Je, kuna Mungu ? Part 6 (Kuumbwa kwa Kaalam)

Salim A. Msangi

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
566
511
Tunaendelea …

Tuliishia kwenye kuumbwa kwa Arshi Tukufu.

Mtume Mtukufu Muhammad (saw), anatufundisha kuwa, baada ya Arshi tukufu, kilicho fuata ni. Kaalam(Pen).
Mtume wa Allah (sw) alipozungumza kuwa Allah (sw), aliiumba Kalaam, aliendela kusema kuwa, wakati Kaalam inaumbwa, Arshi Tukufu ilikuwa juu ya Maji! Hivyo wanazuoni wanachukulia kwamba, Maji yaliumbwa kabla ya Kaalam, na hili halina shaka kabisa, kwenye Quran ana Sunna n ahata kwenye ulimwengu wa sayansi ya leo, tunakubali kuwa kila kitu kiliumbwa kutokana na maji.

Hiyo Kaalam ipoje, ukubwa wake, wino wake, umbo lake n.k hatufaham chochote, lakini ni kaalamu tofauti kwa ufanyaji kazi wake na kalamu tunazo zifahamu.

Kaalam ikapewa amri, Kaalam ikaambiwa iandike, ni nani anaye ipa amri hiyo Kaalam? Allah (sw) ndiye anaye iamrisha Kalaamu iandike.

Kaalam ikajibu, ni niandike nini Mola Wangu?

Kaalam ikajibiwa, andika makadirio ya kila kitu, mpaka Kiyamah!

Kalamu imepewa jukumu la kuandika, kila nukta, kila kiduchu tunacho kijua na tusicho kijua, na kila kikubwa kadhalika, kuandika yote pasina kuacha chochote wala lolote, yoote yatakayo tokea, na yatakayo ahirishwa pia kutokea yoote yameandikwa mpaka kitakapo simama Kiyamah.

Mtume wetu mtukufu anatufundisha kuwa, yoyote, atakaye kufa, na haamini hili, basi huyo si katika sisi, huyo si muislam, huyo bado haja jisalimisha, amekufa kwenye Imani isyo ya kiislam.

Muhammad (saw), mtukufu wa daraja, anatuambia kuwa haya yalifanyika miaka 50,000 (elfu hamsini) kabla ya kuumbwa kwa mbingu na dunia, kabla ya kuumbwa kwa Universe zote 7!

Kabla ya huu ulimwengu tunao ujua na yote yaliyomo, ikiwemo hii dunia na viumbe vyake, kabla ya galaksi, nyota n.k havijaumba, miaka elfu hamsini kabla ya kuumbwa kwao, Allah mtukufu alikadiria kwanza! Kwenye dunia ya leo tunaita ‘Blue Print’, kabla hujajenga nyumba unafanya makadirio, uanchora ramani n.k, naye Allah (sw) kwa utukufu wake, alikadiria yote haya tunayo yaona miaka 50,000 kabla.

Kabla Firauni hajafika kwenye uso wa dunia, alisha andikwa kuwa yeye ni mkazi wa Motoni, kabla mtu ulio dondosha jani lake leo hauja fanya hivyo, miaka 50,000 kabla ya kuumbwa mbingu na aridhi ilishwa andika kuwa leo, muda Fulani, mahala Fulani, jani Fulani litadondoka, tena kasi ya kudondoka imeandikwa, na nini kitafuata baada ya jani hilo kudondoka vyote vimeandikwa. Kabla hujala ulicho toka kukila, miaka 50,000 kabla ya kuumbwa kwa mbingu na ardhi, ilisha andikwa, siku hii ya leo, utakula nini, utakula kwa nani au mahala gani, utakula kiasi gani n.k naathari zitakazo fuatia baada ya kula ulicho kulan azo zilishaandikwa, ziwe athari za muda mfupi au mrefu, nzuri au mbaya zote zilisha andikwa.

