Je kuna combination zimefutwa kidato cha Sita?

MjombaRiziki

Senior Member
Feb 14, 2013
145
129
Wanabodi hali zenu,

Nina Kijana wangu aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana (2015). Matokeo yake ni division 3 ya point 23,alikuwa akichukua masomo ya Sayansi. Kulingana na Matokeo yake Combi inayokubali kwenye huo mchepuo wa Sayansi,ni "CBG". Sasa amenieleza kuwa Combi hii Imefutwa!

Wanabodi naomba kujuzwa kwa yule anaejua, je Habari hii ni Sahihi? Maana nashindwa hata kumuandaa kwa ajili ya pre form 5.
 
Sina uhakika Na ndio nasikia kwako....! Ngoja nifuatilie
 
waTz wengi vilaza kweli,haujui kiingereza unaandika Combi,ndo nini sasa? acha uzinguzi nenda shule.. Andika combination.
 
kuna kombi ilikuwa inaitwa SHE, ilifutwa zamani. kuna nyingine inaitwa HEE, sina uhakika kama bado ipo

Hii siyo kwamba imekuja kwa jina lingine S=Swahili, sasa imekuwa Kiswahili (K) H=History, E=English-hii sasa nafikiri ni Language (L). Kwa hiyo SHE ndiyo HKL (I stand to be corrected).
 
Hii siyo kwamba imekuja kwa jina lingine S=Swahili, sasa imekuwa Kiswahili (K) H=History, E=English-hii sasa nafikiri ni Language (L). Kwa hiyo SHE ndiyo HKL (I stand to be corrected).
uko sahihi kabisa. Kwa sasa inaitwa HKL. kabla haijafutwa wavulana wengi waligoma kusoma hiyo combi, ikabidi waibadilishe jina
 
Ni Tetesi. Katika Pita Zangu Uzumbeni (Mzumbe sec) Nilisikia students wakizitaja CBG, HGK,HGE, Na PGM. But Ngojea Verification ya Mama Ndalichako.
 
Hizo kombi hazijafutwa na hizo ni habari za mtaani tu. Kombi zilizofutwa ni zile zilizoanzishwa mwa juzi tena zilifutwa mwaka jaba kama sikosei. Kombi kama PGE(Phys,Geogr,Economics) EAM(Ecnmcs,Accounts Maths) na zingine zilizokuwa mpya
 
Duh! Jibu Ni Hili Comb Haijafutwa CBG!7
Ushauri Naona Kama Wew Mzaz Unajitahid Kumlazimisha Mtoto Aende Usayansini! Hebu Kaa Nae Muulize Nin Anataka! Sio Kumpelekesha Na Kutaka Sifa! Kumbuka Anayesoma na Kupiga Paper Ni Yeye Na Kwa Hayo Matokeo Ya Point 23 Napata tabu Kumwamin kama hapo CBG atashika Bomba!! Kumbuka Advanced Biology Ina Kitu Inaitwa BIOCHEMISTRY! Na Advanced Chemistry Ina Kitu Inaitwa ORGANIC CHEMISTRY! Bila Kusahau BAM kuna Kitu Kinaitwa Intergration! Vyote Havitak Masihala!! Mpe Uhuru Kijana Wako A Level Pazur Ila Pachungu Kam Atafel Na Kujutia Miaka 2 Aliyopoteza. THANX
 
Back
Top Bottom