Je, Kuna dalili za ile nyongeza ya mishahara?

Je, Kuna dalili za ile nyongeza ya mishahara?

Nyongeza ipo mwezi huu nnauhakika 100% shda inakuja anaongeza shs ngapi? Mfano anaongeza 50,000 itaongezeaje molale? Mwajiriwa unashauriwa kutafuta shughuli nyingine ili kujiongezea kipato
 
Kuwa mzalendo mkuu

dab648a8020eaf1f1fee323917463a8c.jpg
 
wakiwapandishia mshahara mtuambie ili na sisi tupandishe bei tafadhali sana
 
"Nasitisha ajira na nyongeza za mishahara kwa mwezi mmoja au mmoja na nusu HAITAZIDI MIEZI MIWILI"

Wakati huo ilikuwa ni juni 13 hata kama si mtaalamu wa hesabu lakini kwa haraka hadi ikifika sept 13 tayari imetimia miezi mitatu.

Swali langu; je mwezi huu nao watumishi wa uma wataendelea kusomeshwa hiyo namba ama watapewa increments yao kama sheria inavyosema au hapa kazi tu mafao uzeeni?

Na kama sivyo morali na ile ari ya kufanya kazi kwa moyo itakuwepo tena?

Unaruhusiwa kunitukana kama umeona nina kosa lolote.
Hapa kaz tu Kama Korea kaskazini,ukitaka nyongeza ya mishahara acha kaz nenda kajiajiri.
Hapa kaz tu
 
Suala hili linatia hasira sana..
Brain ya mfanyakazi wa tz mwezi huu iko programmed kupokea mshahara wenye nyongeza au kurejeshewa madaraja yaliyositishwa.

Isipotokea miguu itawalegea wafanyakazi, wasipostrike basi wataponda ile mbaya wengine kiwango chao cha furaha kitashuka kwa 40% au zaidi, wengine watakuwa watakuwa mafala tu kwa kuwa muda wamatazamio waliojiwekea (wa juu) utakuwa umeisha na hawawezi kutabiri tena, watalazimika kuwa wapoleee na kujishusha kiwango cha maisha waendane na hali halisi ya sasa.
Serikali fanyeni suprise kwa wafanyakazi mwezi huu watu wachangamke japo kidogo hali ni mbayaaaa....
 
Hapa nilipo nina hasira maana mtu mzima kama mimi kudanganywa kweupeeeee inauma sana.
Hujadanganywa maana unajua ukweli hapa unaongopewa tuuh..!

Silaha ni kusema basi uchukue hatua..!
 
Ni vigumu kutekeleza hayo, Kuhamia Dom, Meli bandarini hakuna, Wanywa pombe mchana wamepigwa bani, Hivyo kodi za pombe zimepungua, Gesti Nazo Wateja watapungua kwa kuhofia kukutana na askari maana wengine wanasaliti ndoa zao, Mapato ya Kodi za Gesti yatapungua, SASA WEWE UNAWAZA UPANDISHIWE MSHAHARA TOKA FUNGU LIPI LA PESA? FANYA KAZI ACHA MAWAZO POTOFU
 
Mkuu kila jambo na wakati wake. Ukifika wakati wa kuwaongezea mishahara watumishi wa uma utajuzwa. Angalau wewe una ajira na hivyo una mshahara ambao ndiyo sasa unapiga kelele uongezwe, wenzako kitaa wanasota ile mbaya kwa kukosa ajira hivyo subiri wao waajiriwe kwaza ndipo serikali ifikirie kukuongeza wewe mshahara.
 
Mkuu kila jambo na wakati wake. Ukifika wakati wa kuwaongezea mishahara watumishi wa uma utajuzwa. Angalau wewe una ajira na hivyo una mshahara ambao ndiyo sasa unapiga kelele uongezwe, wenzako kitaa wanasota ile mbaya kwa kukosa ajira hivyo subiri wao waajiriwe kwaza ndipo serikali ifikirie kukuongeza wewe mshahara.
Wapi vina panda bei
mkupuo Mimi nadai nyongeza kwa mujibu Wa sheria si vinginevyo
 
Back
Top Bottom