‘Hakika sisi tunajua kiasi cha kila kinacho punguzwa na aridhi kutokana nao. Kwetu kipo kitabu kinacho hifadhi yote' (50:4)
'Hautokei msiba katika aridhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika kitabu kabla hatujaumba' (57:22)


Kutaja kwa uchache sana, ila zipo aya nyingi zinazo taja hicho kitabu, ambacho mahala pengine kimetajwa kama ‘mama wa vitabu’, kila kitu kimeandikwa humo, mara ngapi moyo wako utadunda, kwa kasi ipi, mara ngapi utavuta pumzi, utapepesa jicho mara ngapi, hata ukifa kila mwili wako unapo geuka kuwa udongo nayo imeandikwa, mwili wako utaliwa kwa muda gani, kwa kasi ipi vyote vimerikodiwa kwa ‘Mama wa vitabu’.
Jina linguine la kitabu hicho ni ‘Kitabu Kilicho Hifadhiwa’, ikiwa na maana kuwa kilicho andikwa kwenye kitabu hicho, kimeandikwa, hakibadiliki, hakibadilishwi, lakini pia kitabu hicho hakuna yoyote anayekitazama, anaye kisogelea, hata Malaika hawakigusi kitabu hicho, bali Allah (sw)!

Mpendwa msomaji kuna nukta mbili hapa niziweke sawa ili tuendelee uzuri.
Allah (sw), anayo elimu ya kila kitu, ni mjuzi wa mambo yote.

“…. mjue ya kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo katika ardhi, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu”.(Quran .' 5:97)

Zipo aya nyingi kwenye Quran tukufu zinazo taja sifa hii ya ujuzi wa Mola wetu Mtukufu.
Halafu kuna hili.

"Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa”. (Quran 54:53)

"… Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa ila kimo katika Kitabu kilicho wazi”. (Quran 10:61)


Hapo kwenye ayah hizo, Mola Mlezi anazungumzia kitabu kilicho rikodiwa kila kitu humo.

Kwa hiyo Mola mtukufu ni mjuzi wa kila jambo, na lazima awe mjuzi wa yote, sababu ikiwa hatokuwa na sifa hii inamaana anayo mapungufu, naye Yu mbali sana na mapungufu wanayo muhusisha nayo. Kwa hiyo ni lazima awe na elimu na ujuzi wa kila jamba, hali, vitu, n.k, elimu yake ni pana mno, ni kubwa mno.

Kwenye falsafa ya uislam tunafundishwa kuwa, hata miti yote duniani tangua kuumbwa kwa dunia hii mpaka mwisho wa uhai wa dunia hii, ikakusanywa miti hiyo na kufanywa ni kalamu, na bahari zote zikfanywa ni wino, na mbingu zote zikafanywa ni karatasi, basi vita hivyo vitakwisha, ila maneno na sifa na elimu yake Mola wetu Mtukufu itakuwa hatujamaliza kuziandika.

Imekuwa sasa ni kawaida kwa wale wanao pinga uwepo wa MUNGU MMOJA, wanatumia dhana kwamba kama huyo MUNGU MMOJA, anajua kila kitu kwanini awachie haya yatokee, kwanini anichome motoni na mengine mfano wake hayo.

Msingi unabaki ni kwamba LAZIMA AJUE, LAZIMA AWE NA ELIMU YA KILA KITU, IKIWEMO YA MAOVU KUTOKEA AU KUTO TOKEA, NANI ATAKWENDA MOTONI NA NANI ATAKWENDA PEONI. HIYO NI SIFA YA UKAMILIFU AMBAYO MOLA MTUKUFU ANAYO KWA UKAMILIFU WAKE.

Lakini pia kama tulivyo ona kwenye posti zilizo tangulia MUNGU MMOJA, haathiriwi na kiumbe kinacho itwa ‘time’, kwakwe yeye si mpaka jambo litokee ndiyo atambue, kama ilivyo kwa viumbe wake wengine, kwake Yeye Mtukufu, yote ambayo yameshafanyika, yanayo fanyika na yatakayofanyika, kwake Yeye Mtukufu yamesha fanyika kwa ukamilifu wake.

