member

  #13
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Penzi la dhati km lipo lipo kwa upande 1,kwa maana kuwa unaweza ww ukawa unampenda m2 kwa dhati lakn yy hakupend hvyo na kinyume chake.
  penzi la dhat kwa wote wawili camin uwepo wake.
   
 14. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #14
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  hakuna penzi la milele bibie,sometime kuvunjika kwa penzi ni raha ili kujiepusha na mibalaa ambayo ungekumbana nayo kwake. Nalog off
   
Loading...