Halafu elimu hiyo aliyo nayo MOLA MTUKUFU, akaiandika kwenye kitabu chake kilicho hifadhiwa, Mama wa vitabu vyote.
Kimakosa watu wengi wanachukulia kuwa, kwa sababu Allah Mtukufu ni mjuzi wa kila kitu, na kaandika kila kitu, basi, Yeye Mtukufu ndiye kawaandikia watu Fulani, na Fulani waende motoni, wapate majanga kadha wa kadha duniani, na dunia ikumbwe na masahibu haya na yale, na wengine weende Peponi, na wengine duniani waishi bila tabu yoyote (ingawa hii ni dhana tu, kiuhalisia hakuna asiye na tabu hapa duniani) n.k.

Ni makosa, sababu Allah Mtukufu, kama tulivyo eleza, moja ya sifa ya Utukufu wake ni UKAMILIFU WAKE, ukamilifu unahusisha pia kuwa na elimu ya kila kitu na kila jambo n.k, kwa ridhaa, kwa kutaka Kwake na kwa mapenzi Yake, akaamua kuiandika elimu hiyo kwenye kitabu chake. Je kufanya hivyo ndiyo kuna muhukumu kuwa yeye kayafanya haya tunayo yafanya kwa mikono yetu?

Binadam anapo tengeneza biadhaa au kifaa fulani, huwa anaandika kitu kinacho itwa ‘manual’, document hii inakuwa ni muhimu na mahususi kwa yule atakeye kwenda tumia biadhaa husika, moja ya mambo yaliyopo kwenye manual hiyo ni ‘Do’ na ‘Don’t’ za bidhaa husika, na maelezo ya kutosha ya kipi ukifanya biadhaa itadumu muda mrefu na kipi ukifanya hiyo bidhaa utaiharibu mara moja, na zaidi. Je ikiwa mtumiaji wa bidhaa husika akaenda akafanya kinyume na ‘manual’ inavyo elekeza; Je tutamlaumu mtengenezaji sababu alijua kwamba hiki kikifanyika bidhaa itakufa au tumlaumu mtumiaji wa bidhaa ambaye hakufuata maelekezo?

Huo ni mfano mdogo tu, kwamba mtengenezaji anayo elimu ya kutosha ya bidhaa aliyo itengeneza. Lakini hili la yeye kuwa na elimu hiyo halimfanyi kuingizwa makosani kwa uzembe na ujinga wa mtumiaji wa bidhaa.

Sasa iweje MUNGU MMOJA, MTUKUFU, yeye alaumiwe kwa makosa wanayo yafanya viumbe vyake, sababu tu Yeye Mtukufu anayo elimu ya kila kitu? Hii ni dhulma, na hatumdhulumu yoyote ila nafsi zetu.

Swali la msingi la kujiuliza ni ‘Kwanini Yeye Mtukufu anaacha haya yatokee?’ Swali hilo litajibiwa soon…

Elimu ya Allah Mtukufu kwenye mafunzo ya kiislam inatizamwa kwenye kanuni nne.

Kanuni ya kwanza ni kuwa elimu ya Allah (sw) haina mipaka ya mahali, nyakati, wala eneo, imekienea kila kitu elimu Yake.

Kanuni ya pili ni kuwa Allah (sw) akaiandika elimu Yake kwenye kitabu. Yote yaliyo kwisha tokea, yatakayo tokea, yaliyo ahirishwa na yatakayo ahirishwa yote, kabla ya kuumbwa chochote, yaliandikwa kwenye kitabu, huu ni ujuzi Wake Mtukufu.

Kanuni ya tatu ni, Maono , Amri zake na Matakwa yake Allah (sw).
Yeye kuwa ni MUUMBA wa kila kitu, lazima awe, na amri, awe na matakwa ya kutaka jambo fulani liwe, awe na amri ya kuutaka ulimwengu uwe na utokee n.k.

Kanuni hii ya tatu inagawanyika sehemu mbili.

Sehemu ya kwanza ni matakwa Yake Mtukufu juu ya ulimwengu wote, mbingu saba na aridhi zake, yaliyomo baina ya hivyo, tunayo yafahamu na tusiyo yafahamu, yote ikiwemo Arshi tukufu. Yale yote ambayo kwa maumbile yetu tunayaona ni ‘mazuri’ au ni ‘mabaya’ yote yanaingia humu.

Dunia inalizungukaje jua, mwezi unaizungakaje dunia, nyota gani itazaliwa lini, katika hali gani, nyota gani itajimeza na kutengeneza ‘blackhole’, risasi gani ikipigwa itakwenda kwa kasi gani na italeta madhara gani, na kipi kikifanyika madhara yatapungua au kuzidi, mvua itanesha wapi na lini kwa wakati gani kwa kiasi gani, kwanini haita nyesha au kwanini itanyesha kwa kiwango kikubwa au kidogo n.k.

Sehemu ya hii kanuni pia inafahamika kama sharia za kimaumbile ya ulimwengu, Allah (sw), angetaka kitu kikirushwa juu kisirudi chini, lakini kajaalia kwenye sayari yetu urushapo kitu, kinarudi, tufaha likiachika kwenye mti wake, linadondoka chini, hizo ni sharia za kimaumbile, au kwa uwazi zaidi ni Matakwa Yake Mtukufu.

Gari iki kimbizwa ka kasi hii, itamaliza umbali kadhaa kwa muda kadhaa, ukifanya juhudi kadhaa, utapata matokeo kadhaa, ukirusha jiwe kwenye kioo, lenye ukubwa kadhaa, kwa kasi kadhaa, yata tokea madhara kadhaa. Zote hizi tunaita sharia za kimaumbile, nazo zimegawika kutoka za kifizikia, kibaiolojia, kikemia, kijamii n.k. Sheria hizi zipo kwenye Matakwa Yake Allah Mtukufu, kazifungamanisha na hali, mahala, nyakati n.k.

Sehemu ya pili ya kanuni hii, ya tatu ni, Amri zake Allah (sw). Baada ya kuumba na kuweka kanuni za maumbile kwa viumbe, Allah (sw) akaweka amri zake, sharia zake, kanuni zake ambazo zinatuhusu sisi viumbe, na hasa binadam na majini, sharia hizi binadam anayo hiyari, kuzifuata au kuto zifuata, lakini njia yoyote atakayo chagua itakuwa na athari chanya au hasi kutokana na uchaguzi ulio fanya. Mfano wa sharia hizi ni kama amri ya kuswali, kufunga, kuwatendea wema wengine n.k.

Lakini kwenye kanuni hii ndogo ya pili, ni kuwa binadam au majini tukifanya baya, tunawajibishwa nalo, sababu tunayo uhuru wa kulifanya au kutofanya, na tumeshaambiwa ni baya na huenda madhara yake yanafahamika au haya fahamiki, lakini mradi tushaambiwa ni baya, kulifanya lazima tubebe athari zitokanazo na hayo matendo. Kanuni hii ndogo ya pili imelenga kujenga mahusiano yaliyo mazuri baina ya viumbe wengine, mazingira yao, na binadam akiwa msimamizi wa sharia hiz, na endapo hazito fuatwa madhara yake waziwazi yataonekana kwenye uso wa dunia, ikiwemo baharini na nchi kavu, haita ishia hapo tu, binadam atakuja kusimamishwa mbele ya MUUMBA wake na kuulizwa juu ya dhamana hii aliyo pewa na akaipuuza.

Kisha kanuni ya nne ya elimu Yake Mtukufu ni kuhusu viumbe. Vyote unavyo viona ni viumbe vyake, kaviumba Yeye mtukufu, hesabu ya viumbe
hao anayo na hitma za viumbe hao Anayo elimu yake na kwake Yeye hakuna uzito wowote wa kuyafanya na kuyasimamia haya.

…. Itaendelea Inshallah …..

Zilizo Tangulia
Part 1: https://www.jamiiforums.com/threads/je-kuna-mungu-mmoja.1632544/
Part 2: https://www.jamiiforums.com/threads/je-kuna-mungu-part-2.1633136/#post-32960579
Part 3: https://www.jamiiforums.com/threads/je-kuna-mungu-part-3.1634758/
Part 4: https://www.jamiiforums.com/threads/je-kuna-mungu-part-4.1636954/
Part 5: Je, kuna Mungu ? Part 5 (Kuumbwa kwa Arshi Tukufu)
 
Back
Top Bottom